Mafuriko makubwa mjini Ifakara leo Mei 5

Mafuriko makubwa mjini Ifakara leo Mei 5

Hali ni mbaya. Maji ni mengi mji wa Ifakara kwa 80% upo kwenye maji.

Hasara ni kubwa haswa kwa wafanya biashara za hardware. Cement na gipsam zimeharibika kwa kiwango kikubwa.

Kuna baadhi ya familia zinahitaji msaada.

Mtuombee.
Mkuu tuwekee picha/video basi na uzi ushibe vizuri
 
Huo mto hapo ifakara si umejaa, hapo darajani je?
Darajani ni mto Kilombero. Huu unaoleta mafuriko hapa ni mto Lumemo.

Mto Lumemo una Kona kali sana kwa ivo maji yakiwa mengi na yenye Kasi Lazima yamwage Kuna eneo linaitwa Kwa Shungu.

Tatizo kalavati la kutoa maji Kwa shungu ni Moja tu.
 
Yaan kwa haya majanga ya kimbunga na mvua nyingi ulimwenguni na hata hapa Tanzania kuna baadhi ya mikoa imekuwa salama kabisaa bila hata kudhurika na majanga yaliyamo kuanzia wilaya...kata...mitaa na vitongoji vyake...ni kwamba imebarikiwa....? Poleni sana
 
Back
Top Bottom