Tatizo sio kufanya anayoyafanya, yaani ni kama serikali haijiamini na inakaririsha wananchi tuiamini yenyewe ndio imefanya makubwa zaidi
kwa maelezo yako, hakuna sababu ya JPM kuzunguka 2020 kuomba Kura kwa watu ambao tayari ameshawafahamisha kila siku aliyoyafanya.
 
ingekuwa ni mmoja wa waliolazwa nje kule morogoro road sijui kama ungeandika hivi
 
Cc tz hatuna akil ndio maana tuna aman,wajinga wana cfa ya kutojali ,babu yangu ni mzee lakn ni membe damu
 
Hahaahh kitu cha wali harage........ na chai ya bure huku ukisafisha macho kwa ujenzi wa barabara ya lami
 
Kasome Article 8 Of The Constitution Of Republic Of Tanzania
 
Ni Sawa Sawa Na Mchezo Wa Kung'ata Na Kupuliza, Ukipulizwa Unasahau Maumivu Uliyong'atwa
 
Miradi mingi kaikuta mbona, yy hausiki kabisa, mfano upanuzi wa uwanja wa ndege Dar, nimradi ulioanza mda na flyover Tazara

Labda kuuwa demokrasia na kuwapa hekaheka wapinzani wake hapo tutakubaliana
 
Sina shaka ya aina yoyote kuwa Rais Magufuli amejitokeza ni Rais mchapa kazi akisimamia kile anachoahidi na kuamini, na anahakikisha kinatekelezwa ipasavyo.
Kauli yake ya hivi karibuni katika ziara yake ya siku tisa mkoani Mbeya inahitimisha ukweli wa hoja yangu hiyo.

Kwenye mji mdogo wa Mbalizi, ambako alisimamishwa na wananchi na kuelezwa kuwa kero ya maji, kukatika umeme na migogoro ya ardhi ni miongoni mwa kero sugu, alisema, nanukuu:

Kwa miaka mingi tangu uhuru wananchi wamekuwa wakisikia maneno ya kisiasa na ahadi, sasa wamechoka.

Ili kusimamia kauli yake hiyo, Rais Magufuli alitoa amri kwa Waziri mhusika akisema, nanukuu:

Waziri (Prof. Mbalawa) ameahidi wiki tatu, lakini mimi ninamwongezea mwezi mmoja ili akamilishe mradi huu na muanze kupata huduma safi ya maji safi ya bomba.

Hakika wananchi tumechoka na maneno ya kisiasa majukwaani na ahadi hewa, tunahitaji viongozi watendaji, ambao watasimamia maneno na ahadi zao zinatekelezwa.

Dar es Salaam, kwa mfano kukatika kwa umeme au maji si jambo geni. Hali kadhalika barabara nyingi zinazokarabatiwa zimebaki na vifusi kwa muda mrefu wala viongozi wa Serikali za Mitaa na Mamlaka husika hawajali adha wanayopata wakazi. Kila mara ni ahadi tu.

Je, Rais Magufuli atembelee kila kona ya nchi na kutoa maagizo ndiyo kero za walipa kodi zisikilizwe na kutatuliwa.

Viongozi wahusika mjitathmini mkitambua kuwa CHEO NI DHAMANA.
 
Rais anapaswa kuweka misingi au mifumo na siyo kuongoza nchi kwa matamko ya barabarani. Akiondoka madarakani hakika hataacha kitu cha kudumu kwa anaongoza kwa matamko tu. Tunahitaji mifumo ambayo hata aje rais wa namna gani mifumo itamwongoza mfano ni mataifa yaliyoendelea kama USA. Trump hawezi kuiangusha Marekani na ukichaa wake kwani maamuzi ya msingi yanafanywa na wengi na yalishapitishwa na mifumo iliyopo.
 
Kwamba yeye hajui mifumo na mifumo haipo! Ukweli ni kwamba mifumo ipo, sheria zipo, nk.

Kwa mfano kuna viongozi wa Serikali za Kijiji, Serikali za Mitaa, Madiwani, Wabunge na hatimaye Mawaziri. Na kila kiongozi ana majukumu, madaraka na mamlaka yake.

Kilicho wazi ni viongozi "kula bata" na kulewa madaraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…