Ndiyo, maendeleo ya vitu yanaweza kunufaisha ama kuchochea maendeleo ya watu, na vivyo hivyo maendeleo ya watu yanaweza kuchochea maendeleo ya vitu. Kinachohitajika ni kuweka mizania. Na mizania unaweza kuiweka kwa kuinyabua dhana ya 'maendeleo' na kuwa 'maendeleo endelevu'. Hitaji la msingi la 'Maendeleo endelevu' ni 'maendeleo shirikishi', yaani pale ambapo wananchi (ambao ni walipa kodi, wadau wa maendeleo) hushirikishwa katika maamuzi ya vipaumbele kupitia wawakilishi wao (ambapo kwa Tz ni kupitia Bunge la JMT au Baraza la SMZ)....
Mwanzo umeeleza vizuri kuhusu ushirikishwaji wa wananchi wote kuamua vipaumbele vya maendeleo. Lakini kumhusisha Rais Magufuli yaliyotekelezwa katika kipindi cha utawala wake ni UMBUMBU wa kutokujua.
Rais Magufuli ametekeleza vipaumbele vilivyomo kwenye Ilani ya CCM, 2015-2020. Baadhi ya vipaumbele pia vilikuwemo kwenye Ilani ya Vyama vingine vya siasa. Labda kama umesahau nikukumbushe kuwa viongozi wa CHADEMA na ACT-Wazalendo wamekuwa wakidai kuwa Magufuli anatekeleza Ilani zao. Baada ya kufanikiwa kufanya vizuri wasivyotegemea wakabadili kauli na kudai ni maendeleo ya vitu.
Nadharia ya maendeleo ya watu (people-centred development) ina ubishani mwingi. Inachangamkiwa na nchi zinazoendelea. Na nchi ambazo zimeijaribu, kama Tanzania, hazikufanikiwa kujiondoa kwenye dimbwi la umaskini.
Nini maana ya maendeleo ya watu?
Wabobezi wa masuala ya Sayansi ya Kijamii wanaamini "Maendeleo ya watu" ni mbinu ya maendeleo ya kimataifa ambayo inalenga kuboresha kujitegemea kwa jamii, haki ya kijamii, na maamuzi shirikishi. Hii ina maana sehemu kubwa ya pato la Taifa litumike katika maeneo hayo.
Je, pato la Taifa linapatikanaje kwa nchi zinazondelea, ambazo uchumi wake ni tegemezi?
Tanzania ya Baba wa Taifa, ilijaribu kujenga uchumi wa kujitegemea (Azimio la Arusha) ambao haukiondoa nchi katika utegemezi kwa maana hata viwanda vilivyojengwa vilihitaji mitaji kutoka nje. Matokeo yake, jirani zetu km Kenya uchumi wake ulikuwa kwa kasi.
Serikali ya Mzee Mwinyi (Rukhsa) akavunja nadharia ya Ujamaa na Kujitegemea, kulikosababisha nchi kuwa tegemezi kiuchumi kwa 100%. Kukawa na maendeleo yasiyothibitiwa. Viongozi wa Mashirika ya Umma yaliyoanzishwa na Baba wa Taifa (kwa dhana ya Ujamaa na Kujitegemea) wakayafanya mali yao na kuyafilisi.
Serikali ya Mzee Mkapa (utawala bora) aliona hilo ombwe la utawala. Akauza mashirika ya umma yaliyokuwa yanafilisi hazina ya taifa na kuanzisha taasisi zenye kusimamia uchumi km TRA.
Serikali ya Kikwete, anisamehe tu, yeye hakuwa na nadharia yoyote ya kiuchumi, japo ni mchumi kitaaluma.
Kwenye Uchaguzi wa 2015, CCM iliona mapungufu yaliyokuwemo kwenye Tawala za awali ikaja na Ilani iliyobeba mazuri yote ya tawala zilizopita. Kwa mfano dhana ya ujamaa na kujitegemea ndiyo imeongoza katika kuimarishwa kwa njia kuu za uchumi (maendeleo ya vitu). Falsafa ya Mzee Rukhsa ndio inanotumiwa kuwapa nafasi wafanya biashara ndogo ndogo kutokubughuziwa kwa kupewa vitambulisho. Dhana ya utawala bora ya Mzee Mkapa inatumika kuimarisha taasisi zinazosimamia uchumi km TRA na makusanyo ya kodi kwa njia ya kidigitali.
CHADEMA ya Lissu inataka kuirudisha nchi kwenye uchumi wa Baba wa Taifa (maendeleo ya watu) bila mikakati yoyote inayoeleweka katika karne hii ya TEHAMA.