Kama hujui jambo, kaa kimya au uliza uelezwe..
JE, LISSU ALIINGIAJE CHADEMA?
Tundu Lissu alijiunga CHADEMA mwaka 2004.
Mwaka 2003, Lissu alikwenda Tarime kwenye masuala ya madini. Akakutana na Mh. Chacha Wangwe akiwa Diwani wa Tarime akiwa na kesi kumi za jinai. Mh. Wangwe akamwambia Lissu kuwa wanataka kumfunga. Lissu akamwambia aondoe hofu hawataweza.
Mh. Freeman Mbowe akampigia simu Mh. Lissu kumuomba amtetee Mh. Wangwe kwenye hizo kesi zilizokuwa zikifunguliwa kila uchao. Lissu akakubali na akafanya kazi yake kwa weledi wa hali ya juu. Mh. Lissu akasaidia pia kushinda kesi za wananchi wanyonge 366 katika kipindi cha miezi minne tu. Hawa ni wananchi waliokuwa wakiishi pembezoni mwa migodi kabla ya kuswekwa ndani kwa kosa la kuvamia migodi hiyo. Lissu aliwatetea BURE wananchi hawa mafukara na baada ya ushindi wa kesi hizo akatamka-"Uwekezaji umegeuka kuwa unyama Tanzania".
Lissu akaonekana ni mtu asiye na uzalendo na taifa lake kwa kuwasema vibaya wawekezaji ambao serikali ya ccm ilikuwa ikidai walikuwa wakiliingizia taifa mapato makubwa. Hata hivyo, kwa wananchi hao wanyonge, Lissu alionekana ni Mfalme.
Baadae Mh. Mbowe akampigia Lissu na kumuomba asaidie kutafuta wanasheria wengine waingie CHADEMA kama yeye. Lissu akamshangaza Mh. Mbowe kwani bila kupepesa macho, Lissu akasema yeye ni mwanachama wa NCCR MAGEUZI! Mh. Mbowe alistaajabu sana kwani aliamini Lissu ni mwanachama wa CHADEMA. Hivyo, Lissu akamwambia Mh. Mbowe "kama unataka nijiunge nanyi basi najiunga" ndivyo Lissu alivyojiunga CHADEMA.
Tundu Lissu aliendelea na jitihada zake kuwasaidia wananchi waliokuwa wakinyanyasika migodini huku akiacha wateja wenye fedha nyingi Dar Es Salaam.
Kwa Lissu, hakuna kitu kinamuuma moyoni mwake kama akiona mnyonge ana haki lakini anaonewa. Lissu kamwe hawezi kukaa kimya kuona hali hiyo ikiendelea.