Naam, nimeona niliweke hili ili liwe kumbukumbu hapa JF kwa vizazi vijavyo. Kwa watu wenye uelewa wa Juu wa mambo ya kiuchumi,kisiasa na kijamii wanamuelewa Raisi Magufuli (PhD) kwa asilimia 100 hususani kwa hatua zote anazofanya, nitaeleza kwa kifupi tu na kwa kutumia lugha rahisi.

Kisiasa; watu wengi haswa wenye akili zinazoendeshwa na ukoloni mamboleo aidha kwa kufadhiliwa ama kwa ujinga wao wanadanganya watu kuwa mikutano ya kisiasa mfululizo,kila siku ndio demokrasia. Ninataka kuuliza swali kwa baadhi ya wenzetu walio huko kwa hawa wafadhili wa demokrasia hizi chafu, je leo huko Amerika Hillary Clintoni na Jeremy wa uingereza, Hollande wa Ufaransa wanafanya mikutano mfululizo barabarani? (public rally); sasa kwa akili za kitumwa' wajimga huku Afrika na Tanzania wamedanganya kuwa demokrasia ni kusimama kila siku majukwaani.

Kiuchumi, katika sera za kuelekeza wananchi tuwe na fikra za kujitegemea,kufanya kazi na kujiwekea akiba ya chakula na kampeni ya utekelezaji wa uchumi wa kati. Wanasiasa wajinga wenye akili za kitumwa eti wanabeza, wenyewe wanasema Raisi mzuri ni yule anayegawa chakula bure kwa kila mtu hata pale anapolalamika tu, yaani akivaa fulana imeandikwa ''njaa inauma'' apewe chakula eti kwa kizungu wenyewe wanasema Raisi ni 'Conforter in Chief'' eti kwa sababu wameongea kwa kizungu eti mantiki yake ni kubwa sana. Utaona jinsi ukoloni mambo leo unavyowageuza wanasiasa wakware wa kitanzania kugeuka kuwa watetezi wa mabeberu hata kwenye mambo ya msingi.

Kijamii, hapa ni pamoja na maadili, kumeibuka wanasiasa wenye mitazamo ya kitumwa hata kulalamika pale Raisi na mawaziri wanapopinga mambo ya kishoga na kisagaji. Kwa ujinga uliwatawala wamelalamika eti ''Raisi awe mwangalifu kwani tutanyimwa misaada'', kweli ?

Nimechanganua mambo machache ili kuwasaidia wachache ambao bado ulozi wa akili za kitumwa haujawaingia waache mara moja na hata wale waliorogwa basi waone aibu na kugeuka.
 
Ujenzi bomba la mafuta kutaleta ajira na kipato kwa nchi
 

mkuu maendeleo hayana chama hatukatai ila binafsi wewe ni mfuasi wa chama gani-tuanzie hapo
 
Chama cha Walimu Tanzania

kama upo chama cha walim tz naunga mkono hoja yako ilio na mshiko kwako na mkono mrefu ulio elekea kwenye maisha yako-na usithbutu kumkosoa alie kuajiri kama bosi wako -ila alie kupa ajira anaweza kukosoa utendaji wako na ni haki yake kukukosoa na kukuelekeza-
 
Mpaka sasa watumishi wa umma wanatembelea mshahara aliyouacha JK .. Nyongeza ni ile 9% ya paye kwa wale wa mishahara ya chini.. Ambayo haizidi hata sh. 5000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna cha mafanikio hapa ni umaskin kwa kwenda mbele,nchi inaendeshwa kama familia hiv,wafanyakaz wanalia ,wafanyabiashara wanalia,wanafunzi wanalia ,kila kona vilio tu hakuna jipya ,,halafu mkuu anajichanganya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…