Maelfu wamchangia Mbowe katika kampeni ya #MwambaTuvushe ya kumrejesha madarakani CHADEMA

Tunamhitaji Mbowe kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote.Kama kweli wewe ni mwanachadema unatambua hilo.

Kwa hayo madhila yote uliyoandika hapo juu umeona Mbowe amenunuliwa na kusaliti wanamageuzi?Hilo tu linatosha kumuomba Mbowe aendelee si miaka mitano tu bali ikiwezekana hata 15 zaidi
 

Sina shaka na mchango wa Mbowe ndani ya cdm, ila ninasema kwa nafasi ya uwenyekiti imetosha. Hilo la kusema kuwa tunamuhitaji zaidi sasa hizo ni lugha za kila uchaguzi hivyo hamna lolote jipya la kwanini sasa zaidi ya mazoea. Kama ni cdm kukutana na wakati mgumu wala haliwezi kuisha kwa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti, bali wangalau sasa chama kipate sura mpya kwa ajili ya kurudisha hamasa mpya.

Haya yaoendelea hivi sasa hapa nchi ni yanaweza kuendelea kupambaniwa na cdm kama taasisi, na sio kwa uwepo Mbowe kama mwenyekiti. Magufuli hafanyi siasa hasa siasa za ushindani kwa kuwa haziwezi na hatakaa aziweze, sana sana atahakikisha cdm haifanyi siasa, na kwa asilimia kubwa hilo kafanikiwa kwa kutumia vyombo vya dola na taasisi nyingine za kimamlaka, na kwa bahati mbaya sana Mbowe kwenye hali hiyo ni kama kaishiwa mbinu. Hivyo hata kama Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti hakuna jipya zaidi ya haya yanayoendelea, na wakati Magufuli anatoka madarakani miaka 6 ijayo Mbowe atakuwa ni 65yrs. Wakati huo atakuwa anapambana zaidi na afya ya mwili wake kuliko kupambana kuinyanyua cdm. Hili ukubali ukatae lakini habari ndio hiyo.
 


Best tuwe wakweli..Mbowe akitoka wanaweza weka pandikizi lao!Mbowe tu amhitaji zaidi sema apunguze upole upole na hifu hofu!, natamani Mbowe angekuwa ana tabia na hulka za Heche!..hii mijitu ya kuhama hama unaikata kelbu kbs had azime😐!ukiona kunajitu limeanza jipendekeza ccm unalfumua makofi unalifukuza mapema!
 

Ni kweli, sasa kama cdm inaogopa mapandikizi toka ccm mbona walimpa Lowassa nafasi kubwa kabisa ya kugombea urais, na sasa karudi ccm? Au kuna pandikizi zaidi ya Lowassa? Tena huyo Lowassa alikuwa anakaa meza kuu na mikakati na siri zote za chama kazisikia na sasa yuko ccm? Hivi kweli cdm hakuna mtu yoyote mwenye uwezo wa kuwa mwenyekiti zaidi ya Mbowe? Mbona hata sasa Mbowe ni mwenyekiti na viongozi wanazidi kuhamia tu ccm? Kama ni kwenye chaguzi uhuni wa wazi unafanyika na hana lolote anafanya?

Unashauri Mbowe aache upole, inaonekana hujui kanuni ya you can not teach an old dog a new trick. Mbowe ana miaka 58 sasa, unatarajia ajifunze tabia mpya kwenye umri huo? Hapo alipo ni mzee sasa, na sehemu kubwa itakuwa ni kupigania afya yake zaidi kuliko kuleta jambo jipya ndani ya cdm. Tusiwe wepesi kuchotwa na propaganda ya kuwa eti bila Mbowe basi cdm itayumba, na kweli tukae tuamini hiyo propaganda bila kutoka nje ya box. Ni kweli Mbowe alikuwa mwenyekiti bora kabisa cdm, lakini wakati ukuta. Labda kama hicho cheo cha uenyekiti yuko nacho kwa matambiko hapo sawa, na kama ni hivyo basi hicho sio chama bali ni genge la wahuni lililoko kwenye siasa.
 
Bado nasisitiza hata akishinda kwa haki kama itakuwepo, miaka 15 inatosha sana kwa mtu kukaa madarakani
Hapa ni wewe ambaye utakuwa na tatizo.

Hiyo nadharia ya miaka 15, sijawahi kuisoma mahali popote. Hilo ni wazo lako tu.

Mbowe hajawahi kushika 'madaraka' ya kuendesha serikali yoyote.

Hao watakaomchagua, kama ni kwa utashi wao wenyewe, bila shaka watakuwa wanazo sababu zao mhimu za kufanya hivyo, na sio kwa 'dhana' tu ya kubuniwa na mtu mmoja. Kwa hiyo wakimchagua Mbowe, hata kama hukubaliani na tendo lao hilo, huna budi kuliheshimu.

Hao wanaochangishana, ni uamzi wao wenyewe kufanya hivyo; hawajalizimishwa. Sijasoma mahali popote Mbowe alipolalamikia kutokuwa na uwezo wa kulipa hele ya kuchukulia fomu. Sasa lawama juu ya hilo ni ya nini?
 


Ingewekwa namba hadharani kbs wenye mapenzi anachangia hata km mia!
 
Busara za Mbowe ndo kashika amani ya nchi japo ccm awaelewi akiingia mwingine atakubali kuonewa ndipo moto utakapolipuka kutuchoma wote
 
Busara za Mbowe ndo kashika amani ya nchi japo ccm awaelewi akiingia mwingine atakubali kuonewa ndipo moto utakapolipuka kutuchoma wote
Vibaraka wa Lumumba hawalijui hili
 
Ingewekwa namba hadharani kbs wenye mapenzi anachangia hata km mia!
Mpaka sasa mchango wa kumchukulia Fomu Mh. Freeman Mbowe umefikia shilingi Laki:800,000/= bado shilingi laki mbili Naomba Tuonyesha nguvu ya Umma, ndani ya Dakika 30 tupate laki 2 mwenye 250,500,1000,2000,5000,10000.
Tuma kwa namba 0715 444 064 jina ni Twaha mwaipaya. Twendeni kazi.

#MwambaTuvushe
 
Amina mtumishi wa Mungu
 
Mbowe Tano Tena
 
I like it tindo msema kweli...nakuunga mkono kwa hilo
 
Naunga mkono Mbowe kugombea tena kuongoza CHADEMA ili kuivusha kwenye awamu hii ya siasa za hovyo na za kishamba.Lakini siungi mkono huu upuuzi wenu wa kuhamasishana kumchulia fomu.Sina hakika kama Lowassa kawalisisha huu upuuzi.
 
Kwa hyo mbowe akifa na chama nacho kinakufa, kisa tu kutakuwa na mapandikizi?
 
Ila ukitaka kukutana na mashetani live ingia tu mtandaoni.
Yaani chadema washiriki kumpiga risasi Tundu halafu serikali hii,nasisitiza,"serikali hii" makini ishindwe kuwakamata?
Eneo lenyewe lilikuwa na CCTV camera,na walinzi wa serikali,halafu chadema ishiriki kulifanya na wabaki salama?
 

Kwa sababu umeaminishwa kwamba Serikali hii ndio wanao haribu nchi hii. Umeambiwa tetesi weka ukweli wewe basi ambao sio majungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…