fadhili mohamedi
Member
- Mar 26, 2018
- 10
- 2
Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.
Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.
Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.
Mpaka sasa kafanya haya;
Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------
Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;
Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba
Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.
Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.
Miradi Mikubwa ya Maji :
Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga
Vipi kuhusu shs. Tilion 1.5, huu ni wizi ulio vunja record ya zaidi ya millenium mbili.Ninamkubali sana huyu mh Rais ingawa hawezi kufanya kila kitu nilichokuwa natamani kwa mfano sipendi upendeleo awali tuliishi kwenye bwawa la upendeleo na kufanya watoto wa wenyewe kupata kila kitu hapa amepunguza zaidi ya asilimia 75,Kuiibia serikali kwa njia ya semina manunuzi hewa malipo hewa nk kwa sasa asilimia 90 wamedhibiti.Elimu walisoma watoto wao tu hapa mafanikio asilimia 95 tatizo limebakia kwenye elimu ya juu.
Pamoja mazuri mengi lkn mh.angejiweka mbali aache mamlaka zifanye kazi badala ya kuchukua majukumu kama yake binafsi akasimishe kwa mfano vyeti feki angeacha maamuzi yawe ya chombo kingine badala ya kujinadi kwamba yeye amewafukuza au anaposema serikali yangu nk.
Sasa anahaha anataka kufungia watsapp na google, je hii ni sehemu ya maendeleo?
Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.
Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.
Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.
Mpaka sasa kafanya haya;
Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------
Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;
Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba
Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.
Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.
Miradi Mikubwa ya Maji :
Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga
Cha muhimu katiba ifuatweDuuuu!kweli kila baya atatupiwa sijui mlitaka afanyeje ili akipata ushauri wenu aufanyie kazi maana uongozi ni lawama hata ungekuwa wewe kuna mambo ungelaumiwa tu siamini kama anafanya hivi kwa makusudi bali anakuwa na lengo zuri ambalo wasiompenda huvuruga kwa mfano uhasama na vyama vya siasa ulianza siku alipo apishwa walisusa na kutangaza vita aliwafuata bungeni waka msusa wakaanza kumuita majina ya kuudhi huku akipanga kwenda uelekeo fulani wanamvuta shati what do you expect.
Ili tutoke hapa tupate muafaka wa kitaifa mapambano siyo mazuri na serikali ipunguze maadui kwa kusimisha majukumu kwa taasisi maalumu zilizopo mfano vyeti feki siyo kazi ya rais,bandari nk.Maamuzi yawe ni ya taasisi siyo mtu mmoja.
Vyama vya upinzani vijitoe kwenye harakati maana hazina mwisho mfano tulipofanya harakati za uhuru tuliwatukana sana wakoloni lakini leo tunawapigia magoti.
Suala la CAG watu wengi hatuwezi kuelewa malumbao kikubwa wamjibu CAG mwenyewe yeye ndiye mwenye kutujulisha kama wapo sahihi kwa majibu yao au la.
Inasikitisha sana na kwa kweli kwa hali hii "YAJAYO HAYAFURAHISHI"Vipi kuhusu shs. Tilion 1.5, huu ni wizi ulio vunja record ya zaidi ya millenium mbili.
Unasema kakomesha upendeleo, vp kuhusu bomoa bomoa ya Dar iwe halali kwasababu hawakumpigia kura halafu mwanza walimpa kura nyingi wasiwabomolewe ?
je vp kuhusu wasifu wa paul makonda ninamaana vyeti vyake, je kwanini alitimua wengine na bashite kaachwa ? Tena namnukuu ' swala la vyeti kwa mtu anayechapa kazi halinihusu, wewe unafanya kazi nzuri, wewe chapa kazi' alisema raisi akimwambia makonda na uma wa watanzania.
Vp kuhusu trafiki light mahali ambako hakuna hata foreni za za magali labda za kuvusha punda na ng'ombe? Je chato ina hadhi gani au fursa gani za kibiashara au maendeleo hadi ikawa na airport kubwa kiasi hicho ?
Unazungumzia swala la elimu je tangu aingie madarakani ni mtoto yupi wa kiongozi ambaye yupo shule ya kata ?
Je unalifahamu swala la Jesca magufuli aliyepata dv 0 form 4 lakini akawa anasoma chuo kikuu cha uma tena kwa kodi za wananchi, na akipata mkopo wa 100% tena kwa course ambayo masomo yake alifeli, huku watoto wa maskini waliofaulu vizuri, wakilia kwa kukosa mkopo hata kuahirisha masomo yao ?
Je niambie serikali ilichukua hatua gani juu shambulio la Tundu lisu ? Wapo wapi waliomshambulia lisu ? Yupo wapi Ben saanane ? Yupo wapi yule azoli gwanda mwandishi habari wa kibiti?
Wanafunzi wanauwawa tena pasipo kosa mfano mwanafunzi wa chuo cha mwalim nyerere ? Nipe tamko la serikali juu ya hilo? Nipe tamko na hatua iliyochukuliwa juu ya kifo cha Aquilina ?
Vp juu ya wakosoaji wa sera au mwenendo wa nchi wanavyoanza kuhojiwa na uhamiaji ?
Vp kuhusu swala la democrasia na utoaji wa maoni, kwanini azuie mikutano ya hadhara ya kidemocrasia ? Vp kuhusu kuonyeshwa mubashara bunge ?
Niambie kosa halisi la manji ? Na kama alikuwa na hatia niambie kwanini yupo huru ?
Hebu niambie kitu gani mzungu akupe bure pasipo manufaa yake ?
Mzungu hawezi kukuachia bombadier bure pasipo sababu, hilo ni changa kwa watanzania.
Kwanini hataki kufanya ziara kwenye nchi zilizoendelea na kukomaa kidemokrasia akajifunze? Anatembelea rwanda atajifunza nini toka kwa kagame ?
Jiwe litampata mtu gizani ngoja mtoa mada na jeshi lake wajeMbona umeshindwa kuainisha matumizi ya zaidi ya Tshs. trilion 1.5 ( zaidi ya Tshs. bilion 1500). Tueleze zimetumikaje.
Milion 50 Tshs. Kwa kila kijiji zimefikia wapi ?
Huduma bora maslai zaidi. Motisha kwa wafanyakazi zipo wapi.
Vyeti feki na malipo yasiyostahili kufuatana na elimu mbona kaogopa kuwatumbua watu wake wa karibu ?
Maendeleo yanaletwa na watu, sio watu wanaletwa na maendeleo chato kuna vivutio gani mpaka kuwe na aiport kubwa, chato kuna population gani mpaka kuwe na trafick light,au hizo trafick light zitaongoza punda ?
Ukiniambia atakuletea kiongozi mzarendo kama msiba sawa utapata msiba.
Umeweka msumari wa moto kwenye kidondaRushwa bado, ila pamoja na hayo mazuri bado ameharibu kwenye demokrasia, bunge live, tunataka vyeti vya bashite na shutuma zake za ufisadi na uvamizi zifanyiwe kazi