Maelezo ya Wenje yamenyooka zaidi kuliko tuhuma za Lissu! Huenda Mbowe bado ni mtu sahihi zaidi kuongoza CHADEMA

Maelezo ya Wenje yamenyooka zaidi kuliko tuhuma za Lissu! Huenda Mbowe bado ni mtu sahihi zaidi kuongoza CHADEMA

Lissu amekaa kitandani muda gani? Au unadhani Wenje alimkopesha Lissu from day one? Wenje anasema ile siku Lissu amepigwa risasi Wenje alipigiwa simu na Mbowe kuhakikisha Lissu anapelekwa Agakhan hospital lakini Wenje kwa uzoefu wake na kujuana kwake na watu wakahakikisha anapelekwa Nairobi hospital na guarantee ya kulipa aliitoa yeye Wenje
Wenje anasema alimsaidia wakati Lissu hajitambui kwenda hospitali Kenya.

Jibu haya maswali hapo
Lissu angefariki ingekuwaje? Wenje angeidai familia ya Lissu hizo pesa.

Wakati Lissu yuko mahututi alijua kuwa anapewa mkopo?

Ulikuwa msaada au mkopo kwa mgonjwa aliye mahututi?
 
Wenje, Lissu na wengine ndani ya CHADEMA walikuwa wanahongwa pesa na Abdul ili iwaje??
Waache kuisumbua serikali, kuita maandamano ya kudai katiba mpya, tume huru, kupiga kelele kuhusu kuuzwa bandari, kupigia kelele utekaji, mauaji.
 
Sasa hayo maelezo yaliyonyooka yako wapi? Labda, hata wewe huyaamini hayo maelezo yake. Wenje ni ZZK tu, hawezi kuacha fursa yoyote ya hela, namjua kwa karibu sana.

Labda nikuache na wosia wangu, ni kwamba, mtu pekee wa kumwamini katika harakati, ni wewe mwenyewe.

Ova
Acha hii mbuzi Wenje, ilibaki kidogo auze Kura zetu za ubunge wa Nyamagana kwa Masha
 
Sijaona contradictions katika maelezo aliyotoa Wenje lakini pia ameuliza maswali ya msingi sana ambayo ukiyatafakiri kwa fikra huru unaona anachokisema Lissu kuhusu watu ndani ya chama chake kuhongwa pesa za Abdul hakuna mashiko sana.

Abdul kuhusika na hii process ya kumlipa Lissu ndio ni contradiction yenyewe. Wangetumia normal government channels sio mambo ya gizani sababu hiyo ilikuwa haki ya Lissu.

Wewe ukiwa unadai mafao yako serikalini hutayadai gizani kutumia mtu asiyekuwepo serikali mfano kutumia mtoto wa waziri husika.

Haijakaa sawa hii process ya Wenje na Abdul.
 
Waache kuisumbua serikali, kuita maandamano ya kudai katiba mpya, tume huru, kupiga kelele kuhusu kuuzwa bandari, kupigia kelele utekaji, mauaji.
CHADEMA wameacha kufanya hivyo??
 
Kila eneo unapoona limesimama Basi jua Kuna mtu aliesimama. Ukiiona chadema Basi jua Kuna mtu anaifanya kuwa chadema.
Ukiiona polisi Basi jua Kuna baadhi wasio wa kawaida wanaoifanya kuitwa polisi.

Lisu hajafikia hatua yakuifanya chadema kuwa Kama tunavyoiona. Ni mtu tu muhimu ndani ya chama.
 
CHADEMA wameacha kufanya hivyo??
Wamepunguza makali. Hawana moto kabla ya maridhiano, baada ya Mbowe kutoka jela na kukutana na Samia.

Wamekuwa watetezi wa Samia zaidi kuliko kudai haki kwa Watanzania. Walimpa tuzo kule Moshi, akatoa milioni 150 kwa kanisa kupitia Mbowe.
 
Yes Mbowe ukimchambua anaonekana ni MTU sahihi Ila wakati aliopo ndo sio sahihi.

Lissu anatembea na Wave (Wimbi) la watu wanaotaka kuona mabadiliko ya kweli na siasa za ushindani. Hivyo hawataki kumchambua na kuangalia weakness areas zake.

Hii ndo Kama ile 2015 - kuna watu wengi walipata ubunge na udiwani kupitia Wimbi la mabadiliko Ila katika uwezo walikuwa hawana uwezo wowote .

Means unaweza kuwa MTU sahihi Ila ukawa haupo katika wakati sahihi.

Mbowe inambidi aachie ngazi hii itamjengea Heshima sana. Asibishane na wakati
Wakati ni ukuta.

.........Ila FAM hawezi achia uenyekiti unampa madeal mengi sana.
 
Abdul yuko katika nafasi nzuri ya kukwamua mambo ya washikaji, marafiki na ndugu zake pamoja na watu wengine wachache wanaoweza kukatana kama ilivyotokea kwa Wenje ila hayuko katika nafasi nzuri ya kukwamua mambo ya kinchi.
Akiwemo Wenje?
 
Wamepunguza makali. Hawana moto kabla ya maridhiano, baada ya Mbowe kutoka jela na kukutana na Samia.

Wamekuwa watetezi wa Samia zaidi kuliko kudai haki kwa Watanzania. Walimpa tuzo kule Moshi, akatoa milioni 150 kwa kanisa kupitia Mbowe.
Ulienda kwenye maandamano waliyoitisha CHADEMA mwaka huu?
 
Nimesikiliza maelezo ya Ezekiel Wenje aliyetuhumiwa na Lissu kumpeleka Abdul kumuhonga pesa, ukiniuliza mimi naona maelezo ya Wenje yamenyooka sana kuliko tuhuma alizokuwa anarusha Lissu dhidi ya watu anaodai wamehongwa.

Swali ambalo limebaki sasa ni kwamba Lissu anafanya mambo haya kwa sababu au faida zipi ukizingatia inaleta mgawanyiko sana ndani ya chama chake!

Nilikuwa nasubiria kwa shauku kumsikia Mbowe atajibu vipi tuhuma za watu wake kuhongwa pesa za Abdul lakini maelezo ya Wenje yamenyooka sana, yanatosha na naona yana ukweli mkubwa kuliko tuhuma za Lissu.

I have the same opinion, baada ya kumsikiliza kwa makini Mr. Wenje, nimegeuza kabisa fikra zangu na kujua Tundu Lissu ni mtu muongo sanaaa na mropokaji sana, hana hekima wala busara, muongo kuliko shetani.

Mbowe bora aendelee kuwa Mwenyekiti wa Chadema..!! Sina shaka hata kidogo, Lissu sio kabisa.
 
Inawezekana kabisa ukizingatia pia kuna pesa ambayo Wenje alikuwa anategemewa atalipiwa kutokea malipo ambayo Lissu angelipwa na serikali, imetokea wamekaa na mtu wa karibu kabisa wa demigod wa nchi akaona ngoja ajaribu bahati yake labda wanaweza kumtendea Lissu haki yake na yeye akaambulia shillingi alizotumbukiza kuokoa uhai wa Lissu.
Pesa gani wenje alitegemea kulipwa kwenye stahili za lisu?
Naomba ufafanuzi
 
Inategemea na wepesi wa kichwa chako kilivyo, sioni ugumu wa haya unayouliza ukizingatia suala la Lissu limekuwa mjadala muda mrefu katika nchi, ni kitu rahisi tu kuanzisha small talk inayohusiana na nchi inavyokwenda na kisha kuchomekea hilo.
Naona umeamua kujizima data au kuwa tabula rasa
 
Back
Top Bottom