okonkwo jr
JF-Expert Member
- Jun 14, 2015
- 2,419
- 1,738
Mheshimiwa rais mtukufu kwa niaba walimu na mimi nikiwa miongoni mwao,napenda kukukumbusha kuwa walimu hawahitaji mishahara mikubwa kama ambavyo wamekuwa wakidai,kwani kwa sasa ukiangalia walimu ni wengi sana unakuta shule moja inawalimu 60 huku baadhi ya walimu wakifundisha mkondo mmoja walimu wawili ,kukuthibitishia hili, ni shule ninayofundisha mimi tuko walimu 20,wanafunzi 60 kwa shule nzima,na kuna baadhi ya walimu wanafundisha darasa moja walimu wawili,kwa mtazamo wangu na nafsi yangu naona kama mshahara ninao pewa ni wabure,kwani kwa siku ninakipindi kimoja cha dakika 40,hivyo napendekeza kama ulikuwa na lengo la kutuongezea mshahara walimu naomba usitishe mara moja,pesa hiyo inunue dawa,pia isaidie masikini na yatima.