binti kiziwi
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 11,201
- 28,642
Hiyo sentensi ya mwisho haiko sawa mkuu. Kikubwa mwambie wifi ajue aina ya ngozi aliyonayo itamsaidia kununua mafuta yanayoifaa ngozi yake au yanayodeal na tatizo husika la ngozi yake, ukimuona mtu anahangaika na ngozi muache na zaidi sana mtie moyo sababu katika uimara wa afya ya akili, ngozi yenye afya inachangia kwa asilimia kadhaa, kikubwa asinunue “vipako” by vipako namaanisha mafuta haya yanayotengenezwa na watu ambao sio chemists, hayajulikani yana mchanganyiko wa nini na nini kisayansi.Nisha tumia mwaka wa 15 huu, cha kushangaza ngozi yangu ipo vizuri kuliko wife mwenye mabegi mawili ya mafuta.
Ngozi ziko tofauti , mwingine ana tatizo la ngozi kweli kweli, Kwahiyo akisema atumie product moja kama wewe hatoboi, hawa si wengine bali ni watu wenye acne prone skin na wenye sensitive skin au combination ya vyote.
Kama uwezo upo, mwache ahangaike na ngozi yake, asisahau kucheki homone.