Mafao wanayopata wenza wa viongozi wakuu wastaafu ni kufuru

Huyo wa Msoga achana naye.
 
Kufuru inafikiwa baada ya vigezo vipi?

Je, mlinganisho wa mafao na posho umefanywa na nchi zipi?
====================
Hivi majuzi tu watu walikuwa wakilalamika Mama Maria Nyerere katelekezwa- Mama yetu wa Taifa alisota sana-sasa amepata mafao stahiki mnataka myaondoe?

Mnasahau manufaa yanayopatikana ya muda mrefu.

Kutoa mafao na posho kwa Viongozi hao na wenza kunaweza kuwavutia wagombeaji wa Urais ambao hawatakuwa na mawazo ya kuingia madarakani na kuanza kuchota mabilioni wakianza kufikiria misoto aliyopata Rais Nyerere na Mama Maria miaka ya nyuma.

Vilevile, tukichukulia mafao hayo kama uwekezaji, yaani Investment in stability.

Utaona inaweza kuwakatisha tamaa viongozi wa zamani kutafuta mamlaka kwa njia zisizo za kidemokrasia au kuingilia chaguzi alaimradi wanaoenda kuchaguliwa watakuwa wakiwapendlea katika Biashara zao n.k

Nafikiri tusubiri tuone manufaa au hasara ya marekebisho ya sheria baada ya miaka 15 hivi.
 
Tumzungumzie mama Salma kikwete na Bibi sitti mwinyi na Bibi khadija..

Mme wa salma yupo na anadeal kibao tu..
Watoto wake (Japo sio wa kuwazaa) wapo na hata Ridhiwani Ni Mbunge na Naibu waziri..

Yeye mwenyewe ni Mbunge na Anapokea pesa iliyotakata tu..

Twende kwa sitti na Hadija..
Wana wao ni Wabunge na Wengine mawaziri na Hata Rais pia wanaye (Hussein,Abasi na Abdallh mwinyi)

Walikuwa wanahitaji booster za nini????
 
Kumbe nchi hii ina hela sijui inashindwa nini kuwapa manesi walimu na maaskari hela zao zote wakistaafu mpaka serikali inaanza kusumbuka kubuni sheria ya ajabu ajabu iitwayo kikokotoo!Ambacho kimepelekea hao wastaafu kupata mafao ya aibu
 
Pesa za Madini, Pesa za Utalii, Pesa za Bandari zinaishia mifukoni na Familia zao tu.

Tumepigwa
 
Huu sasa ndo uvunjifu wa amani

Why?

1. Cheo cha u Rais kitatafutwa kwa gharaama yeyote hata kwa damu, sio utumishi tena ni serious unfairness.

2. Hii unfairness itawauma wazalendo wa kweli walio kwenye mfumo, watainuka wasalitu.

3. Huwezi tesa watu mda wote kwa dhuluma, elastic limit itafikiwa tu na watu wataondokwa na hofu.

4. Mungu Hapendi dhuluma na watu wakilalamika sana atapitisha fagio/azabu.

........ angalieni hii kiburi ya ccm
 

Watanzania wengi masikini, huduma za kijamii sehemu nyingi azijafika, wazazi wanajifungua kwa shida sana vijijini, umeme shida, matozo kibao bila ya msingi.

Itafika kipindi kwa ugumu wa maisha watu watakuwa awana tena ofu wala woga, tuombe sana mungu. Masikini ndo wanapata shida sana hicho kidogo chao wanakitafuta kinakatwa kodi, mara tozo mara sijui nn.

Masikini ndo milija ya kuwalisha matajili ndomana miaka yote masikini anaendelea kunyonywa bila huruma.
 
Mume nae katupiga kwenye mikataba ya gas bado ana share zake kwenye makampuni ya madini kama ile ya kule Arusha, kama ni baraka tu, hii familia imebarikiwa hapa duniani, sujui huko mbinguni..

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Hapa duniani wamefunga mkataba na shetani ndo maana wanamuua yeyote anayetishia ama kuongilia maslahi yao
 
Kama wenye nchi tumekubaliana na hali, kwa nini watu wasile mema ya nchi....
 
Kabla Samia hajatoka Madarakani wata extend hadi kwa Mke/Mme wa Waziri mkuu, Mkuu ww majeshi,IGP, Jaji mkuu, Spika wa Bunge na Mawaziri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…