Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Hakika tuliochaguliwa ni wengi bali wateule ni wachache.Natazama namna Magufuli anavyolijenga upya taifa letu sina shaka huyu ni mteule wa Mungu.Basi na tuzidi kumuombea ili wale waovu wa harakati hizi za maendeleo Mungu akazibatilishe nia zao!

Huyo ni chaguo la shetani mana hata nayeye hujiita mungu.
 
Mkuu wanaoponda ni mission town na club yao ndio hiyo imetaifishwa usicheze na Hapa Kazi tu!
Kweli kbsa. Umenena vyema mwana Lumumba
-waliondolewa fao la kujitoa ni mission town
-Walionyimwa mikopo na mission town
-Waliosimamishiwa ajira nao ni mission town
-wanaolalamika dawa hazipo hospitali nao ni mission town

KUMBE MISSION TOWN WAPO WENGI HIVYO. Hongera sana kwa kulitambua hilo
 
Baada ya hotuba yako ya jana, wazee wameiona miaka ile ya Nyerere, wanafanya tathmini na kuona utawala wako umerudisha heshima. Wanajiuliza vile viwanja vya mpira kila mtaa viko wapi? Michezo mashuleni ipo wapi? Wanafunzi watafanyaje vizuri bila michezo ya kuchangamsha miili yao?

Name naunga hoja za wazee hao mkono. MCHAKAMCHAKA mashuleni urudishwe kama sisi tulivyokimbia tulifundishwa ukakamavu. Hawa kinda waliozaliwa kuanzia enzi za Mkapa na Jakaya, ovyo sana ndo hao wanaotukana tu kwenye mitandao na kulia lia tu hawataki kujishughulisha.

Magufuli kaza buti, bado usiwasikilize wavivu na mafisadi.
 
Mm ni mwananchi wa kawaida ila nachukia kuona kila anayelalamika kwa matatizo yake anaitwa fisadi na mvivu.

Kama wewe umefanikiwa kupata kazi kwenye mazingira ya kifisadi na saiz upo salama, ni jambo la kushukuru na sio kubeza wenzako ambao kweli wanalia kwa shida zao

Hao wazee wanaomsifia rais ni masikini na hawana wivu wa maendeleo. Wivu wao ni wakike wa kidhani matajiri ndio waliowapa umasikini
 
zamani hakukuwa na walalamishi kama wewe! Kwani lazima utegemee kuajiriwa tu? Watanzania wangapi wameajiriwa? Utazeeka kwa kulalamika maana hata ukiajiriwa bado utalalamika tu!
 
Wafuatao ni kama hawapo kwenye viunga vya siasa za Tanzania:-

1. Said Kubenea

2. John Mnyika

3. Tundu Lissu

4. Ester Bulaya

5. Halima Mdee

6. John Mrema

7. Edward Lowasa

8. Fredrick Sumaye

9. David Kafulila

10. Silinde

11. James Mbatia (Mama Tanzania)

12. Mchungaji Msigwa

13. Sugu

14. Professor J

15. Joshua Nasari

16. Salum Mwalimu

17. Wilfred Lwakatale

18. Lawrence Masha

19. Kingunge Ngombare Mwilu

20. KUB- Freeman Alkael Mbowe

**************************

Na wengineo wengi ambao wewe utawaongeza hapa.

Mbona wapo kimya sana hawa watu?Zile amsha amsha za kipindi kile vepe? Au wamesafiri nje ya nchi kikazi?

Au vya kusema havipo?Maana naona Mh Rais anatekeleza na yale waliyokuwa wanayapigia kelele kila kukicha.
 
Nilimsikiliza kwa makini sana Mhe Rais Magufuli alipokuwa akiongea na wahariri na waandishi wa habari kwa kujibu maswali yao. Nimemuelewa kabisa anatamani sana hii nchi iwe ya namna ya tofauti sana na hapa ilipo.

Anatamani Maliasili za nchi hii zilete maisha mema kwa watanzania wote na katika hali ya usawa kabisa. Kila mtanzania aweze kwenda shule, atibiwe na kupata huduma zote za msingi za kijamii katika hali isiyo na manyanyaso.

Ana malengo mengi mazuri sana hapendi wizi, rushwa, uvivu, Uonevu na uongo. Mhe pia anaona ndoto zake hizo hawezi kufika kwa nguvu yake peke yake bila ya kusaidiwa na wananchi wa nchi hii kwa kila mmoja katika nafasi yake aidha ni kiongozi wa Chama cha siasa, kiongozi wa serikali, mkulima, mfanyabiashara au yeyote yule ndio maana amekuwa na pia alisisitiza juzi akiongea na waandishi kuwa tumsaidie ili atimize ahadi zake alizoahidi watanzania.

Tumuunge Rais Magufuli ili anyoshe Taifa letu na tule matunda ya nchi yetu kama Taifa kwa ujumla badala ya kuliwa tu na wachache wajanja.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu wabariki watanzania.
 
habari zenu wanajamvi, nimekua nikisoma thread nyingi humu jamii forum watu wengi wamekua walalamikaji bila kuwa na mantiki ya ulalamikaji wao.

watu wengi walilalamikia sana utawala uliopita na kuongea maneno mengi ya kashfa kwa utawala uliopita sasa mambo yamerekebishwa na mabadikiko tunayaona.

nimekua nikijiuliza sana hivi wanaolalamika na kutengeneza thread nyingi humu jf hawaoni zuri hata moja linalofanyika?

ila nimegundua walalamikaji wengi ndo waliokua wapigadili wakubwa na wengi wao mirija imefungwa au wameondolewa kazini wamekuja jf huku wakijifanya chui waliojivika ngozi ya kondoo.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom