GE2025 Mafuriko ya askari polisi na wanajeshi barabarani leo kulikoni?

GE2025 Mafuriko ya askari polisi na wanajeshi barabarani leo kulikoni?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
M gen z yamekuwa tishio na ngumu kujua kiongozi wake wamdhibiti, ma gen z wameamua kuachana na wanasiasa hata wa upinzani hawana imani nao tena, wanajifanyia mambo yao kukiwasha watakavyo. Hawa mgamga wanakimbiakimbia mitaani kutisha wananchi wasilete fyokofyoko kuelekea uchaguzi ujao. Sia ajabu akaibuka kiongozi wa kijeshi atamke neno la kitisho kwa wananchi watulie wasifurukute, huyo kiongozi anaweza kushurutishwa ajitokeze kwenye media apige mkwara wananchi watulie wasilete za kuleta kuelekea uchaguzi mkuu. Viongozi wa dini wanapuuzwa kutuliza mizuka ya wananchi na wengine wapo upande wa wananchi. Mambo ni mengi kuelekea uchaguzi mkuu
 
Hao Hao wanajeshi watapiga kura hata Kama watu hawatokwenda kupiga kura. CCM wahuni sana
hawa ni wahuni waliokubuhu kwelikweli, wameshindikana, ni wahuni sugu. Angalia wanavyofanya kampeni zao mwaka huu, ni wao tu ndio wametawala anga na ardhi wanajifanyia abrakadabra kwenye kampeni watakavyo. Hawatasita kufanya manuever kwenye uchaguzi kama kawaida yao!
 
1759468581579.png


Wanafanya Route March.
 
Wakifanya hivi siku ya uchaguzi wananchi hawatajitokeza kwenye vituo vya kupiga kura, labda wavae kiraia na wasibebe silaha. Hawa wanaweza kuharibu uchaguzi kwa akili hizi
2015 ilikua hivi na watu walijitokeza kupiga kura ila wahalifu hawawez jitokeza
 
Leo ijumaa kila sehemu au kila kikosi kuna kuwa na root match kwa kiswahili zoezi la kaza mwili hutembea kulingana na mkuu wa kikosi atakavyo amua ni KM ngapi ila huanzia 8km msitishe watu hayo yana fanyika sana kila ijumaa
 
nyie mmesema mnataka kuangusha serikali kwa hiyo wawaache tu maana maandamano yenu lengo serikali ianguke
Mwanachi kuangusha serikali sio jambo rahisi Mzee, hapo huwa ni wana usalama wakiwa kwenye sare za kiraia
 
Acha kupotosha, Wapi JWTZ wameshindwa kulinda mipaka ya nchi? Wapi JWTZ kaja kupandana na wewe mtaani?
Bandari yetu inamilikiwa na Oman jwtz wamelala usingizi
Twiga wanapanda ndege jwtz wamelala usingizi
Madini Tanzanite inatoroshwa jwtz wamelala usingizi
Ngorongoro ardhi ya Masai inamilikiwa na UAE, Kuna minara Yao jwtz wamelala usingizi
Watanganyika wenzetu wanaotekwa na kuuliwa JWTZ wamelala usingizi

Hao wanalinda mipaka Gani?
Au hujui majukumu ya jeshi la wananchi kwenye katiba na yepi
 
Acha kupotosha, Wapi JWTZ wameshindwa kulinda mipaka ya nchi? Wapi JWTZ kaja kupandana na wewe mtaani?
Kule mara maasai wa Kenya Wana ingiza mifugo yao Nchini Tena mbugani miaka nenda rudi. Rwanda the same.

Mtwara je , Magaidi wanaingia na kutoka

Majambazi ya Kenya yanakuja kuua wafanyabiashara matajiri na wenye kuleta ushindani wa viwanda vya Kenya na kurudi mchana siku hiyo hiyo .

Acheni siasa nchi Iko katika Hali mbaya
 
Hiyo ndio njia ya kutatua changamoto za wananchi?....
Unaposhindwa kutimiza wajibu na kubaki kubwabwaja tu hii ndio inabaki njia pekee...
Ila muda ni mwalimu mzuri sana!
 
Back
Top Bottom