Tanzania tunatumia akili sana hatukurupuki hata siku moja, na hata hili tutashinda Kama tulivyoshinda Vita vya ukombozi, M23, Idd Amin na tulivyoishangaza dunia tulivyoishinda Corona.
1) Msumbiji ni nchi huru hatupaswi kuingilia mambo yao hadi watakapotuomba kuwasaidia.
2) Hata wakituomba tuwasaidie lazima tupime maji kabla ya kupeleka majeshi kichwa kichwa kama KDF ilivyojipeleka Somalia, tukiona tunaweza kushinda hiyo vita peke yetu bila madhara makubwa, tutakwenda, vinginevyo tutawasiliana ili twende kama SADC.
3) Sasa hivi tumeweka majeshi yetu kule mpakani, Hakuna hata Sungura anaweza kuingia kutokea Msumbiji.
Jambo moja ninakuhakikishia kwamba iwe itakavyokua, wale magaidi watafutwa kama tulivyowafuta Kibiti wakakimbilia Masumbiji. Hivi tunavyofanya ndio Kenya ilipaswa kufanya, sio kukimbilia kuingia Somalia wakati mpaka wa Kenya na Somalia upo wazi Alshabab wanaingia Kenya kwa urahisi.
Sent from my TECNO-L8 using
JamiiForums mobile app