Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, salaam.
Mimi mmoja wa watu nilikuwa nakufuatilia sana na kukubali kisiasa, toka ukiwa waziri awamu za nyuma, Rais, na sasa Rais mstaafu.
Kwa sasa unlikuwa unafit sana nafasi ya Elder Statesman, mwanasiasa mwandamizi nchini, ambaye kwa uzoefu wake kulitumikia Taifa ungetumika kama point of reference kwa mambo yote nchini , kisiasa na kiuchumi.
Lakini cheo hiki cha Elder Statesman kina gharama ya kuishi above controversy, yaani mtu asiwe na figisu zozote.
Tuje kwenye kichwa cha mada.
Umetudissapoint mzee, tena sana.
You are not in control of your wife.
Mswaada uliopitishwa na bunge, kwa msukumo mkubwa wa mke wako Salma Kikwete, wananchi hawakuufurahia.
Hiyo ni kuutumia vibaya umaarufu wa Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwamba umaarufu wa Kikwete umetumika kujilimbikizia mali, hilo halijakaa vizuri.
Siingii kwenye uchambuzi wa mafao yenyewe, lakini kiuhalisia kuutumia umaarufu wa jina la Kikwete kujilimbikizia mali, ambazo ni kodi za wananchi, sipepesi macho huo ni ufisadi wa fedha za umma.
Namalizia kwa kusema, sijui kama swala la mafao ya wake za viongozi, kama lilivyosukumwa na mama Salma, je? Je, lilipita chujio la familia ya Kikwete?
Na je? Kikwete anaweza tokea hadharani kutetea hilo?
Wasalaam mzee Kikwete, bado una muda wa kudhibiti mihemuko ndani ya familia yako.