Bora hata kwa wasomali huko na wa caribeean sio tishio sana, Mnaijeria anapindia meza juu chini aisee.
Tatizo la black Americans wengi huwaza kupata pesa kwa uhalifu, kulewa madawa ya kulevya, kuwaona wanawake kama bitches ama hoes, n.k
Wanaijeria hawanaga ujinga huu
..mimi nina mtizamo tofauti kidogo na wewe.
..kwa kiasi fulani nakubaliana na malalamiko na machungu walionayo Wamarekani weusi.
..binafsi sijui akili zangu zingekuwaje kama ktk Tanzania yetu ancestors wangu wangekuwa wameshikwa UTUMWA na kubaguliwa kwa muda mrefu.
..tatizo la Wamarekani weusi siyo la kuliangalia juujuu tu. tunatakiwa tujielimishe kuhusu nini kilitokea kwa hawa ndugu zetu na athari zake kwa vizazi na vizazi.
..wengine mnasahau kwamba Wamarekani weusi walikuwa wanabaguliwa mpaka miaka ya 60 wakati ambapo Watanganyika tayari tulikuwa huru.
..Malcolm X aliuwawa mwaka 1965. Na Martin Luther King Jr ameuwawa mwaka 1968. Kwa maana hiyo hawa ndugu zetu walikuwa wanabaguliwa wakati sisi Watanzania tukiwa huru.
Je Waafrika wanateka nafasi, na kuziba fursa, za Wamarekani Weusi?
..Jibu langu ni NDIO.
..Wanigeria, Waghana, etc wanapofika Marekani na kupata uraia wanaanza kutambuliwa kama "Blacks", yaani ni sawa na Mmarekani mweusi ambaye ni mzao wa waliokuwa Watumwa. Lakini huyu Mnigeria, Mghana, etc hajapitia changamoto na matatizo waliyopitia Wamarekani weusi.
..Jambo lingine ni kwamba Mnigeria, Mghana, anayeweza kusafiri na kufika Marekani mara nyingi ni mtu ambaye ana ELIMU, hivyo siyo sahihi kumuweka ktk kundi moja na Mmarekani mweusi ambaye hana elimu ya kutosha, amekulia ghetto, na ametunzwa ktk familia ya mzazi mmoja.
..Nimeangalia kidogo kuhusu Mnigeria Adewale "Wally" Adeyemo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha wa Marekani. Huyu bwana wazazi wake walihamia Marekani toka Nigeria. Baba yake alikuwa mwalimu, na mama yake alikuwa nesi. Mpaka hapo utaona kwamba huyu bwana hakukulia "uswazi" au ghetto. Inawezekana kabisa alikuwa na maisha na makuzi mazuri kuliko hata Wamarekani weupe. Lakini linapokuja suala la fursa anachukuliwa kama "Black", na Joe Biden anapewa sifa kwamba ameteua Mmarekani mweusi ktk nafasi kubwa.
..Kwa hiyo mpaka hapo mtaona kwamba wapo watu ambao hawastahili kupewa nafasi zilizotengwa kwa Black Americans lakini wanazichukua. Na Wamarekani weusi wana haki ya kulalamika kwamba wanapunjwa. Na matukio na namna hiyo yapo mengi.
..Nadhani kabla ya kuwalaumu Wamarekani Weusi ni vizuri tukajielimisha kuhusu historia yao. Mimi ktk kujielimisha kwamba nimeshangazwa sana na jinsi gani waliweza ku-survive unyama waliokuwa wakifanyiwa. Zaidi, nimekutana na Wamarekani weusi ambao wanasonga mbele ktk maisha pamoja na kwamba jamii yao inapitia ktk ubaguzi wa waziwazi, na mwingine wa kificho.
NB:
..Kuna Mmarekani mweusi ni kocha wa timu ya american football alikuja hapa Tanzania na kujitolea kujenga shule maeneo ya Umasaini.