Mafanikio ya mwanamuziki Burna Boy, nini tunajifunza?

Wee ni team domokaya lazima umteteee, lol
 
Hasimamishi na huku huyo demu aliyetoa madai hayo(Stefflon Don) aliishi naye miaka zaid ya mitano,muda wote huo alikuwa anatumia vidole!?
Kwanza hajasema kwamba hasimamishi alisema ana oerformance mbovu kitandani
Kuishi na mtu kwa zaidi ya miaka 5 haimaanishi kwamba jamaa alikuwa vizuri kwenye eneo la unyumba.

Pengine kuna kitu cha ziada kilichomfanya huyo mwanamama aendelee kuwepo na jamaa, mbali kabisa na uwezo wa jamaa kuperform.

Hata hivyo, baada ya kauli ya huyo mwanamama, Burna alikiri hadharani kuwa ni kweli hana nguvu za kiume, akasema kwake yeye kuwa na pesa tu inatosha kuliko hizo nguvu za kiume.
 
Hivi mnaadithiana hii ishu huko vijiweni au tu wewe na wenzio humu mmeamua kuwalisha maneno tu Burna Boy na huyo mchumba!? Alichosema Stefflon Don ni hiko chini kwenye screenshot "poor performance" ambacho ni kinyume kabisa na maneno mnayomjaza kuwa alisema Burna Boy hana nguvu za kiume..Hivi ni vitu viwili tofaut tafadhali eleweni hilo
 
Kwa nini Burna Boy peke yake, vipi players wetu hawafikii levels walizofikia akina JJ Okocha, Nwanko Kanu.
Vipi hatuna movie stars kama Genevieve Nanji, Noah Ramsey.
Kwanini hatuna waandishi kama Chinua Achebe.
Vipi kuhusu kuwa na business personalities kama Dangote.
The list is endless, tusitafute namna ya kuwasakama music artists wetu wakati kila nyanja tuko nyuma hata elimu, uchumi, infrastructures na health care system.
Kama Mtanzania umefanya kitu gani kusogeza mafanikio ya nchi kisanaa, michezo, elimu, uchumi au afya mbele?
 

Kuna nyimbo zingine hazitumii kiingereza lakini zinafika mbali kwanini
 
Hakuna cha kiingereza wala nini... muziki ni lugha ya dunia. Hata uimbe kwa kichina kama muziki ni mzuri utapenya tu. Kina Brenda Fassie, Yvone Chakachaka na wakali wengine toka SA wanaimba kiingereza? Wakongo je? Yousso Ndour? Hawa vijana wetu uwezo wao mdogo. Huyu Diamond kinachombeba ni ujanja wake mwingi wa kucheza na mitandao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…