Tanzania = Tanganyika + Zanzibar 🙏
• Mke wa Mwl, Julius K. Nyerere, Maria Nyerere.
• Wake wa Ali H. Mwinyi, Sitti na Khadija Mwinyi.
• Mke wa Benjamin W. Mkapa, Anna Mkapa
• Mke wa Jakaya M. Kikwete, Salma Kikwete
• Mke wa John P. Magufuli, Janeth Magufuli
• Mume wa Samia S. Hassan, Hafidh Ameir
Kwa mujibu wa The Political Service Retirement Benefits Act [CAP. 225] kila mwezi hawa watalipwa 60% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani.
Kama Rais aliyepo madarakani anapokea TZS 50,000,000 kwa mwezi, mwenza wa Rais atalipwa malipo/mafao ya TZS 30,000,000 kila mwezi.
Rais akistaafu, mwenza/wenza wake atapokea/watapokea (kwa mkupuo) 25% ya mshahara wa Rais alioupokea wakati wote akiwa madarakani.
Mfano, kama Rais alikaa madarakani kwa kipindi cha miaka 10, akalipwa TZS 4,000,000,000, mwenza wake atalipwa TZS 1,000,000,000 kwa mkupuo.
Pamoja na malipo hayo ya fedha, pia wenza hawa sita (6) wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watapata mafao mengine kama ilivyoelekezwa;
1. Nyumba ambayo Rais alipewa na alikuwa akiitumia kama makazi baada ya kustaafu itakuwa mali yake halali baada ya mume/mke wake (Rais) kufariki.
2. Atapokea posho ya matengenezo ya kila mwezi katika maisha yake yote akiwa hai kiasi ambacho ni sawa na 60% ya mshahara wa Rais aliye madarakani.
3. Mke/mume wa Rais atatibiwa ndani na nje ya Tanzania, na matibabu yake yatagharamiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
4. Mjane wa Rais mstaafu atapata huduma ya magari mawili, na dereva wawili kufanya shughuli zake za kila siku. Serikali inalipia gharama za mafuta.
5. Magari anayopewa mjane wa Rais yatabadilishwa baada ya miaka 5. Kuna maintenance allowance. 60% ya mshahara wa Rais aliye madarakani kila mwezi
6. Malipo ya fedha kulipa mishahara kwa kiwango cha kima cha chini cha mishahara ya watumishi kwa; dereva, mpishi, mfua nguo na mtunza bustani
7. Mke/mume wa Rais atapata huduma ya usafiri kwa gharama za serikali hadi mahali pa kuishi kwa maisha yake yote hadi pale ambapo kifo kitawatenganisha.
8. Mke/mume na watoto wanapata ulinzi kutoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kutokana na mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Usalama wa Taifa.
9. Gharama za mazishi ya mke/mume wa Rais yatakuwa chini ya serikali. Serikali ya Tanzania itagharamia kwa 100% msiba wa mwenza wa Rais
10. Mjane wa Makamu wa Rais, anapata stahiki kama za mjane wa Rais isipokuwa tofauti yake ni moja, atapata gari moja la Serikali na dereva mmoja.
#Martin Maranja Masese #Termus #DevOps
MABADILIKO YA SHERIA YA MAFAO YA VIONGOZI NA FAMILIA ZAO:
Jina la sheria - THE POLITICAL SERVICE RETIREMENT BENEFITS ACT, (CAP. 225)
"THREAD"
BADILIKO 1:
Ongezeko la kifungu kipya cha 9A ambacho hakipo kwenye sheria kinachotaja mafao ya mke/mume wa rais mstaafu. Baada ya rais kustaafu, mwenza/wenza wake atapokea kiasi cha fedha (kwa mkupuo) sawa na 25% ya mshahara wa rais alioupokea katika kipindi chote alichokuwa madarakani. Yaani, kama rais alikaa madarakani kwa miaka 10, akalipwa mshahara wa TZS 3B, basi mwenza wake atalipwa TZS 750M, fedha ambayo inalipwa kwa mkupuo.
BADILIKO 2:
Kwenye kifungu cha 11 kinachohusu mafao ya mjane wa rais mstaafu (survivor's pension) ambapo kwa sasa kila mwezi mjane hulipwa 40% ya mshahara wa rais aliye madarakani. Asilimia imeongezwa na sasa mjane atalipwa 60%. Mfano kama rais anapokea TZS 30M kwa mwezi, basi mjane wa rais atalipwa TZS 18M kila mwezi.
BADILIKO 3:
Ongezeko la kifungu kipya cha 12A ambacho hakipo kwenye sheria kinachotaja mafao ya mke/mume wa makamu wa rais mstaafu. Baada ya makamu wa rais kustaafu, mwenza/wenza wake atapokea kiasi cha fedha (kwa mkupuo) sawa na 25% ya mshahara wa makamu wa rais alioupokea katika kipindi chote alichokuwa madarakani. Yaani, kama makamu wa rais alikaa madarakani kwa miaka 10, akalipwa mshahara wa TZS 2B, basi mwenza wake atalipwa TZS 500M, fedha ambayo inalipwa kwa mkupuo.
BADILIKO 4:
Kufutwa kwa kifungu cha 13 ambapo makamu wa rais anapofariki akiwa madarakani, au baada ya kustaafu (kabla hajalipwa mafao yake), mwenza wake, atalipwa (survivor's pension) sawa na 40% ya mshahara wa makamu wa rais aliye madarakani, na stahiki nyingine zilizoelezwa kwenye jedwali la sheria hiyo, ikiwemo nyumba, matibabu na mengine mengi. (kifungu hiki kimefutwa).
Kifungu kipya cha 13 ambapo makamu wa rais anapofariki akiwa madarakani, au baada ya kustaafu (kabla hajalipwa mafao yake), wategemezi wake (dependants) watalipwa kiasi cha fedha sawa na mshahara wote wa makamu wa rais alioupokea wakati akiwa madarakani. Mfano, kama makamu wa rais alikaa madarakani kwa miaka 10, akalipwa TZS 2B kama mshahara, basi wategemezi wake watalipwa kiasi hiko cha TZS 2B kama pension. Ifahamike, kwa mujibu wa sheria hii, neno "dependants" limefafanuliwa kwenye kifungu cha 4, na maana yake ni mke au wake, mume, watoto (ambao walikuwa ni tegemezi kwa marehemu), pamoja na wazazi wa marehemu (wategemezi).
Pia, mke wa marehemu (makamu wa rais) atalipwa fedha (survivor's pension) kila mwezi sawa na 40% ya mshahara wa wa makamu wa rais aliye madarakani kwa sasa. Pia, atapata stahiki nyingine zilizotajwa kwenye jedwali la sheria hii.
BADILIKO 5:
Kifungu cha 14 kimeongezwa kifungu kidogo cha "4" kinachotoa haki ya "msaidizi wa kazi" mmoja kwa mtu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu kabla ya sheria hii kutungwa. Hapa tunazungumzia Mawaziri wakuu wastaafu wakati wa Mwalimu.
BADILIKO 6:
Ongezeko la kifungu kipya cha 14A ambacho hakipo kwenye sheria ya sasa> Kifungu hiki kinataja mafao ya mke/mume wa Waziri Mkuu mstaafu. Baada ya Waziri Mkuu kustaafu, mwenza/wenza wake atapokea kiasi cha fedha (kwa mkupuo) sawa na 25% ya mshahara wa Waziri Mkuu alioupokea katika kipindi chote alichokuwa madarakani. Mfano, kama Waziri Mkuu ameshika madaraka kwa miaka 10, akalipwa mshahara wa TZS 1B, basi mwenza wake atalipwa TZS 250M, fedha ambayo inalipwa kwa mkupuo (lump sum).
BADILIKO 7:
Kifungu cha 15(2) kimefanyiwa nyongeza ya neno "granted monthly", ambapo kwa sheria ya sasa, kifungu hiki kinamtaja mjane wa Waziri Mkuu kupokea kiasi cha fedha 40% ya mshahara wa Waziri Mkuu aliye madarakani. Kilichoongezeka ni kwamba, hiki kiasi atakuwa analipwa KILA MWEZI.
BADILIKO 8:
Kifungu cha 18(2) kimefanyiwa nyongeza ya neno "granted monthly", ambapo kwa sheria ya sasa, kifungu hiki kinamtaja mjane wa Spika wa Bunge kupokea kiasi cha fedha 40% ya mshahara wa Spika aliye madarakani kwa sasa. Kilichoongezeka ni kwamba, hiki kiasi atakuwa analipwa KILA MWEZI.
BADILIKO 9:
Badiliko la JEDWALI la sheria hii linalotaja nyongeza ya mafao ya viongozi.
1. Rais mstaafu ameongezewa idadi ya magari kutoka magari 2, sasa atapata magari 3 yasiyopungua uzito wa tani 3 (yaani hawezi pewa Corola, bali ni gari kubwa kama V8 n.k, ambapo atapewa magari mapya kila baada ya miaka 5.
2. Rais mstaafu ameongezewa idadi ya madereva toka 2 na sasa atapewa 3.
3. Sheria ya sasa inataja gharama za mazishi kwa rais mstaafu tu, nyongeza iliyowekwa ni gharama ya mazishi kwa mwenza wake. Yaani kama rais mstaafu atafiwa na mke/mume wake, basi Serikali itagharamia mazishi hayo.
4. Makamu wa Rais mstaafu ameongezewa idadi ya magari kutoka gari 1, sasa atapata magari 2 yasiyopungua uzito wa tani 3 ambapo atapewa magari mapya kila baada ya miaka 5.
5. Makamu wa Rais mstaafu ameongezewa idadi ya madereva toka 1 na sasa atapewa madereva 2.
6. Makamu wa Rais atajengewa nyumba ya kifahari. Ikumbukwe, kwa sheria ya sasa, ni Rais mstaafu pekee ndiye anajengewa nyumba.
7. Sheria ya sasa inataja gharama za mazishi kwa Ma