Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mimi kama Mtanzania mzalendo na mwenye kuipenda nchi yangu Tanzania
Nasema kama taifa tuna kila sababu ya kumshukuru sana Mungu, kwa kutupatia mh Rais Dr John Joseph Pombe Magufuli
Nayasema haya kwa sababu, moja ya changamoto kubwa barani Afrika, ni kukosa viongozi wenye dhamira ya dhati katika kuongoza mataifa na watu wao

Sisi Tanzania leo tuna la kujivunia sana tena sana na kutembea kifua mbele, kwa kumpata Rais wa aina hii

Ndani ya muda mfupi katika uongozi wake, ni ukweli usiopingika kuwa anaonyesha kabisa kuwa ana dhamira safi juu ya nchi yake

Mifano ipo mingi sana nisingependa kuiorodhesha humu ndani, ila kwa mtanzania yeyote mwenye akili timamu hawezi kupingana na hili

Japokuwa kama binadamu kuna mapungufu machache sana, ambayo nina uhakika kama taifa tukishikama sote kwa pamoja, mapungufu haya sio kikwazo cha kutukwamisha kwenda tunapotakiwa kwenda

Itoshe tu kusema, Tanzania tuna bahati sana tena sana ya kumpata Rais Dr John Joseph Pombe Magufuli

Tutakuja kumkumbuka sana kiongozi huyu shupavu na mwenye uzalendo wa kweli

Mungu mbariki Rais Magufuli
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
 
Kwa muda ambao amekuwa madarakan na mambo aliyoyafanya kwa kweli kabsa Mweshimiwa anaitaji kupongezwa na kila mpenda maendeleo amefanya mengi ila mimi nitaorothesha mambo machache 1.kulifufua shirika la ndege la tanzania,viongozi wote waliopita kila mmoja aliimba wimbo wa kulifufu hili shirika lakini miaka 10 ilipita tulichoambulia nikuambia michakato inaendelea kwa mweshimiwa kazi imeonekana ndege zimenunuliwa na watu wanapanda pamoja na kwamba walisema ni mbovu,2jambo la pili hostel za chuo cha kikuu cha dar es salaam ilikuwa ni moja ya kilio cha muda mrefu cha wanafunzi wa chuo hicho imetumika billion kumi majengo ya meonekana tena mazuri 3 jambo la tatu miradi ya barabara za juu ubungo na tazara wakati wa utawala wa mzee mkapa meya wa jiji mzee Kimbisa kama sijakosea jina alizungumzia sana suala la kujenga barabara za juu kwa ajili ya kupunguza folen mjini aliondoka ikabaki story mwenshimiwa Magufuli yeye amefanya kazi kila mwenye macho anaona,watanzania tufike mahali panapo itaji kusifia tusifie mazuri nilazima tuyasema tusiwe tunasubiri mabaya tu ndiyo tupinge kelele yanapotokea mazuri tuyaseme pia tena tuyaseme kwa nguvu wakati tukisubiri ripoti ya kamati inayochunguza mchanga wa thahabu ni vizuri tukiri kuwa mweshimiwa Magufuli kazi anafanya na zinaoneka
 
Wapendwa baada ya raisi wa mioyo ya watu kupoa imechangia wafuasi wake kumbeza kwa sasa wamebaki kufuatilia utendaji uliotukuka wa serikali ya awamu ya tanoo.
Hakika awamu ya 5 hongereni sikuhizi kona zote nyie ndo mnatajwaaa
MUNGU AWABARIKI
 
Hapa Kazi Tu imempeleka Lowasa kwa Buriani. Siasa zitamshinda soon
 
Hapa Kazi Tu imempeleka Lowasa kwa Buriani. Siasa zitamshinda soon
Nimesoma Songea boys huwa nikiona unavyolidhalilisha hili jina na LIZA huwa naumia sana Lizaboni ni kitongoji cha wajanja Songea we fala sijui umetoka wapi unajizalilisha kwa buku 3.kuteuliwa kwenyewe huteuliwi kazi kumbwela tu
 
Ni ukweli usiopingika Rais Magufuli ameanza kutumia busara na hotuba zake zimeanza kupunguza ubabe, kejeli na majigambo. Kwa mbali, ameanza kuthamini hisia za watu.

Pamoja na haya Magufuli ni mwanasiasa licha ya yeye kutaka kulazimisha awe tofauti na wenzake.

Nisingependa kutolea mfano jinsi Bashite alivyotudhihilishia hilo, lakini ukweli upo wazi. Takribani miezi kumi iliyopita Mh Rais aliwaondoa vijana kwenye ajira kwa kisingizio cha uhakiki. Takwimu zinaonyesha kuwa wafanyakazi takribani 19,000 waliondolea kwa kuwa hawakuwepo kazini na wanafuatia na hawa wa sasa hivi na kufanya jumla kuu kuwa karibu na 30,000. Bajeti iliyopita waliahidi kuajiri vijana 70,000+. Matokeo yake ameajiri vijana takribani 7000+.
Ukiangalia net effect ni redundancy ya watu 22,000+ licha ya uwepo wa taasisi nyingi kuajiri kimya kimya wakati wa sasa hivi na kukosekana kwa uwazi kuliko wengi tunavyodhani. Ushahidi upo.

Magufuli yuleyule akiongea na waandishi Ikulu alisema zuio lile limekwisha muda wake. Lakini kwenye majukwaa watu wanalalamika. Walipewa mikataba hawajarudi makazini. Hawafahamu hatma yao.

Ila kwa kuwa Magufuli ni engineer wa siasa, aliamua kuajiri madaktari wale waliokuwa waende Kenya akiacha vijana wanaohangaika kusubiri neno uhakiki.

Leo umewaahidi vijana unaotegemea maombezi kwao kwa mujibu wa maneno yako waajiriwe ili wakuombee, kiuhalisia, kauli yako ni ya kisiasa iliyokosa ushawishi wa kisiasa na hivyo kuwa siasa za kiinjinia.
 
Yaani Bashite pekee ndo kawaokoa baadhi ya ma-RC na ma-DC toka kwenye kadhia ya uhakiki.
 
Salam ndg zangu.

Kwanza kabisa niweke wazi, mm sina chama. Mm napenda mtu mchapakazi, awe wa CUF, CCM, CHADEMA, nk.

Mh Rais, Dk JPM amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania wanakuwa na maisha mazuri, si wanyonge, si matajiri.

Toka ameaingia madarakani amekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya taifa letu. Mh Rais n mkweli sana na yuko wazi.

Watumishi hewa, likizo hewa, pensheni hewa, posho hewa, wanafunzi hewa, mishahara hewa, mikataba hewa siyo vitu vidogo jamani.Tuache uvyama.

Wakurugenzi hewa amewapiga chini wengi kwa makosa mbalimbali yanayoisababishia hasara serikali. Hii siyo hatua ndogo jamani. Haogopi mtu kwa jina lake, cheo chake, historia yake, fedha zake nk. Anapiga chini tu.

Bilioni 800 kulipa mishahara hewa kwa mwaka si hela ndogo. Sasa amezuia. Wapigaji walikuwa wengi sana.

Mtoto wa maskini ambaye amesoma, anakosa kazi. N kwasababu ya watu wachache wajanja wajanja tu, hawajasoma wala nini.

Tukaze buti.
 
Bashite.
Screenshot from 2017-04-28 13-46-51.png


Swissme
 
Rais anajua anachokifanya.
Ipo siku hawa wakosoaji wakuu watamtumia kama Rejereo wakiwaponda viongozi wengine kwenye nafasi kama yake.
Inahitaji utulivu wa nafsi kuelewa mazuri yake ili ushauri anapopungua ingawa Mazuri ni mengi na Yanatufaa sisi walala hoi.
 
Salam ndg zangu.

Kwanza kabisa niweke wazi, mm sina chama. Mm napenda mtu mchapakazi, awe wa CUF, CCM, CHADEMA, nk.

Mh Rais, Dk JPM amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania wanakuwa na maisha mazuri, si wanyonge, si matajiri.

Toka ameaingia madarakani amekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya taifa letu. Mh Rais n mkweli sana na yuko wazi.

Watumishi hewa, likizo hewa, pensheni hewa, posho hewa, wanafunzi hewa, mishahara hewa, mikataba hewa siyo vitu vidogo jamani.Tuache uvyama.

Wakurugenzi hewa amewapiga chini wengi kwa makosa mbalimbali yanayoisababishia hasara serikali. Hii siyo hatua ndogo jamani. Haogopi mtu kwa jina lake, cheo chake, historia yake, fedha zake nk. Anapiga chini tu.

Bilioni 800 kulipa mishahara hewa kwa mwaka si hela ndogo. Sasa amezuia. Wapigaji walikuwa wengi sana.

Mtoto wa maskini ambaye amesoma, anakosa kazi. N kwasababu ya watu wachache wajanja wajanja tu, hawajasoma wala nini.

Tukaze buti.

"Mh Rais ni mkweli sana na yuko wazi"

Mh! Hata mimi sina chama, Ila hapo kwenye bold umenishangaza sana, are you for real?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Yapo mambo wanafanya vizuri na mengine tunaweza sema yamewashinda, mf suala la sukari ni wazi limewashinda wamebaki kuumiza wananchi.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom