Amani ya Bwana iwe nanyi wadau,
Ni dhahiri shahiri kuwa kwa yanayotokea leo Tanzania sio tu yanawashangaza watanzania bali yanaishangaza dunia kwa ujumla, na haya yote yanatokana na Huyu mtu ambaye dunia nzima inapata habari zake saivi kuanzia kutoka kwenye twitter, facebook, magazeti hadi vyombo vya habari mbalimbali duniani. Huyu si mwingine ni John Pombe Magufuli kwa watu wengine wanamuita buldoza ila mie napenda kumuita mtumishi wa Mungu.
Kusema kweli huyu mtu amemuonyesha raisi wa marekani ambaye wakati alipotembelea nchi ghana miaka michache iliyopita alisema wakati anahutubia bunge la ghana kuwa Africa need strong institutions and not strong leaders. Kama kumprove mtu wrong basi Magufuli kusema kweli kamprove Barack Obama wrong kwa sababu nitakazozieleza hapa chini.
1. Magufuli amemuonyesha Obama kuwa ndani ya Tanzania ambayo ni sehemu ya Africa kulikuwa na strong institutions ambazo zimewezeshwa vizuri kiutendaji na hata kivifaa ila havikuwa efficient tu kwa sababu hakuwepo strong leader, sasa strong leader amepatikana efficiency yake imeanza kuonekana
2. Magufuli kwa kipindi kifupi sana amemuonyesha Obama kuwa waafrika ni jamii ya kipekee sana ambao ili waende ni lazima aliye juu awe mtu wa namna fulani hasa kiutendaji na kiuadilifu ambapo yeye ndo anadetermine kama nchi iende mbele au vipi.
Hizi hapo juu ni sehemu tu ya mifano ambayo magufuli amemuonyesha Obama kuwa Africa inaitaji strong leaders na sio strong institutions na nauhakika sio tu Magufuli aliyemuonyesha Obama. Najua kwenye list hii wapo pia Paol Kagame ambaye jinsi nchi inavoenda chini wa uongozi wake inaonesha kuwa Obama azlikuwa wrong kuhusu Africa, sio tu hapo hata Marehemu Meres Zenawi kwa alichofanya Ethiopia pia ni ujumbe kwa Obama.
Napenda kumaliza kwa kusema Africa ni Africa na pia ulaya ni ulaya na Marekani ni Marekani pia. Na kwa Africa tumeshajionea kuwa ili bara hili lisonge viongozi jamii ya Patrice Lumumba, Sankara, Meres Zenawi, Muhamad Ghadafi, Paol Kagame na huyu wetu John Pombe Magufuli ni muhimu kwa mustakabali wa bara letu.