Mafao wanayopata wenza wa viongozi wakuu wastaafu ni kufuru

Mafao wanayopata wenza wa viongozi wakuu wastaafu ni kufuru

Kule Mbeya wanashukuru kwa kujengewe vyoo na Japani
FB_IMG_1709622231274.jpg
 
Kufuru inafikiwa baada ya vigezo vipi?

Je, mlinganisho wa mafao na posho umefanywa na nchi zipi?
====================
Hivi majuzi tu watu walikuwa wakilalamika Mama Maria Nyerere katelekezwa- Mama yetu wa Taifa alisota sana-sasa amepata mafao stahiki mnataka myaondoe?

Mnasahau manufaa yanayopatikana ya muda mrefu.

Kutoa mafao na posho kwa Viongozi hao na wenza kunaweza kuwavutia wagombeaji wa Urais ambao hawatakuwa na mawazo ya kuingia madarakani na kuanza kuchota mabilioni wakianza kufikiria misoto aliyopata Rais Nyerere na Mama Maria miaka ya nyuma.

Vilevile, tukichukulia mafao hayo kama uwekezaji, yaani Investment in stability.

Utaona inaweza kuwakatisha tamaa viongozi wa zamani kutafuta mamlaka kwa njia zisizo za kidemokrasia au kuingilia chaguzi alaimradi wanaoenda kuchaguliwa watakuwa wakiwapendlea katika Biashara zao n.k

Nafikiri tusubiri tuone manufaa au hasara ya marekebisho ya sheria baada ya miaka 15 hivi.
Then tunaomba msaada wa kujengewe vyoo?
FB_IMG_1709622231274.jpg
 
Kwa uliyoandika, japo mengine umeapproximate kwa sababu zako za kisiasa, hakuna shida juu ya hayo malipo.

Labda kama na wewe mleta uzi ungeleta mawazo yako iwaje!! Sio kulalama tu bila suluhisho wala mbadala.

Ila kwa nature ya wapinzani na wananchi wa Tz kwa ujumla, huu uzi unatosha kuleta tafrani mitandaoni hasa twitter na jf.

Note: twitter (X) na  jf tu na sio huko mtaani kwa wasioijua hii mitandao ya kijamii.
 
Napenda hii angle yako ya kufikiri...I just hope waliopendekeza Sheria hii ndicho walichokikusudia na ndicho kitakachofanyika...less than that Sheria hii inaenda kutengeneza dynasties...na zikikaa zikajikusanya vizuri...zitatawala hii nchi mpaka yesu arudi....
 
Kwa akili kama hizi zako huwezi ona shida,
 
kwa sisi ambao baba zetu walifariki mapema na kutuacha na mzazi mmoja tena asiye na ajira joto lajiwe tunalijua..

jamani unyonge mnyongeni ila haki yake mpeni aheni wapate hiyo hela hawa wake wa viongozi hizo pesa hawali peke yao wanamsululu wa wananchi wanawagongea kuja kuwaomba msaada hapo bado vikundi vya wanawake wenzake vinamuangalia yeye..

mfano mama maria bibi yetu yule pale watoto na wajukuu wote analea pale wapo nyumbani wanategemea mafao hayo ndio waishi.
alafu ingekuwa hayo mafao yamewafanya kuwa matajiri wakubwa hapo ningesema sawa ila wengi wao wanaishi kawaida tu. hawana makuu wamama wa watu.
mimi kwa hili naipongeza serikali sana sisi.
 
Napenda hii angle yako ya kufikiri...I just hope waliopendekeza Sheria hii ndicho walichokikusudia na ndicho kitakachofanyika...less than that Sheria hii inaenda kutengeneza dynasties...na zikikaa zikajikusanya vizuri...zitatawala hii nchi mpaka yesu arudi....
Taifa la wajinga lazima tutawaliwe nao
 
Tanzania = Tanganyika + Zanzibar 🙏

• Mke wa Mwl, Julius K. Nyerere, Maria Nyerere.
• Wake wa Ali H. Mwinyi, Sitti na Khadija Mwinyi.
• Mke wa Benjamin W. Mkapa, Anna Mkapa
• Mke wa Jakaya M. Kikwete, Salma Kikwete
• Mke wa John P. Magufuli, Janeth Magufuli
• Mume wa Samia S. Hassan, Hafidh Ameir

Kwa mujibu wa The Political Service Retirement Benefits Act [CAP. 225] kila mwezi hawa watalipwa 60% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani.

Kama Rais aliyepo madarakani anapokea TZS 50,000,000 kwa mwezi, mwenza wa Rais atalipwa malipo/mafao ya TZS 30,000,000 kila mwezi.

Rais akistaafu, mwenza/wenza wake atapokea/watapokea (kwa mkupuo) 25% ya mshahara wa Rais alioupokea wakati wote akiwa madarakani.

Mfano, kama Rais alikaa madarakani kwa kipindi cha miaka 10, akalipwa TZS 4,000,000,000, mwenza wake atalipwa TZS 1,000,000,000 kwa mkupuo.

Pamoja na malipo hayo ya fedha, pia wenza hawa sita (6) wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watapata mafao mengine kama ilivyoelekezwa;

1. Nyumba ambayo Rais alipewa na alikuwa akiitumia kama makazi baada ya kustaafu itakuwa mali yake halali baada ya mume/mke wake (Rais) kufariki.

2. Atapokea posho ya matengenezo ya kila mwezi katika maisha yake yote akiwa hai kiasi ambacho ni sawa na 60% ya mshahara wa Rais aliye madarakani.

3. Mke/mume wa Rais atatibiwa ndani na nje ya Tanzania, na matibabu yake yatagharamiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

4. Mjane wa Rais mstaafu atapata huduma ya magari mawili, na dereva wawili kufanya shughuli zake za kila siku. Serikali inalipia gharama za mafuta.

5. Magari anayopewa mjane wa Rais yatabadilishwa baada ya miaka 5. Kuna maintenance allowance. 60% ya mshahara wa Rais aliye madarakani kila mwezi

6. Malipo ya fedha kulipa mishahara kwa kiwango cha kima cha chini cha mishahara ya watumishi kwa; dereva, mpishi, mfua nguo na mtunza bustani

7. Mke/mume wa Rais atapata huduma ya usafiri kwa gharama za serikali hadi mahali pa kuishi kwa maisha yake yote hadi pale ambapo kifo kitawatenganisha.

8. Mke/mume na watoto wanapata ulinzi kutoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kutokana na mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Usalama wa Taifa.

9. Gharama za mazishi ya mke/mume wa Rais yatakuwa chini ya serikali. Serikali ya Tanzania itagharamia kwa 100% msiba wa mwenza wa Rais

10. Mjane wa Makamu wa Rais, anapata stahiki kama za mjane wa Rais isipokuwa tofauti yake ni moja, atapata gari moja la Serikali na dereva mmoja.

#Martin Maranja Masese #Termus #DevOps
Acha iwe hivyo coz;-

Kama taifa tuliamua KAZI kubwa inayolipa Santa iwe siasa kuliko usomi na ueledi was elimu yoyote ile!!

Hilo ni janga la kisera na msimamo kama nchi!!

Tanzania itapata maendeleo ya kweli tutakapoamua mapesa meeengi yasijazwe kwenye siasa!!
 
Pesa zote hizo na bado wanaomba misaada kutoka nje ata sielewi mm hapa kuna formula gani, pesa zote hizo ilikuwa akuna haja ya kuomba mikopo nje wala misaada wakati tuna pesa sana
Viongozi wameweka masrahi yao mbele,hawajali wengine kabisa. Kwa ujumla ni ulafi tu
 
Huyo Mama Salma Kikwete angetuhurumia kidogo.

Huyo anakula hizo "kufuru zote" hapo juu, bado anaongezea posho za bungeni, mshahara wa ubunge, na kiinua mgongo kinachofikia milioni 200 baada ya miaka mitano ya ubunge wake kwisha.

Huyu kama akijua mbinu za uwekezaji anaweza kuitwa bilionea siku sio nyingi, akawaajiri vijana wa kitanzania, lakini kama ndio zile akili zetu za ngomani, anaweza akawa ndio kwanza anawaza 2025 atarudi vipi bungeni aendelee kutukamua wajinga.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Huyu mama ana huruma
Bado na mtoto pia ni mbunge na ni N/waziri pia
Hii nchi inaoongozwa ki chief
 
Back
Top Bottom