Mafanikio ya mwanamuziki Burna Boy, nini tunajifunza?

Wanigeria wamepenya katika media na maeneo muhimu ya entertainment duniani. Sasa hivi wana elimu na ufahamu wa kutosha kujua nini wanatakiwa wafanye muziki na wasanii wao wapenye katika masoko duniani.

Kuna sehemu Marekani nimeshangaa niliposikia muziki wa Nigeria unapigwa na watu wanapagawa kabisa. Juzijuzi nimeona wana hadi TV series zao BET.

Mwisho wa siku ni elimu bora kwanza asikudanganye mtu.
 
Tunajifunza u freemason haulipi.
 

Jamaa wanajituma sana na pia Burna ana Management inayojielewa ,FAMCHEZO na Diddy?
 
Kiwango cha mafanikio kwa mtu hakipimwi kwa kumlinganisha na mwezie kinapimwa kwa malengo aliyojiwekea na utekelezaji wake.

Kwenye mziki mipango mikubwa inahitaji mtaji mkubwa, wasanii wetu wanamitaji????

Mtu pekee ambaye tunawezasema anamtaji (diamond) ndohuyo kaamua kuugawa mtaji wake kwenye biashara na Mziki. Kama angewekeza kwenye mziki pekeake pengine angekuwa mbali zaidi ( na labda hili sio Lengo lake kuwekeza kwenye mziki pekeake)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…