Kuanguka kwa CCM na kuvurunda kwa serikali ya awamu ya nne sio sula la bahati mbaya bali ni mpango uliosukwa ukasukika hasaaa chini ya magwiji wa siasa za kiswahili na wabobevu wa kitaaluma wakiongozwa na Mzee wa hekima za nera Mzee Mtei, Mzee Bob Makank na kijana machachari wa enzi hizo Freeman Aikael Mbowe,
Hakukuwa na njia ya mkato bali kukaa chini na kuchora ramani ndefu ya kuangusha utawala huu wa ccm wenye kila aina ya maovu dunia, na wenye maajabu yote duniania, hilo lilikuwa kama fumbo la imani vile na sasa ni udhihirisho.
Kwa wale walioanza kufuatilia siasa za kiswahili siku za jana itakuwa vikumu kwao kuelewa na kuamini hili nilisemalo, lakini waelewe kuwa Jakaya Mrisho Kikwete ambae leo hii ni rais wa Tanzania ni mwanachama wa Chadema anayetambuliwa kwa kadi yake HALALI aliyokabidhiwa 25/6/2005 na Mzee Mzee Mtei katika ardhi ya Bagamoyo chini ya ushuhuda wa Mbowe, Mzee Makani na wadau wengine kadhaa mhimu.
Hilo lilitokea baada ya kuwa na mvutano mkali ndani ya ccm wakati Kikwete akiamini kuwa sasa ni "zamu" yake kuteuliwa kugombea urais wa Tanzania, makundi makubwa yaliyokuwa yakiongozwa na yeye Kikwete yalimtisha kiasa cha kufikia hatua ya kujiandaa kukikimbia chama hicho, ambapo hatua hiyo iliwafanya wazee wahekima kubuni mbinu ya kuiua ccm kwakupandikiza jasusi mhimu ndani ya ccm,
Walimfuata kwanza Bagamoyo, wakamshawishi aje Chadema agombee urais na kwakuwa alikuwa na majority angeshinda, akakubali na kukabidhiwa kadi rasmi ya uanachama, ikawa sasa anasubiri tu jina lake likatwe ili ajiunge na jeshi hilo la ukombozi, Lakini nyuma ya pazia wazee hawa walikuwa tayari wamemuingiza kwenye rada za kumtumia kuivuruga ccm na kuiangusha kabisa bila yeye kujua.
Mungu sio Yericko wala Jakaya, jamaa akapenya uteuzi pale Chamwino Dodoma, ambapo mgombea wa Mkapa bwana Abdala Kigoda alifia mfukoni mwa Mr Cleaner, hili ulikuwa ushindi wa Wazee wa Chadema kwani mpango wao ulikuwa umetimia, walitambua kuwa hana uwezo wa kuiongoza ccm bali ndie mtu pekee wakuiangusha.
Baada ya hapo kilichotokea na kinachoendelea kutokea nyinyi mnakiona na mnakijua,
Kama hamkioni na kukijua subirini 25/10/2015.
Asante wazee wa Chadema, asante Jakaya mwanachama HAI wa Chadema uliyetimiza mission uliyotumwa bila kujijua.
Kwaheri ccm, Kwaheri udharimu!