Mafundi simu wa upande wa hardware naomba tukutane hapa

Huo mtambo ni mtambo ambao unasaidia sana ktk mambo ya hardware,unaweza kutoa ama kuweka aina yoyote ya ic bila matatizo yoyote tofauti na blower,blower wakati mwingine kwa fundi asie jua kubalance joto na upepo huweza kuharibu simu badala ya kuitengeneza tatizo ni bei ghali sana ila ni nzuri sana
 
Mkuu huo mtambo unaweza ukawa bei gani?
 
Na kama nataka kujifunza kutengeneza simu ninapaswa kufanyaje?
Ukitaka kujifunza ufundi simu kwanza mtafute fundi ambaye yupo karibu na maeneo unayo ishi. Jaribu kushinda naye hata week moja. akuelekeze mawili matatu. yani uujue ule mwanzo tu.
kama kufungua simu. kuunga mic speaker. Kubadilisha vioo kuweka system chaji nk.
Harafu baada ya hapo mambo mengine utajiongeza mwenyewe. kwa kugoogle na akili yako zaidi.

Ila tambua ufundi hardware hauna mwisho na inafaa ujifunze vitu vipya kila siku Ili uendane na wakati. kwasababu nayo matatizo ya simu yanazaliwa Mapya kila siku.
 
Tupe hizo hatua mtalam
 
Karibu sana mkuu tuongezane ujuzi.
 




Wakuu inawezekana hili TATIZO LA HUAWEI Y300 kujiwasha na kisha kuonesha INAJICHAJI ni tatizo kubwàaaaaà?

Mafundi wawili wameishindwa.

kubadili IC charging bado haijawa suluhu nin tatizo hapa wakuu
 




Wakuu inawezekana hili TATIZO LA HUAWEI Y300 kujiwasha na kisha kuonesha INAJICHAJI ni tatizo kubwàaaaaà?

Mafundi wawili wameishindwa.

kubadili IC charging bado haijawa suluhu nin tatizo hapa wakuu
Hiyo simu achana nayo haitengenezeki itakupotezea muda bure
 
Safi sana tena unapotengeneza mteja anakuona inajenga imani 'It builds confidence to a customer'
Mambo vp mkuu
Nina tecno W4 ilizima gafla nikiwa naangalia video haionyeshi chochote kwenye screen ila nikiichomeka charger inawasha taa nyekundu tatizo linaweza kuwa lipi
 
Wadau mi nina Techno Y2 ina miezi mitatu tangu niinunue lakini siku nne baada ya kui ununua ikaanza kujizima niliporudi dukani wakanambia labda tatizo ni betri wakanipa betri nyingine lakini hali ikawa ni ileile.
Ikijizima haiwaki mpaka utoe betri halafu uirudishie.
Nimeongea na watu kadhaa wanaomiliki simu kama hii wameniambia kuwa wana tatizo hilo hilo.
Waungwana naomba ushauri wenu kuhusu tatizo hili.
Natanguliza shukrani
 
Mambo vp mkuu
Nina tecno W4 ilizima gafla nikiwa naangalia video haionyeshi chochote kwenye screen ila nikiichomeka charger inawasha taa nyekundu tatizo linaweza kuwa lipi
Hyo taa inablink au unawaka moja kwa moja???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…