Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Herode
Mzee wa Mifadhaiko alipoona mhanga wa Risasi ni mzima yuko Nairobi akatuma watu(kina Samia)
Mhanga yule akarudi, wakaanza kuweweseka, imekuwaje risasi 16 zishindwe wakati 3 huwa zinamaliza kila kitu?
 
TISS wanapaswa kuelewa huyu mtu hafai kuongoza miaka 5 mingine, au lasivyo taifa atalimaliza kabisa na ataleta machafuko.

Hafai kabisa, ana ubaguzi wa wazi kabisa wa ukabila na uchama. Ni hatari kuliko COVID19.
 
Viva CCM Viva magufuli
Mungu mbariki magufuli
Karibu sana Karibu Sana...lakini hebu tulia kidogo, nikuulize kaswali kadogo tu. Kama wewe ndio ulikuwa Magufuli, ungewaambia nini wazazi wa Ben Saanane?

Ungemwambia nini mama yake ambaye amelia kwa miaka minne hadi machozi yamemkauka akisubiri ripoti ya alipo mwanaye?

Ungemwambia nini baba yake ambaye kwa miaka minne amehuzunika akitamani tu siku ifike ampe mazishi mwanaye kama mauti yalimfika?

Kweli ungekuwa na ujasiri wa kuomba kura zao ili uendelee kuwa Rais? Sasa nakuuliza, huu uthubutu alio nao Rais Magufuli je kautoa wapi?
 
Amefanya kazi kubwa sana ya kuua upinzani upinzani umekufa kabisa.
2.Amefanya kazi kubwa sana ya selikali yake kupiga wabunge risasi.
3.Amefanya kazi ya selikali yake kupoteza watu.
4.selikali yake imefanya kazi kubwa sana ya kuajiri vijana.
5.selikali yake imefanya kazi kubwa sana ya kuteka watu.

Hakika JPM amslefanya kazi kubwa sana
Upinzani upi umekufa
 
Karibu sana Karibu Sana...lakini hebu tulia kidogo, nikuulize kaswali kadogo tu. Kama wewe ndio ulikuwa Magufuli, ungewaambia nini wazazi wa Ben Saanane?

Ungemwambia nini mama yake ambaye amelia kwa miaka minne hadi machozi yamemkauka akisubiri ripoti ya alipo mwanaye?...
Niwambie nini? Kila siku watu wanakufa kwa kunyongwa kupigwa/mapanga/nondo/mishale/mikuki/risasi au huyo saa 8 ndio kiumbe Cha Kwanza kufa? Kwahiyo mtu akifa au kuuliwa basi raisi awajibike? Unaishi sayari gani ndugu? Mungu mbariki magufuli
 
*Anaandika Mwl M.H .Wage kuhusu mafanikio ya #JPM katika sekta ya kilimo.*

[emoji2936] *#JPM* Ameongeza pato la Taifa linalotokana na Kilimo kwa 17% toka trilioni 25.2(2015) mpaka trilioni 29.5(2019).
[emoji2936] *#JPM* Amefanya sekta ya Kilimo sasa ichangie 28.2% ya pato la Taifa na kuajiri 58% ya watanzania.

[emoji2936] *#JPM* Amefanya nchi ijitosheleze kwa Chakula kwa 121%.
[emoji2936] *#JPM* Ameongeza uzalishaji wa mazao makuu ya biashara Pamba, Korosho, Kahawa, Chai, Pareto,Tumbaku, Mkonge toka Tani 796,502(2015) mpaka 1,144,631(2019).

[emoji2936] *#JPM* Ameongeza upatikanaji wa Pembejeo toka Tani 36,614,28(2015) mpaka 76,725,52 mwaka 2015 ongezeko la 110%
[emoji2936] *#JPM* Ameongeza uzalishaji wa ndani wa mbegu bora toka tani 2,060,497(2015) mpaka tani 6,917,317(2020) ongezeko la 53%.

[emoji2936] *#JPM* Ameongeza thamani ya mauzo ya mazao ya bustani(Horticulture) toka dola milioni 412(2015) mpaka dola milioni 779(2019) na kuchangia 38% ya pesa zetu za kigeni.
(Tumeanza kupeleka bidhaa za mboga na maua katika soko la ulaya moja kwa moja).

[emoji2936] *#JPM* Ameimarisha upatikanaji wa Mbolea kwa pamoja(Bulk Procurement System) unaosaidia kupata mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu.
[emoji2936] *#JPM* Ameongeza Idadi ya Viwanda vya mbolea nchini toka 4(2015) mpaka 13(2019).
[emoji2936] *#JPM* Ameanzisha jumla ya Viwanda 189 vya kuchakata mazao ya Kilimo.

[emoji2936] *#JPM* Amefuta ushuru wa tozo za ada 105 kupunguza nyingine 4 Kati ya 146.
[emoji2936] *#JPM* Ametekeleza kikamilifu mkakati wa Taifa wa vijana kushiriki katika kilimo(NSYIA) toka uliozinenduliwa 2016 ili kuwavutia vijana kushiriki katika kilimo, mikoa 12 na halmashauri 81 zinatekeleza mpango huu.

[emoji2936] *#JPM* Ameongeza eneo la kilimo Cha umwagiliaji toka hekta 461,326(2015) hadi 694,715(2020)
[emoji2936] *#JPM* Amerejesha mali za ushirika ndani ya miaka mitano zilizoporwa na kuuzwa kinyume na utaratibu.
Kutoka NCU(Mwanza),SHIRECU 1984(Shinyanga),KNCU(Kilimanjaro).

[emoji2936] *#JPM* Kupitia wakala wa taifa wa kuhifadhia chakula amejenga maghala ya kisasa na vihenge na Kuongeza uwezo wa nchi wa kuhifadhia chakula toka tani 251,000 hadi Tani 501000.

mohamedwage09@gmail.com
Screenshot_20200907-103743_1.jpg
Screenshot_20200907-103909_1.jpg
 
Naamini humu jamvini wapo vijana wako na watakufikishia taarifa hii na nyingine nyingi zinazoandikwa na wanajamii forum.

Kila jambo lililo jema linalopigiwa kelele na wapinzani kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu lifanyie kazi wakati huu wa kampeni. Tunaamini serikali bado ipo. Endeleeni kuboresha na kuweka mikakati mbalimbali ya kupambana na kila changamoto inayoibuliwa na wapinzani kwani kwa kufanya hivyo kufikia October 28 mashimo yote yatakuwa yamesha sawazishwa na njia itakuwa nyeupe.
 
Naunga mkono hoja. Magufuli kushinda ni lazima hilo halina ubishi kwa upinzani wa sera za ubwabwa na kuku rosti njia ni nyeupe mpaka ikulu
Rungwe mnamuonea tu!Wala yeye hapambani kushinda,hapa ni CCM vs CHADEMA,basi!So ukisema upinzani uwe unarefer CDM!
 
Naamini humu jamvini wapo vijana wako na watakufikishia taarifa hii na nyingine nyingi zinazoandikwa na wanajamii forum.

Kila jambo lililo jema linalopigiwa kelele na wapinzani kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu lifanyie kazi wakati huu wa kampeni. Tunaamini serikali bado ipo. Endeleeni kuboresha na kuweka mikakati mbalimbali ya kupambana na kila changamoto inayoibuliwa na wapinzani kwani kwa kufanya hivyo kufikia October 28 mashimo yote yatakuwa yamesha sawazishwa na njia itakuwa nyeupe
Mengi yamefanywa silaha kubwa ya wapinzani imebaki katika ajira, ILANI imeahidi mil.8 vijana wengi wana iman na nyie CCM msiwaangushe
 
Rungwe mnamuonea tu!Wala yeye hapambani kushinda,hapa ni CCM vs CHADEMA,basi!So ukisema upinzani uwe unarefer CDM!
Hahahaha hata yy anamalengo ya kuelekea ikulu mkuu angekuwa hana nia angeacha kama alivyofanya TLP chama chochote kile kilichobeba form ya urais ujue ni mpinzani Wa CCM
 
Back
Top Bottom