Mafundi makochi Mungu anawaona!

Mafundi makochi Mungu anawaona!

Nina visofa vyangu nilinunua laki 3 mwaka wa 12 huu naendelea kutumia, nilivikarabati mara moja. Nilikuwa na mpango wa kuvitupa au kugawa nibadilishe na mpya, kama mambo yako hivyo ngoja niendelee kuvikarabati tu, maana hakuna namna..
 
Kuna sofa niliikuta kwa Mzee Fulani kigogo serikalini,nikakaribishwa nikakaa,ni kama umekalia puto,mnabishana wewe unaibonyeza yenyewe inkurudisha juu,unabaki unanesa.miaka 7,narudi tena pale anaishi kigogo mwingine na sofa ni ile ile na ubora ule ule.kutafiti bei nikakuta ni 13 mln set.

Jamani hela zitafutwe popote ziliko.

kuna fundi nilimkuta kituo kipya gongo la mboto,yeye nauza 1.3 ml set,nikakuta malighafi anayotumia si ya kuungaunga inaridhisha ingawa sofa lake haliwezi kuishi miaka saba hata iweje,kwa hiyo hela ndio changamoto kuu ya bidhaa mbovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi niliisha apa kuwa sitanunua "tenga la nyanya" lililofunikwa vizuri na kitambaa na kuwa kochi. Nitaendelea kukalia mninga wangu na kubadilisha mito tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Makochi ya mafundi wa Bongo mengi hata ukikaa hu-balance vizuri. Unajikuta unainamia kwa mbele zaidi au kwa nyuma zaidi.
 
Wewe ulianza story yako kwa ku refer mafundi wa hapa bongo, ndio maana wadau wakakushangaa kwa kutaja hiyo bei ya 5ml
Ndio ziko kochi za kiswahili mitaani hadi 5mil. ndio ninazozungumzia! Kwa macho utadhani imported kumbe kanjanja ndo nimesema wamuogope Mungu!
 
We nunua godoro na mbao ita fundi home atengeneze unaona mpk mwisho


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sawa fundi Benja,weka namba zako basi
Sio wote. Me sofa zangu nafanya kubadilisha kitambaa tu na pale ninapotaka style mpya. Fundi wangu yupo tanga sabasaba pembeni ya tanga pazuri Ana center kubwa kiasi anaitwa Benjamin makoko. Huwa naingia gharama za usafiri za kuniletea popote nilipo maana huwa sikai Tanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni kwamba nyinyi hamfiki bei , una pesa ya tecno ila unataka kitu chenye ubora wa Iphone..haipo hiyo mkuu

Ninasema hivyo kwasabu nina ofisi ya furniture , chini ya mil 2.. Huwez pata sofa ya uhakika wa kudumu walau miaka 5 na kuendelea ...mwenye mil 1 atapata bidhaa ya mil 1.. Mwenye mil 3 atapata bidhaa ya mil 3 ... Iko hvyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Unapiga misasa mingapi on average hizo mbao zako hadi kutoa kitu chenye hadhi ya 5m? Kwenye hio karakana yako kuanzia namba 60?
 
Back
Top Bottom