Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Pima maono yake na utendaji kazi wake utagundua Dr Magufuli ni zaidi ya chama cha siasa.

Hata ukiiangalia CCM kwa makini utagundua bila ya Dr Magufuli itayumba na kurudia enzi zake za mazoea.
Ukienda kwenye vyama vya upinzani utakuta vyote vinamkubali kasoro watu wachache sana lakini hata viongozi wao wakuu Mbowe, Mbatia. Zitto, Mrema, Prof Lipumba na Cheyo wote wanamkubali japo kwa namna tofauti.

October nitapanga foleni kumpigia kura Rais Magufuli na Diwani.....mbunge atanisamehe.

Maendeleo hayana vyama!
 
Vyama vya upinzani vinavyomkubali magu ni TLP,NCCR na CUF na wanamkubali kwasababu wapo Kwenye Payroll.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Watanzania tumshukuru Kikwete na Mkapa kwa kutuletea magufuli,hakika hata yule ambaye alikuwa kipofu ameona, Bubu kaongea na kiziwi kasikia-uongozi wa JPM umeleta funzo kubwa sana.hope next time watu wataelewa nini maana ya kiongozi na wataelewa maendeleo ni watu sio vitu.
 
Pima maono yake na utendaji kazi wake utagundua Dr Magufuli ni zaidi ya chama cha siasa.

Hata ukiiangalia CCM kwa makini utagundua bila ya Dr Magufuli itayumba na kurudia enzi zake za mazoea.
Ukienda kwenye vyama vya upinzani utakuta vyote vinamkubali kasoro watu wachache sana lakini hata viongozi wao wakuu Mbowe, Mbatia. Zitto, Mrema, Prof Lipumba na Cheyo wote wanamkubali japo kwa namna tofauti.

October nitapanga foleni kumpigia kura Rais Magufuli na Diwani.....mbunge atanisamehe.

Maendeleo hayana vyama!
" AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU " Nkulunzinza alipewa ukubwa kuliko huu unaotoa wewe , lakini nadhani umeuona utukufu wa Mungu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
October nitapanga foleni kumpigia kura Rais Magufuli na Diwani.....mbunge atanisamehe.
Mkuu usemayo ni kweli kabisa, ingawa hayo tunayo ita maono yake mengine ushauri na misimamo ya washauri wake ndani ya serikali na ndani ya chama chake (hapa kuna CCM wachache sana kundi lile la wanaojiona wa asili wakiwa wameunganisha mawazo na CCM mpya ya wageni).

  • Mwaka 2015 nilipiga kura kwa mtindo wako uliotaja na mwaka huu 2020 tukijaliwa nitafanya hivyo pia, Magufuli lazima nimpe tena kura yangu.
  • Sijawahi kuwakubali wagombea wengi wa udiwani na ubunge wa CCM au wa uraisi wa upinzani isipokuwa Dr. Slaa.
  • Mwaka 2010 niliwapa CHADEMA kura zote tatu, hivi unawezaje kumnyima kura Dr. Slaa au kura ya ubunge kwa Mnyika wa enzi zile siyo wa sasa?
  • Unawezaje kumyima kura ya ubunge Zitto Kabwe wa wakati ule?
 
Dikteta kachoka huyo atuachie Ikulu yetu Watanzania haraka sana. Kazi imemzidi kimo kabaki KUBWABWAJA upuuzi tu na kutumia madaraka yake vibaya kudhalilisha na kudhulumu Watanzania.
 
Yaani mimi na akili yangu timamu kabisa nikapange foleni ili kumpigia kura magufuli!! Kwa lipi alilonitendea mimi mtumishi wa umma tangu alipoingia madarakani!!

Mchagueni nyinyi walamba miguu yake.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Pima maono yake na utendaji kazi wake utagundua Dr Magufuli ni zaidi ya chama cha siasa.

Hata ukiiangalia CCM kwa makini utagundua bila ya Dr Magufuli itayumba na kurudia enzi zake za mazoea.
Ukienda kwenye vyama vya upinzani utakuta vyote vinamkubali kasoro watu wachache sana lakini hata viongozi wao wakuu Mbowe, Mbatia. Zitto, Mrema, Prof Lipumba na Cheyo wote wanamkubali japo kwa namna tofauti.

October nitapanga foleni kumpigia kura Rais Magufuli na Diwani.....mbunge atanisamehe.

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu wenzako wamemfananisha Magufuli na Yesu! Naona na wewe unaelekea huko huko!
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Ni bonge la coward tu! Najua atashinda/atashindishwa. But kura yangu hapati....nitawapa wanyonge kama sehemu ya pole kwao kwa kujaribu kushiriki.

Ni kama vile naangalia game ya ndondi. Bondia mmoja anapendelewa na refa na pamoja na gloves refa kamruhusu kutumia rungu na bondia mwingjne kafungwa kamba mkono yote lakini anajitahidi hivyo hivyo kukwepa ngumi na virungu na kujaribu kurusha ngumi.......nitamshabikia huyo pamoja na kuwa najua atapigwa na kuumizwa vibaya.

Ukweli tuuseme tu (Maendeleo hayana vyama!)
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Haya ni maneno kutoka kinywani mwake kwamba kazi ni NGUMU, ina MATESO MAKUBWA, HALALI. Kazi imemshinda it is TIME FOR HIM TO GO without further delays.

Pima maono yake na utendaji kazi wake utagundua Dr Magufuli ni zaidi ya chama cha siasa.

Hata ukiiangalia CCM kwa makini utagundua bila ya Dr Magufuli itayumba na kurudia enzi zake za mazoea.
Ukienda kwenye vyama vya upinzani utakuta vyote vinamkubali kasoro watu wachache sana lakini hata viongozi wao wakuu Mbowe, Mbatia. Zitto, Mrema, Prof Lipumba na Cheyo wote wanamkubali japo kwa namna tofauti.

October nitapanga foleni kumpigia kura Rais Magufuli na Diwani.....mbunge atanisamehe.

Maendeleo hayana vyama!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mkuu Yohana Mbatizaji, nje ya 'hidden identity of being key board worrior" wa timu Lumumba; sijui kwa nini napata hisia kuwa "true identity" yako kuwa, wewe ni Polepole na yule unaye mtambulisha kama Mzee Mgaya ni Abdullah Bulembo.
 
Rais Magufuli haitaji kampeni, Kazi zake tu ni kampeni, huyu Rais ni chaguo la Mungu kwa sababu!
1: ana hekima
2: amesaidia watu wa tabaka la chini ambao kimsingi ndo sauti ya Mungu.
3: nidhamu kazini imerejea saiv
4: mikopo kwa wanafunzi haichelewi tena inakuja kwa wakati
5: Hamna njaa kama kipindi cha nyuma
6: Rushwa imepungua kwa kiasi kikubwa
7: ufisadi umepungua..
8: kapunguza foleni dar es salaam.
9: Hamna wenye vyeti feki saiv tunaheshimiana kazini
10: ukifanya kosa Hamna cha kuhamishwa kama zamani ni kutenguliwa

Note: Mwaka 2015 nilikuwa upinzani maana niliona CCM sio chama tena! Lakini kwa Kazi za huyu Rais magufuli, sioni sababu ya kutomuunga Mkono!
Kuna miungu mingi sana sijui ni mungu yupi labda wa gamboshi.
 
  1. Ifuatayo ni tathmini yangu juu ya utawala wa rais Magufuri katika miaka yake mitano.Lengo ajue wapi amefaulu wapi bado ili arekebishe makosa kama atapata miaka mingine mitano.

    1.Pamoja na kujengwa miradi mikubwa Kama SGR, Stiegersgorge ,Ununuzi wa ndege .

    A. Hali ya Umaskini imeongezeka sana ndani ya miaka mitano.mzunguko wa pesa umepungua kutoka bilioni 220 mpaka bilioni nane .

    B .Wafanyabiashara wengi wakubwa wamehama nchi baadhi wamekwenda Zambia hivyo kuathiri mzunguko wa pesa na ajira .

    C. Biashara nyingi zimefungwa hii ni kutokana na makadilio makubwa ya kodi hivyo wafanyabiashara wakaamua kufunga biashara hivyo kuathiri mzunguko wa pesa na ajira .

    D . Ukosefu wa ajira ndani ya miaka mitano serikali imeshindwa kuajiri kama serikali iliyopita ilivyofanya ,serikali hii imeajiri kiujanjaujanja .

    E . Serikali imeshindwa kupandisha mishahara ndani ya miaka mitano ,hivyo kushindwa kuongeza mzunguko wa pesa .

    F . Mahusiano ya kimataifa , serikali hii imeshindwa kuimarisha mahusiano ya kimataifa Kama ilivyoyakuta chini ya JK na awamu zilizopita. Kumbuka balozi wa umoja wa Ulaya alitimuliwa hivyo , umoja wa Ulaya kusitisha misaada na kusema unaangalia upya mahusiano yake na Tanzania.Barua mbalimbali za masikitiko za ubalozi wa marekani ,Sweeden , Uholanzi kuhusu Ukiukaji haki za binadamu, demokrasia na utawala bora .Awamu hii imekuwa na matukio mengi sana ya ukiukaji wa haki za binadamu , watu kupotea , kufungwa , kuwekwa ndani bila mahakama kuthibitisha makosa ,kesi za ajabu za wakosoaji wa awamu ya tano zimejaa tele zisizokuwa na sababu .

    G. Ukiukaji mkubwa wa sheria na katiba awamu hii tumeona nchi inaendeshwa kwa amri za rais za papo kwa papo bila kujali sheria zinasemaje? Mifano mingi watumishi wateule wa rais kufukuzwa papo bila kujali sheria ,katiba na haki zao.

    H . Serikali kufanya Manunuzi na matumizi ya mabilioni ya pesa bila idhini ya bunge ,mfano mzuri ununuzi wa ndege.

    J . Serikali kulisimamia bunge badala ya bunge kuisimamia serikali rejea maagizo aliokuwa anapewa Ndugai na rais.

    K . Serikali kuingilia muhimili wa mahakama .

    L .Kuzolota huduma za afya ,mfano awamu hii kina mama wakijifungua mtoto wa kiume Tshs 50000/=.Mtoto wa kike 40000/=Tofauti na awamu iliyopita.

    M . Ukandamizaji mkubwa wa uhuru wa vyombo Vya habari.

    N . Ukandamizaji mkubwa wa demokrasia hasa uhuru wa vyama vya siasa , ambavyo havina madhara yoyote kwa serikali.

    O . Kuzolota kwa mifuko ya hifadhi ya jamii , hivyo Kupeleka wastaafu kulipwa kwa shida awamu nne , kidogo kidogkidogo.

    P . Serikali ya awamu ya tano kuendeshwa kwa propaganda zaidi kuliko uhalisia ikiwemo kuficha takwimu mbalimbali mpaka kutungwa sheria ya kuzuia watu kutoa takwimu .

    q .Ukuaji u humi ,Enzi za JK uchumi ulikuwa kwa 7% ,Sasa hivi tunaambuwa uchumi unakuwa kwa 7% ,Sasa alichofanya kwenye Ukuaji uchumi nini ? Ingawa WBna IMF wanasema 2020 /2021 makadirio ya Ukuaji uchumi ni 2% kabla ya Corona.Wakuu itaendelea . Stay tuned . Unakaibishwa kuongeza , kuchangia ,maoni , ushauri.
 
Duh! wewe jamaa uwe unaweka na paragraph kwenye andiko lako.

Anyway, huyo jamaa angeruhusu uwanja sawa wa kufanya siasa, angeshangazwa sana na matokeo ya kwenye uchaguzi muu wa mwaka huu 2020.Ukweli Watanzania hawahitaji ndege na madaraja tu! Wanahitaji pia 'mkate'

Na mkate huo huo ndiyo ulio wapindua watawala wa Ufaransa mwaka 1789 na pia Urusi mwaka 1917. Watanzania wanataka maisha bora na siyo bora maisha kisa eti unanunua ndege.
 
  1. Ifuatayo ni tathmini yangu juu ya utawala wa rais Magufuri katika miaka yake mitano.Lengo ajue wapi amefaulu wapi bado ili arekebishe makosa kama atapata miaka mingine mitano. 1.Pamoja na kujengwa miradi mikubwa Kama SGR, Stiegersgorge ,Ununuzi wa ndege .A. Hali ya Umaskini imeongezeka sana ndani ya miaka mitano.mzunguko wa pesa umepungua kutoka bilioni 220 mpaka bilioni nane .B .Wafanyabiashara wengi wakubwa wamehama nchi baadhi wamekwenda Zambia hivyo kuathiri mzunguko wa pesa na ajira . C. Biashara nyingi zimefungwa hii ni kutokana na makadilio makubwa ya kodi hivyo wafanyabiashara wakaamua kufunga biashara hivyo kuathiri mzunguko wa pesa na ajira .D . Ukosefu wa ajira ndani ya miaka mitano serikali imeshindwa kuajiri kama serikali iliyopita ilivyofanya ,serikali hii imeajiri kiujanjaujanja . E . Serikali imeshindwa kupandisha mishahara ndani ya miaka mitano ,hivyo kushindwa kuongeza mzunguko wa pesa . F . Mahusiano ya kimataifa , serikali hii imeshindwa kuimarisha mahusiano ya kimataifa Kama ilivyoyakuta chini ya JK na awamu zilizopita. Kumbuka balozi wa umoja wa Ulaya alitimuliwa hivyo , umoja wa Ulaya kusitisha misaada na kusema unaangalia upya mahusiano yake na Tanzania.Barua mbalimbali za masikitiko za ubalozi wa marekani ,Sweeden , Uholanzi kuhusu Ukiukaji haki za binadamu, demokrasia na utawala bora .Awamu hii imekuwa na matukio mengi sana ya ukiukaji wa haki za binadamu , watu kupotea , kufungwa , kuwekwa ndani bila mahakama kuthibitisha makosa ,kesi za ajabu za wakosoaji wa awamu ya tano zimejaa tele zisizokuwa na sababu .G. Ukiukaji mkubwa wa sheria na katiba awamu hii tumeona nchi inaendeshwa kwa amri za rais za papo kwa papo bila kujali sheria zinasemaje? Mifano mingi watumishi wateule wa rais kufukuzwa papo bila kujali sheria ,katiba na haki zao. H . Serikali kufanya Manunuzi na matumizi ya mabilioni ya pesa bila idhini ya bunge ,mfano mzuri ununuzi wa ndege. J . Serikali kulisimamia bunge badala ya bunge kuisimamia serikali rejea maagizo aliokuwa anapewa Ndugai na rais. K . Serikali kuingilia muhimili wa mahakama . L .Kuzolota huduma za afya ,mfano awamu hii kina mama wakijifungua mtoto wa kiume Tshs 50000/=.Mtoto wa kike 40000/=Tofauti na awamu iliyopita. M . Ukandamizaji mkubwa wa uhuru wa vyombo Vya habari. N . Ukandamizaji mkubwa wa demokrasia hasa uhuru wa vyama vya siasa , ambavyo havina madhara yoyote kwa serikali. O . Kuzolota kwa mifuko ya hifadhi ya jamii , hivyo Kupeleka wastaafu kulipwa kwa shida awamu nne , kidogo kidogkidogo. P . Serikali ya awamu ya tano kuendeshwa kwa propaganda zaidi kuliko uhalisia ikiwemo kuficha takwimu mbalimbali mpaka kutungwa sheria ya kuzuia watu kutoa takwimu . P .Ukuaji u humi ,Enzi za JK uchumi ulikuwa kwa 7% ,Sasa hivi tunaambuwa uchumi unakuwa kwa 7% ,Sasa alichofanya kwenye Ukuaji uchumi nini ? Ingawa WBna IMF wanasema 2020 /2021 makadirio ya Ukuaji uchumi ni 2% kabla ya Corona.Wakuu itaendelea . Stay tuned . Unakaibishwa kuongeza , kuchangia ,maoni , ushauri.
Baada ya kuandika uwe unamtumia yule kaka yako aliyehitimu form mwaka jana anapitia na kufanya marekebisho ndiyo unatuma huku JF
 
Back
Top Bottom