Mafanikio ya Wanaijeria waishio Marekani yanawakera sana Wamarekani weusi wazawa

Hao black Americans wanadai umasikini wao umesababishwa na biashara ya utumwa, hivyo wanatakiwa walipwe fedha kama fidia, vyuoni wapewe nafasi maalumu za upendeleo, kampuni yoyote inayoajiri lazima iwatengee nafasi maalumu za ajira.

Hao jamaa ni watu wa ovyo sana
 

hiyo mijamaa ndani ya vichwa vyao imejaa fikra za kibaguzi, lakini wao ndio haweshi kulalamika wanabaguliwa
 
Siwezi kubishana na wewe kuhusu wanaijeria.

Nitakuwa napoteza muda ila ukweli ni kuwa wanaijeria ni matapeli hata uandike kitabu kizima.

Kwanza wewe ni me au ke?
Nataka kujua kwa nini unawatetea
 
Wapopo ni wapambanaji sanaaaa, na ni watu wa kuthubutu,

..Nigeria ina watu 206 millioni, na eneo la nchi yao ni 357,000 square miles.

..Tanzania ina watu 60 million, na eneo la nchi yetu ni 365,000 square miles.

..Watanzania tukiendelea kuzaana kwa wingi, na tatizo la ajira lisiposhughulikiwa, tutakuwa na "uthubutu" kama wa Wanigeria.
 

..mimi nina mtizamo tofauti kidogo na wewe.

..kwa kiasi fulani nakubaliana na malalamiko na machungu walionayo Wamarekani weusi.

..binafsi sijui akili zangu zingekuwaje kama ktk Tanzania yetu ancestors wangu wangekuwa wameshikwa UTUMWA na kubaguliwa kwa muda mrefu.

..tatizo la Wamarekani weusi siyo la kuliangalia juujuu tu. tunatakiwa tujielimishe kuhusu nini kilitokea kwa hawa ndugu zetu na athari zake kwa vizazi na vizazi.

..wengine mnasahau kwamba Wamarekani weusi walikuwa wanabaguliwa mpaka miaka ya 60 wakati ambapo Watanganyika tayari tulikuwa huru.

..Malcolm X aliuwawa mwaka 1965. Na Martin Luther King Jr ameuwawa mwaka 1968. Kwa maana hiyo hawa ndugu zetu walikuwa wanabaguliwa wakati sisi Watanzania tukiwa huru.

Je Waafrika wanateka nafasi, na kuziba fursa, za Wamarekani Weusi?

..Jibu langu ni NDIO.

..Wanigeria, Waghana, etc wanapofika Marekani na kupata uraia wanaanza kutambuliwa kama "Blacks", yaani ni sawa na Mmarekani mweusi ambaye ni mzao wa waliokuwa Watumwa. Lakini huyu Mnigeria, Mghana, etc hajapitia changamoto na matatizo waliyopitia Wamarekani weusi.

..Jambo lingine ni kwamba Mnigeria, Mghana, anayeweza kusafiri na kufika Marekani mara nyingi ni mtu ambaye ana ELIMU, hivyo siyo sahihi kumuweka ktk kundi moja na Mmarekani mweusi ambaye hana elimu ya kutosha, amekulia ghetto, na ametunzwa ktk familia ya mzazi mmoja.

..Nimeangalia kidogo kuhusu Mnigeria Adewale "Wally" Adeyemo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha wa Marekani. Huyu bwana wazazi wake walihamia Marekani toka Nigeria. Baba yake alikuwa mwalimu, na mama yake alikuwa nesi. Mpaka hapo utaona kwamba huyu bwana hakukulia "uswazi" au ghetto. Inawezekana kabisa alikuwa na maisha na makuzi mazuri kuliko hata Wamarekani weupe. Lakini linapokuja suala la fursa anachukuliwa kama "Black", na Joe Biden anapewa sifa kwamba ameteua Mmarekani mweusi ktk nafasi kubwa.

..Kwa hiyo mpaka hapo mtaona kwamba wapo watu ambao hawastahili kupewa nafasi zilizotengwa kwa Black Americans lakini wanazichukua. Na Wamarekani weusi wana haki ya kulalamika kwamba wanapunjwa. Na matukio na namna hiyo yapo mengi.

..Nadhani kabla ya kuwalaumu Wamarekani Weusi ni vizuri tukajielimisha kuhusu historia yao. Mimi ktk kujielimisha kwamba nimeshangazwa sana na jinsi gani waliweza ku-survive unyama waliokuwa wakifanyiwa. Zaidi, nimekutana na Wamarekani weusi ambao wanasonga mbele ktk maisha pamoja na kwamba jamii yao inapitia ktk ubaguzi wa waziwazi, na mwingine wa kificho.

NB:

..Kuna Mmarekani mweusi ni kocha wa timu ya american football alikuja hapa Tanzania na kujitolea kujenga shule maeneo ya Umasaini.
 
Siwezi kubishana na wewe kuhusu wanaijeria.

Nitakuwa napoteza muda ila ukweli ni kuwa wanaijeria ni matapeli hata uandike kitabu kizima.

Kwanza wewe ni me au ke?
Nataka kujua kwa nini unawatetea
Amewafahamu kupitia stori za vijiweni. Nimeishi nao mbele wale sio watu kwenye hela na zaidi hawatosheki na hata akiwa na kazi nzuri pembeni lazima atakuwa dili chafu drugs, magendo, utapeli na ushirikina ndo usiseme kafara za kutisha nje nje nimezishuhudia.
...Kama ni ke walishapuliza long time
 

..Watanzania tukizaana na kufikia watu million 206, na tusipotatua tatizo la ajira, tutakuwa kama Wanigeria.
 
Mkuu, niliyoyashuhudia na kujifunza kutoka kwa watu wa kenya, nigeria, philippines, india, bangladesh na ethiopia wanaoishi nje nilijiona mwenye bahati sana kuwa mtanzania. Kutokana na idadi kubwa ya watu huko kwao hakuna ardhi, hakuna ajira so kama umezaliwa kutoka familia masikini utakufa hivyo hivyo, utataka kufanya kibarua lakini mwenye kibarua hana hela ya kulipa unafika wakati unasubiri tu mungu akuchukue.
Tuache kabisa hizi fikra za eti wazungu wanatuonea wivu kwasababu tupo wengi na wakati huo huo hatutaki kuangalia maisha ya watu wa hizo nchi nilizozitaja.
 
Mkuu hizo dimension zako sio za kweli aisee

Unaijua 365 square mile kweli?? hio ni area ndogo mno hata Dodoma kubwa zaidi ya hapo tena sana .
 
Mkuu hizo dimension zako sio za kweli aisee

Unaijua 365 square mile kweli?? hio ni area ndogo mno hata Dodoma kubwa zaidi ya hapo tena sana .

..kweli.

..nilitaka kusema Tanzania ina eneo lenye ukubwa wa 365,000 square miles.
 
Hawa watu walichotushinda ni population na mfumo wa kuanza kusafiri mapema lakini siyo wajanja kama wanavyokuzwa,kuna mafala wengi tu wa kipopo wakiingia kingi hata mbongo anawapiga.
 
Napenda sana guts zao hao jamaa ni next level

Kingsmann
Ukitokea kaya maskini lazma uwe na guts. Mfano mie sahizi nipate fursa ya kuingia mamtoni lazma ntakaza sana yani sio kipole pole. Kule kazi ya kijinga tu ya mtaani inaweza kukupa maisha freshi kabisa ukala mpaka dollar mia au zaidi kwa masaa 8 tu. Bongo kazi gani ya kitaa itakupa laki 2?

Ila wenzetu wazawa wana privileges nyingi na serikali inawathamini zaidi ila hizo fursa za hali ya chini hawazichangamkii..Mfano kufanya kazi Laundry, Ku deliver mizigo, kubeba box, kufagia mabarafu and the like. Hizo kazi za hivyo kwao sio kazi wala kwa caucasians wa ki US ndio kabisaa hawagusi.
 
Wanaijeria wanachukiwa kwa sababu ya utapeli na kuwalaghai wanawake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…