Barani Africa, Nigeria imeiambukiza nchi ya Tanzania ugonjwa usiotibika kirahisi. Maigizo. The carrier of this disease was the late Kanumba the great in the movie called Dar to Lagos. Mambo ya "this food is too much pilipili". Since then raia wa Tanzania wamekuwa wapenzi wa kutizama maigizo kwenye luninga kama ilivyo kwa Wanigeria.Na Kanumba alijizolea umaarufu mkubwa ajabu. Mazishi yake yalivunja record ya msiba wa Baba wa Taifa. Rest in peace the legend.
Kanumba aliacha pengo kubwa katika tasinia ya Bongo Movies.Kulikuwa na ombwe katika maigizo. Tasinia hii ilianza kupoteza mashabiki kila uchao kwa sababu ya kukosekana kwa wahusika mathubuti wenye kuigiza visa vya kusisimua.
Lakini tangu ujio wa filamu ya Hapa Kazi tu, ombwe hili linaekea kuzibwa barabara.Mhusika mkuu ana kaliba ya Kanumba; anajua kubuni na kuigiza visa vinavyosisimua ajabu. Kwa vile huu ugonjwa kutoka Nigeria umewaathili Watanzania, na sasa wanapenda maigizo ya kwenye TV, awamu hii inaanza kupendwa sana. Sasa hivi kila siku watu hawabanduki kwenye TV zao, wanataka kushuhudia vitimbi na makeke ya 'Kanumba' wao.Na filamu ndiyo kwanza imeanza. Ni filamu ya kusisimua ajabu. Na inaelekea mapema kuvunja record ya mauzo iliyokuwa inashikiliwa na ile filamu maarufu ya "Kasi Mpya Nguvu Mpya" Tayali mamulaka ya Bongo Movies imethibitisha kwamba filamu hii ya Hapa Kazi tu imekamata soko vilivyo. Hakuna movie nyingine inakohoa ndani ya Bongo.
Movie hii itafika kwenye climax pale balaza la mawaziri litakapoteuliwa. Tunaambiwa kwamba wahusika sasa hivi wanajifua vilivyo ili kuendana na kasi ya mhusika mkuu. Hili ni booonge la movie. Muda huu macho na masikio ya hadhira yako wazi muda wote. Sio filamu ya kukosa hii. Kila mtazamaji anaisubiri kwa hamu episode hii. Lakini mimi ninachokisubiri kwa hamu ni the END ya hii movie. Please guys stay tuned more drama is coming. Order more nuts, more popcorn please.