Maendeleo ya mtu yana uzuri asilimia 30 tu zinazobakia asilmia 70 ni uchafu mtupu ambao hubaki siri yake maisha

Maendeleo ya mtu yana uzuri asilimia 30 tu zinazobakia asilmia 70 ni uchafu mtupu ambao hubaki siri yake maisha

Siyo kwa ubaya lakini!

Naomba kuwatia moyo wenye uwezo mdogo kama mimi wa ugali na dagaa na tembele!

Ukweli ni kwamba sisi tuko bora kuliko hao wanaoonrkana wamefanikiwa!

Tunachofanya ni halali, tunachochuma ni jasho la haki tunagawana na familia maisha yanasonga!

Wanaoonekana wamefanikiwa sana wala siyo wa kuwaonea gere! Wengi wao ni wa kuwahurumia kwa upande mwingine!

Uhalali wa mali zao walizochuma kwa wema ni 30% tu...hizo zingine ni uchafu mtupu, ufisadi, umalaya, ukahaba, wizi, magendo hata ushirikina ni sehemu ya 70% ya mali zao!

1. Wapo wafanya biashara wakubwa wanaishi kwa nguvu za waganga tu, wanalala chini, hawavai chupi ..nguo moja au marufuku zingine!

2. Kuna wanasiasa tunawatamani Leo kisa wamelamba uteuzi, lakini yaliyowahi kuwakuta kabla ya kuteuliwa ukisimuliwa utabakia mdomo wazi! Uchawi, kuchapika na mengine mengi wamepitia wrngine walikwapuamo na magonjwa!

Kiufupi wengi waliofanikiwa sana tusichekelee juu juu kwa mali walizo nazo laiti kama tungejua chimbuko la mali zao tungewapiga marufuku hata kutoa sadaka misikitini na kanisani!

Machoni tunawaaeshimu sana sana! Lakini mafanikio yao yana ufusika kwa 70%

Sisi ni bora kuliko wao hata kama tumefulia lakini familillah siku zinasonga kwa aman ya 30%!

Tukiamua wote tuifanye ile asilimia 70% dunia itatikisika, amani itapotea, nch itatikisika!

Hivyo 30% ya aman ni bora kuliko 70% yao isiyojulikana!

Mungu anatupigania!
Yaani wewe haujuhi kwamba chakula unavyokula ndo vizuri. Utajiri wa kula chakula ambavyo si natural ni kutoka tu
 
Kwa amani 👍👍
Nyie lazima mtakuwa na roho ya kwanini sana...Mjifunze kufurahia mafanikio ya wenzenu, ndipo sa nanyi mtafanikiwa...Formular ya maisha ipo hivi, you cannot give what you do not have...Moyo wako ukijaa umasikini kama mnavyo onyesha wewe na mtoa mada lazima maisha yenu yajaee huzuni na umasikini.

Njoo kwetu kaskazini nikuonyeshe watu wenye mafanikio, elimu, pesa, watoto n.k lakini hawana mbambamba kabisa...
 
Back
Top Bottom