Maendeleo ni nini? Ukweli kuhusu maendeleo ya vitu na maendeleo ya watu

Maendeleo ni nini? Ukweli kuhusu maendeleo ya vitu na maendeleo ya watu

Maendeleo ya vitu ni pale unapotumbua wafanyakazi kwa kuwaonea ili upate pesa ujenge reli

Maendeleo ya vitu ni pale Mishahara haiongezeki ili kupata pesa ya kununua madege

Maendeleo ya vitu ni pale wafanyabiashara wakubwa wanabambikiwa kesi zisizokuwa na dhamana ili badae wafilisiwe zikajengwe bara bara

Maendeleo ya vitu ni pale hajira mpya hazitolewi kwa Vijana ili kujenga barabara

Maendeleo ya vitu ni pale wananchi wwpobomolewa nyumba zao bila fidia ili kupanua bara bara, ni muhimu lakini taratibu zote zifatwe. Na mambo mengine mengi ongezea wewe.

Nimemuelewa sana huyu baba tundu lisu.
 
watu wakipata maendeleo wataleta vitu hata mandege kama fastjest walivyofanyaga.
vitu bila kuwawezesha watu ni kazi bure.
Kiuhalisia kuna gharama za matumizi ya kawaida na gharama za maendeleo. Katika familia, gharama za matumizi zinahusu chakula, mavazi, matibabu, usafiri nk. Gharama za maendeleo ni makazi, mashamba, elimu nk

Kwa nchi gharama za matumizi ni za kuendesha Serikali na maendeleo ni ujenzi wa vichocheo vya kukuza uchumi, kwa maana ya maendeleo ya vitu (njia za usafiri, viwanda, shule, hospitali, umeme, maji, nk), na kuboresha huduma za jamii, kwa maana ya maendeleo ya watu (afya, maji, elimu)
 
Hilo Sasa ni suala la kiuongozi. Kama wanapata kipato kizuri ilipaswa Sasa wawekeze kwenye huduma za kijamii

Huyo ndiye kiongozi tuliye naye anayetuambia kuna maendeleo kama Barabara na ununuzi wa ndege.
Ethiopia wana barabara nzuri kuliko za huko kwetu, pia wana ndege zaidi ya 50 wakati sisi tuna hizo pangaboi ambazo ziko yard tu.
Iki ni kielelezo kizuri kutuonesha kuwa tunahitaji maisha mazuri ya watu na siyo mendeleo ya vitu.
 
Kiuhalisia kuna gharama za matumizi ya kawaida na gharama za maendeleo. Katika familia, gharama za matumizi zinahusu chakula, mavazi, matibabu, usafiri nk. Gharama za maendeleo ni makazi, mashamba, elimu nk

Kwa nchi gharama za matumizi ni za kuendesha Serikali na maendeleo ni ujenzi wa vichocheo vya kukuza uchumi, kwa maana ya maendeleo ya vitu (njia za usafiri, viwanda, shule, hospitali, umeme, maji, nk), na kuboresha huduma za jamii, kwa maana ya maendeleo ya watu (afya, maji, elimu)
Umesema vizuri sana ndugu Mwengeso. Hilo ndilo linalofanywa na serikali ya Magufuli
 
Maendeleo ni ya watu kwanza,mahitaji ya watu ndio yatakayopelekea kua na maendeleo ya vitu.Huwezi kuanzisha vitu kama hakuna watu wakuvihitaji.Ata barabara zinajengwa kulingana na mahitaji ya watu,hospitali hivyo hivyo zinajengwa kulingana na mahitaji ya watu.Nahiyo nikwasekta zote.Kwahiyo Ni watu kwanza wapate uwezo ndipo mahitaji yatawalazimisha kupata hivyo vitu.
 
Huyo ndiye kiongozi tuliye naye anayetuambia kuna maendeleo kama Barabara na ununuzi wa ndege.
Ethiopia wana barabara nzuri kuliko za huko kwetu, pia wana ndege zaidi ya 50 wakati sisi tuna hizo pangaboi ambazo ziko yard tu.
Iki ni kielelezo kizuri kutuonesha kuwa tunahitaji maisha mazuri ya watu na siyo mendeleo ya vitu.
"Huko kwetu". Rudi nyumbani, kumekucha
 
Maendeleo ni ya watu kwanza,mahitaji ya watu ndio yatakayopelekea kua na maendeleo ya vitu.Huwezi kuanzisha vitu kama hakuna watu wakuvihitaji.Ata barabara zinajengwa kulingana na mahitaji ya watu,hospitali hivyo hivyo zinajengwa kulingana na mahitaji ya watu.Nahiyo nikwasekta zote.Kwahiyo Ni watu kwanza wapate uwezo ndipo mahitaji yatawalazimisha kupata hivyo vitu.
Umeeleza vizuri ila kuna sehemu nadhani haziko sawa.
Nakubaliana nawe kuwa maendeleo ni ya watu kwanza kwa kigezo cha uwepo (existence) ya watu hao. Watu wakishakuwepo, huhitaji wakuambie kuwa wanahitaji
Shule
Hospitali
Barabara
Maji
Nishati ya umeme
Mskazi n.k. Hili ni lazima utekeleze kww kujenga na kuweka mazingira wezeshi. Hili haliwezekani Kama una uchumi dhaifu. Unahitaji pesa. Pesa zinapatikana kwa
Kukusanya Kodi. Hii ni lazima watu wawe na vipato, kuwe na biashara na viwanda vya kutozwa Kodi
Unahitaji kutumia rasilimali zako kuwezesha hilo.
 
Hizo nchi unazozisemea zilianza kwanza kuboresha maisha na hali za watu wake kwakuweka mazingira sawia yakujipatia mahitaji yao yakijamii,kielimu,uchumi,afya na mengine,na hii nikwasababu watu hao hao kwanamna moja au nyingine ndio waliotumika kuleta hayo maendeleo ya vitu,kuanzia nguvu kazi zao hadi makusanyo ya kodi ambazo serikali ndio ilizitumia kufanya miundombinu mbali mbali kwa kadri mahitaji yalivyoruhusu.Hawakuanza kuweka miundombinu ya vitu visivyokua na mahitaji alafu wasubiri watu waje kuweza kuvitumia badae.
Nchi zote zinazoitwa zimeendelea, Zina maendeleo ya vitu yaliyoleta maendeleo ya watu.

Nchi zote hizo, Zina huduma za afya nzuei, huduma za elimu Bora, wanna miundombinu ya usafiri mizuri, wana ndege, treni, magari, viwanja vya ndege vingi n.k

SWALI

Unadhani wamewezaje kutoa huduma zote hizo Kama hawana uchumi mzuri

Uchumi mzuri unaletwa na nini?

Uwekezaji mzuri huleta uchumi mzuri. Tanzania inajitahidi Sana kuhakikisha huduma nzuri zinapatikana Hulu uwekezaji uliendelea
 
Hizo nchi unazozisemea zilianza kwanza kuboresha maisha na hali za watu wake kwakuweka mazingira sawia yakujipatia mahitaji yao yakijamii,kielimu,uchumi,afya na mengine,na hii nikwasababu watu hao hao kwanamna moja au nyingine ndio waliotumika kuleta hayo maendeleo ya vitu,kuanzia nguvu kazi zao hadi makusanyo ya kodi ambazo serikali ndio ilizitumia kufanya miundombinu mbali mbali kwa kadri mahitaji yalivyoruhusu.Hawakuanza kuweka miundombinu ya vitu visivyokua na mahitaji alafu wasubiri watu waje kuweza kuvitumia badae.
Mabadiliko ya kweli yana gharama kubwa, yanahitaji mtu jasiri na mzalendo kweli kweli
 
Waungwana,

Kwanza nikiri kuwa mimi sio mtaalamu wa uchumi Ila ninafahamu kuhusu maendeleo. Suala la maendeleo linatafsirika tofauti kutokana na mitazamo tofauti.

Hapa karibuni pamekuwa na kelele sana kuwa watanzania wanataka maendeleo yao (maendeleo ya watu) na siyo maendeleo.ya vitu.

Uzi huu uwe ni kujadili kati ya vitu hivyo viwili na mimi nitashiriki kama mchangiaji muongozaji.

Nini Kifanyike?

Amani Msumari
Tanga
Swali lako ni la kisomi kuhusu nadharia ya "maendeleo". Wakati huu wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, yeyote anayeaminisha wapiga kura kuwa kuna maendeleo ya watu anaota ndoto za mchana.

Yawezekana viongozi wa juu wa Upinzani wanajitahidi kutafuta jinsi ya kuiondoa CCM madarakani kwa kuwa Serikali yake ya 5 imefanya mambo makubwa ya kimaendeleo. Ili kufanikiwa ni kuhadaa wapiga kura kuwa hayo maendeleo ni ya vitu siyo ya watu.

Je, mgombea udiwani, kwenye Kata, ataweza kueleza wapiga kura hayo maendeleo ya watu ni yapi?

Ukweli utabaki kuwa wapiga kura wanataka viongozi watakaoweza kushughulikia/kumaliza kero zao za maendeleo ambazo ni ubovu wa barabara na madaraja, upungufu au umbali wa shule na zahanati, uhaba wa maji safi na salama, kukosekana kwa nishati ya kupikia na mwanga, nk.
 
Balambile bamutu ba kongo
 
Ndiyo, maendeleo ya vitu yanaweza kunufaisha ama kuchochea maendeleo ya watu, na vivyo hivyo maendeleo ya watu yanaweza kuchochea maendeleo ya vitu. Kinachohitajika ni kuweka mizania. Na mizania unaweza kuiweka kwa kuinyabua dhana ya 'maendeleo' na kuwa 'maendeleo endelevu'. Hitaji la msingi la 'Maendeleo endelevu' ni 'maendeleo shirikishi', yaani pale ambapo wananchi (ambao ni walipa kodi, wadau wa maendeleo) hushirikishwa katika maamuzi ya vipaumbele kupitia wawakilishi wao (ambapo kwa Tz ni kupitia Bunge la JMT au Baraza la SMZ). Serikali hupeleka hoja ya maendeleo bungeni, hoja hujadiliwa kwa kina (palipo na vichwa vingi hapaharibiki jambo) na hatimaye muafaka hufikiwa kuhusu kipi kipewe kipaumbele na kwa namna gani. Kufikia hatua hii, haya ni maamuzi ya wananchi, na kinachotokea wote hujivunia au hujihisi ni 'mali yao' (sense of ownership) na hivyo hutumia kila jitihada kuyalinda na kuyaendeleza kwa namna yo yote ile sio tu kwa ajili ya wakati uliopo, bali pia kwa vizazi vijavyo.

Sasa kwa bahati mbaya, utamaduni wa 'maendeleo' wa Tanzania ya Magufuli ni kwamba maamuzi ya vipaumbele na utekelezaji wake ni jukumu la Rais. Rais pekee. Rais ndiye alfa na omega, ndiye mwanzo na mwisho wa mustakabali wa jamii. ni mungu mdogo. Rais ndiye anajua waTz wanataka nini na sivinginevyo na anayepinga ni msaliti, ni kuadi wa mabeberu (ikipatikana fursa aondolewe uhai wake). Rais ndiye apewe open check na asiulizwe vipi (japokuwa historia ya utendaji wake akiwa waziri inaonesha ni hatari tupu mtu kama huyu kumpa open check). Bunge kazi yake ni kusifia na kucheza mdundiko - uwe utopolo au la maana. Historia ya binadamu inadhihirisha kuwa maamuzi ya kichwa kimoja hayajawahi kuwa na tija. Matokeo yake wananchi wakiwa wamenyong'onyea kwa unyonge (kama ambavyo amewabatiza - wanyonge) wanaangalia kila kitu ni cha Magufuli, ndege za Magufuli, barabara za Magufuli (of course, yeye hulka yake inamtuma afurahie hiyo hali) lakini kimsingi ni matumizi mabaya ya madaraka na wananchi hawataacha kulalamika na kupinga ama chini chini au kwa uwazi. Haishangazi anaanza kuwatishia tena bila soni walipaji kodi kuwa wasipochagua wagombea wa chama chake, basi watajuta (Chagua CCM au chagua majuto) - hatawaletea 'maendeleo'. Wadau wengi wameeleza humu humu, JF - ni hatari isokifani kuwa na Rais ambaye amekaa madarakani miaka mitano lakini hajui au anajifanya kutojua wajibu wa urais, na hata wajibu wa mbunge!!!! Na wananchi tunashangilia!!!
 
But kwnn yaliyofanywa yameshindwa boresha maisha ya watu.Watz wengi walishasahau Ni lini walikunywa chai ula maramoja kwa siku saa kumi Hadi kesho Tena.Kama umebahatika kula Milo 3 shukuru.
Watanzania gani hao wasiolima?
Asilimia kubwa ya watz ni wakulima na wanajilimia chakula chao, au ulitaka wapewe chakula bure?
 
watu wakipata maendeleo wataleta vitu hata mandege kama fastjest walivyofanyaga.
vitu bila kuwawezesha watu ni kazi bure.
Ni rahisi kuongea hivyo km umezaliwa 90s. Uhalisia ni vitu ndo vinawaletea watu maendeleo. Kipindi cha nyuma hakukuwa na miundombino hivyo usagirishaji wa watu na malighafi ulikuwa mgumu sana. Wengi walishindwa kufanya biashara nje ya MIKOA au Wilaya zao, kwa mf. Mazao ya mboga mboga huwezi safirisha kwa siku 2 yasiharibike.
Gharama za maisha nazo zilikuwa juu kwa sababu ya gharama za usagirishaji, mf. Vifaa vya ujenzi kutoka Kiwandani mpaka kwa mlaji bei inakuwa mara 3.
Hatukuwa na wataalam wa sayansi kwa sababu hakukuwa na miundo msingi ya maabara katika shule achilia mbali hao waalimu.
Kwa ufupi, ni kujitoa ufahamu tu kukataa uendelezaji wa vitu eti uwezeshe watu. Kwa mchango wako, hizo fast jet zingegua wapi km hamna viwanja?
 
SWALI FIKIRISHI 2

Upi ulikuwa mtazamo wa Mwl. Nyerere alipoongelea maendeleo ya watu?
Nyerere katika kitabu chake cha "Freedom and Development" alitafsiri maendelea kwa kupitia lensi ya watu kuwa tunataka maendeleo ya watu siyo maendeleo ya vitu. Lakini maana ya maendeleo ya watu alikuwa na maana ya kuwawezesha kujipatia kipato cha kutosha kuendesha maisha yao, kuwapa elimu, kuwapa huduma za afya na kufanya maisha yao yasigubikwe na rushwa au dhuluma ya aina yoyote. Lengo likiwa ni kupigana na maadui wanne wakuu: umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma. Kwa hiyo Nyerere alipokuwa anajenga barabara zile za kutoka Dar hadi Tunduma au kutoka Chalinze hadi Arusha, kununua ndege hadi anaondoka aliacha ndege 14, na kujenga viwanda, mashirika ya umma kama vile UDA, KAMATA, TRC, ATC alikuwa anajenga vitu lakini lengo likiwa ni kurahisisha uwezo wa watu kujipatia kipato cha kutosha kuendesha maisha yao. Alipoondoka elimu yote ya Tanzania ilikuwa ya bure, na hata huduma nyingi za afya zilikuwa bure. Ndiye aliyeanzisha kundi linaitwa anti-corruption squad kupigana na rushwa, ingawa kundi hilo halikufanikiwa sana.

Definition ya Nyerere kuhusu maendeleo ya watu ilikuwa hiyo; sijui kama nimejibu swali lako.
 
Back
Top Bottom