Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Magufuli ndio rais pekee alie fanya wapinzan waone tume ya uchaguz Sio huru kwa sababu. Wamekosa hoja za kujadili wameona wafe na tume hii ikiwashinda wataanza kupambana na kwann rais ni mweusi
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Rais Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Rais Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee wa madili wote watamchukia Rais Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali fulani!

Tuwafichue wote wanaopanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

Habari zaidi, soma =>Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tutampima kwa matokeo kama vifaa vya kutosha mahospitalini, madawa ya kutosha, wafanyakazi wa kutosha hasa elimu na afya, vitendea kazi vya kutosha mashuleni, wanafunzi wenye sifa elimu ya juu wote wanapata mikopo, barabara nzuri, maji salama, umeme wa uhakika, uchumi wa mtu mmoja mmoja umekua n.k hatutampima kwa ziara maofisini

kipengele cha kwanza una maoni gani hadi sasa
 
Leo Ni Mei mosi mwaka wa tano Sasa wafanyakazi wameambulia patupu, Mimi kwa upande wangu sioni cha maana alichofanya kuwazidi waliomtangulia. Tena wao walifanya mambo mengi ambayo yamewafanya wakumbukwe Hadi Leo.

Kabla hatujamchinja kwenye sanduku la kura tuambie amefanya nini cha maana.
 
Serikali nyingi Afrika huwa hazitegemei Sanduku la Kura ili kusalia Madarakani,huwa yanafanyika Maigizo flani hivi kuaminisha Dunia ni kama vile Kula na Kipofu.
 
Leo Ni Mei mosi mwaka wa tano Sasa wafanyakazi wameambulia patupu, Mimi kwa upande wangu sioni cha maana alichofanya kuwazidi waliomtangulia. Tena wao walifanya mambo mengi ambayo yamewafanya wakumbukwe Hadi Leo.

Kabla hatujamchinja kwenye sanduku la kura tuambie amefanya nini cha maana.
Huu ndio uwe mwaka wa kumuadhibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bia yetu,
Ivi mtu kama wewe wakiona comment yako ndugu zake mama Rwakatare, Maige na Yule wa Mwanza wanajisikiaje ? hii ishue ya corona ni nzito sana aisee na ni ubish wa magufuli ndio umetufikisha hapa, ataenda nchi ya ahadi pekeyake ? watu wanapukutika aisee

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Yan sijawah kuona nchi yenye watu wajinga na wapumbavu kama TANZANIA, yan na dhoruba yote hii waimba mapambio yakusifu na kutukuza bado wapo ??

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Akihubiri Kanisani kwake leo askofu Gwajima amewawekea video clip ya hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa leo Ikulu ndogo ya Chato.

Askofu Gwajima amesema alichofanya Rais Magufuli ni ujasiri ambao haujawahi kuonyeshwa na kiongozi yoyote duniani.
Hotuba hii ingetolewa na Trump wa USA au Johnson wa UK ingekuwa ndio habari kuu ya dunia kwa sasa lakini kwa sababu imezungumzwa na kiongozi wa Afrika haitapewa uzito wa juu.

Gwajima amesema siyo kwamba anamfagilia Rais Magufuli bali ukweli ni kwamba Dr Magufuli ni chaguo la Mungu.
 
Askofu wa wajinga, aangalie kwanza kashfa alizonazo za kueneza ukabila na kadhalika kabla mtu hajamsikiliza askofu wa wajinga.
 
Back
Top Bottom