Mafanikio ya mwanamuziki Burna Boy, nini tunajifunza?

Wanaigeria wanajitambua na kupeana support.

Diamond na menejiment yake wanaangalia namna ya kubenifit kwa kiwakamua vilivyo upcomings kupigia mikataba ya kipuuzi.


Diamond akipata tetesi kuna msanii anarelease wimbo anahakikisha anatoa wimbo haraka kumfunika.

Soko lisilo na uwiano si soko bali anguko la anayelidhibiti

wasanii wapendane na kupeana sapoti
 


Inawezekana Diamond humfuatilii, Diamond alikaa miezi zaidi ya nane baada ya kutoa album yake ya FOA.Juzi ndio katoa nyimbo mpya na hata hiyo album alikaa karibia miezi sita ndio akatoa album.

Pili hivi unatizamaga nyimbo mpya zinazo achiwa na wasanii wa Nigeria MTV,mfano Burna ,Wizkid juzi wameachia nyimbo mpya na kuna lundo wasanii kibao wameachia nyimbo,bongo hapa kwanza wasanii hawatoi nyimbo kwa fujo.

Nitajie msanii mpya aliye achia nyimbo juzi na Diamond nae ndani ya wiki hiyo akaachia nyimbo.Mondi ktk miaka hii mitatu mfululizo naona hata mziki kidogo aliupa mgongo alikuwa anabuild media yake hata nyimbo alikuwa haachii kwa fujo.

Hivi ktk hii Industry ya Bongo fleva kuna msanii aliyebaniwa kama Diamond?Nitajie msanii ambaye alibaniwa na zaidi ya media tatu kubwa Tz ila still akasimama na yy na label yake nitajie MMOJA TU.Nitajie msanii mmoja aliye jitokeza akaongea na kusema hii sio sawa mmoja tena kwenye vyombo vya habari.
 
Bado nasisitiza nilichokisema.
Kama upo kwenye industry utakuwa na macho ya kuona rafu zake.

Tuendelee kula nyama, mtori upo chini
 
Hamna kitu kama hichi, kwenye gemu lolote hamna upendo ni chuki kwa kwenda mbele. Ngozi nyeusi uwa hawaombeani heri kwenye kutafuta pesa thubutuu. Wanigeria basi huwajui vizuri ukiona wasanii wao wanapatana sana basi ujue hao ni kabila moja labda yoruba, Igbo, Hausa, fulani n.k. Kwa ukabila Nigeria hata wakenya hawaoni ndani.
Ukiwaona wanapatana basi ujue ni kabila moja hao. Bado naendelea kusisitiza tatizo kubwa ni lugha, waanze kutumia na kiingereza sasa lazima watapata masoko zaidi. Hata movies tu, kwenye Netflix movie za Nigeria na Ghana zipo kibao shauri ya lugha, sasa hivi hata za Kenya zimeanza pia. Za bongo ilitoka moja hio ina subtittles lakini hata huyo mwandishi wa subtittle alikua anachapia pia. Lugha ni muhimu sana.
 
Hivi ulimsikia Shatta Wale wa Ghana alivyokuwa akiuzungumzia mziki wa Nigeria na huyu si msanii mdogo kishafanya Collabo mpaka na Beyonce, Siongei kujifurahisha.

Hakuishia hapo tu akapost clip ya Mr Flavor kwenye account yake ya twitter akiblame kwamba kuna baadhi ya wasanii wa nje wanafanya vizuri zaidi ya wanaija akatoa mfano wa Diamond, ila hawapewi airtime na vyombo vya Naija pamoja media kubwa za International.

Nakumbuka Vannesa Mdee alishawahi kuongea tukitaka mziki wetu utoboe zaidi vyombo vya kimataifa lazima tuwe na Decision Makers kwenye hizi media za kimataifa na ndicho kinacho tokea sasa,hivi brother unatizama MTV Africa, kaangalie playlist yao 70% ni mziki wa Nigeria,kafanye research yako hata ya siku tatu angalia playlist ya MTV Base.Wale jamaa wanajua kubebana na si wabinafsi na wasanii wao wanashirikiana mno.Lugha sio kila kitu SA na Kenya si wanazungumza Kingereza now wapo wapi.
 
Umejitahidi kuelezea lakini Kenya hawana wanamuziki wa kutoboa anga za kimataifa kwa kifupi muziki wao ni huko huko East Africa, Diamond baada ya kuimba na Davido angeendelea kuimba kilugha cha malkia angetoboa maana ilikua hata ukienda kumbi za muziki mamtoni unasikia nyimbo yao na ilikua inatajwa sana kua ni ya Diamond. South Africa walianza kuja maana hata majuzi vifo vya wanamuziki wao vimesikika kimataifa.
Turudi kwenye muziki wa bongo, hivi unajua akina Diamond/harmonize uwa wakija unyamwezini wanaoingia wengi ni east africans lakini wakija wanaija/ghana hadi wazungu wanafurika kwenye hizo kumbi...nambie sababu ni nini???LUGHA wanaousikia muziki na kuelewa maneno yanayoimbwa. Anyway, I agree to disagree ila mie ndio nilichoona hilo ni tatizo.
 

Nalijua ila Kingereza pekee hakitoshi kufika huko halafu sio lazima wote tufuka level za Burnaboy,hata tukifikia level za Fally Ipupa,Angelica Kidjo its OK.

Issues ni jinsi ya kupush kazi zetu nayo tatizo.Nigeria ukiachana hayo niliyo ya taja,wale jamaa walitumia sana hela ,Wizkid huyu Kafanya Collabo na Tyga imemtoka hela,kafanya na Cris brown imemtoka hela,badae akaja kufanya Collabo na Drake hii ndio ikaja kumtoa japo hizo collabo zote hakufanikiwa kufanya video,sababu dau alilowapa ni la audio tu. Njoo kwa Davido hela zimemtoka kwa Meek Mill,Fireboy kwa Ed hela imemtoka na nilisikia jamaa mwanzoni walikuwa wanahonga mpaka made kwa mujibu wa Davido now wapo pale.

So Kingereza pekee bado hakitoshi lazima ukubali kuwekeza kwenye mziki wako ni kitu ambacho kwa wasanii wetu hawana uthubutu,mwenye uthubutu huo ni Diamond,pili hili la decision makers kwa ajili ya kupush mziki wetu kwenye media za kimataifa hatuna,ndio maana nyimbo zetu hazi onekani sana MTV,BET nk

Ndio maana nikakwambia Kingereza pekee hakitoshi,mziki huu kama ukimsikiliza Shatta Wale level za kimataifa kuna fitina kubwa sana zifanyavyo na wanaija walio shikilia hizi media kubwa.
 
Haswaaaa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…