Maelezo ya Wenje yamenyooka zaidi kuliko tuhuma za Lissu! Huenda Mbowe bado ni mtu sahihi zaidi kuongoza CHADEMA

Wenje anasema alimsaidia wakati Lissu hajitambui kwenda hospitali Kenya.

Jibu haya maswali hapo
Lissu angefariki ingekuwaje? Wenje angeidai familia ya Lissu hizo pesa.

Wakati Lissu yuko mahututi alijua kuwa anapewa mkopo?

Ulikuwa msaada au mkopo kwa mgonjwa aliye mahututi?
 
Wenje, Lissu na wengine ndani ya CHADEMA walikuwa wanahongwa pesa na Abdul ili iwaje??
Waache kuisumbua serikali, kuita maandamano ya kudai katiba mpya, tume huru, kupiga kelele kuhusu kuuzwa bandari, kupigia kelele utekaji, mauaji.
 
Acha hii mbuzi Wenje, ilibaki kidogo auze Kura zetu za ubunge wa Nyamagana kwa Masha
 
Sijaona contradictions katika maelezo aliyotoa Wenje lakini pia ameuliza maswali ya msingi sana ambayo ukiyatafakiri kwa fikra huru unaona anachokisema Lissu kuhusu watu ndani ya chama chake kuhongwa pesa za Abdul hakuna mashiko sana.

Abdul kuhusika na hii process ya kumlipa Lissu ndio ni contradiction yenyewe. Wangetumia normal government channels sio mambo ya gizani sababu hiyo ilikuwa haki ya Lissu.

Wewe ukiwa unadai mafao yako serikalini hutayadai gizani kutumia mtu asiyekuwepo serikali mfano kutumia mtoto wa waziri husika.

Haijakaa sawa hii process ya Wenje na Abdul.
 
Waache kuisumbua serikali, kuita maandamano ya kudai katiba mpya, tume huru, kupiga kelele kuhusu kuuzwa bandari, kupigia kelele utekaji, mauaji.
CHADEMA wameacha kufanya hivyo??
 
Kila eneo unapoona limesimama Basi jua Kuna mtu aliesimama. Ukiiona chadema Basi jua Kuna mtu anaifanya kuwa chadema.
Ukiiona polisi Basi jua Kuna baadhi wasio wa kawaida wanaoifanya kuitwa polisi.

Lisu hajafikia hatua yakuifanya chadema kuwa Kama tunavyoiona. Ni mtu tu muhimu ndani ya chama.
 
CHADEMA wameacha kufanya hivyo??
Wamepunguza makali. Hawana moto kabla ya maridhiano, baada ya Mbowe kutoka jela na kukutana na Samia.

Wamekuwa watetezi wa Samia zaidi kuliko kudai haki kwa Watanzania. Walimpa tuzo kule Moshi, akatoa milioni 150 kwa kanisa kupitia Mbowe.
 
Wakati ni ukuta.

.........Ila FAM hawezi achia uenyekiti unampa madeal mengi sana.
 
Abdul yuko katika nafasi nzuri ya kukwamua mambo ya washikaji, marafiki na ndugu zake pamoja na watu wengine wachache wanaoweza kukatana kama ilivyotokea kwa Wenje ila hayuko katika nafasi nzuri ya kukwamua mambo ya kinchi.
Akiwemo Wenje?
 
Wamepunguza makali. Hawana moto kabla ya maridhiano, baada ya Mbowe kutoka jela na kukutana na Samia.

Wamekuwa watetezi wa Samia zaidi kuliko kudai haki kwa Watanzania. Walimpa tuzo kule Moshi, akatoa milioni 150 kwa kanisa kupitia Mbowe.
Ulienda kwenye maandamano waliyoitisha CHADEMA mwaka huu?
 

I have the same opinion, baada ya kumsikiliza kwa makini Mr. Wenje, nimegeuza kabisa fikra zangu na kujua Tundu Lissu ni mtu muongo sanaaa na mropokaji sana, hana hekima wala busara, muongo kuliko shetani.

Mbowe bora aendelee kuwa Mwenyekiti wa Chadema..!! Sina shaka hata kidogo, Lissu sio kabisa.
 
Pesa gani wenje alitegemea kulipwa kwenye stahili za lisu?
Naomba ufafanuzi
 
Inategemea na wepesi wa kichwa chako kilivyo, sioni ugumu wa haya unayouliza ukizingatia suala la Lissu limekuwa mjadala muda mrefu katika nchi, ni kitu rahisi tu kuanzisha small talk inayohusiana na nchi inavyokwenda na kisha kuchomekea hilo.
Naona umeamua kujizima data au kuwa tabula rasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…