Maendeleo ya ujenzi wa stesheni za reli ya kisasa - SGR

Na hii ndo sababu alishindanwa na mota
 
Sitaki hata kidogo kukukatisha tamaa, kwa sababu natambua juhudi zenu hizi za miundombinu ya reli; lakini jibu lako hapo juu haliridhishi wala kutia moyo hata kidogo.

Na pia, huwa inaniwia vigumu sana kuitumia Kenya kama mfano kwa jambo lolote tunalotaka kulifanya sisi Tanzania, kwa sababu najua hakuna mifano mizuri ya kuiga huko, kasoro tu labda jitihada zao kubwa walizofanya kwenye elimu yao.
Baada ya kuandika haya, naomba nitumie mfano wa uendeshaji wa reli yao mpya.

Imewabidi waingie ubia na wachina kuiendesha reli hiyo kwa kujua kwamba wangeweka kichwa ngumu na kuiendesha wao miaka hii ya mwanzo, pato la reli hiyo na uchangiaji wake katika kulipa deni ungekuwa mgumu sana au kutokuwepo kabisa.

Sasa mimi sisemi kwamba nasi inatubidi tutafute wabia wa kutuendeshea reli hiyo itakapokuwa tayari. Lakini ninaposoma taarifa kama hii uliyoweka hapo juu, inanitia wasiwasi sana kama kweli tunajiandaa kufanikisha uendeshaji wa reli yetu hii mhimu!
Kama hadi sasa ndio mnajitayarisha kufikiria kuwaandaa watu wetu wawe na uwezo tosha wa kusimamia na kuendesha reli hii, hali hii haitii matumaini makubwa sana.

Naanza kujiuliza kama hii itakuwa na tofauti sana na hii ya mjerumani, kama mambo yenyewe ndio yalivyo hivi.

Pia niseme natambua wewe ni mwajiriwa hapo TRC, huenda upo kwenye kitengo cha habari.
Inawezekana hujafuatilia vizuri kunakohusika juu ya jambo hili.

Hebu jaribu tena kulifanyia kazi na utuletee mrejesho wake hapa, jinsi maandalizi yanavyofanywa kuiendesha hii reli kwa ufanisi mkubwa sisi wenyewe, bila ya kuwategemea wabia toka nje. Hili litakuwa jambo la kujivunia sana kama tunavyoendelea kujivunia juhudi zenu za kufufua reli ya mjerumani.

Bado wale wazee wa karakana, wapi (Morogoro?) waliokuwa wanafufua mabehewa na vichwa vya reli tunawatolea kofia kwa uzalendo wao huo.
Hebu hao wazee endeleeni kuwaenzi kwa juhudi kubwa walizolifanyia taifa hili.

Tunaitaka Tanzania ya namna hiyo kwenda mbele.
 
Si kweli. Mbona wanalipa vizuri Tu?

Hilo jina halipo sawa.
 
Ukiondoa hilo tatizo la kuchelewesha malipo, hapo ndipo utakapoona tofauti kubwa sana kati ya reli hii na ile ya wachina iliyojengwa Kenya na Ethiopia.

Uwepo wa wananchi wetu kufaidika na ujenzi wa reli hii.

Mimi ningeomba sana, TRC wawe makini zaidi katika kuhakikisha kwamba baada ya ujenzi huu, nasi tutakuwa tumepata uwezo wa kuwa na wataalam wetu, kwamba tukihitaji kujenga kipande kingine cha reli kama hiyo isitulazimu kwenda tena kuwatafuta hawa watu waje wajenge kipande hicho.

Ujenzi wa hizi barabara zetu na madaraja umekuwa mfano mbaya. Hatuwezi kuendelea hivi hivi miaka yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…