Magari gani ya kununua nyakati hizi kwa kijana?

Magari gani ya kununua nyakati hizi kwa kijana?

I love BMW hasa X5 hizi advanced models. Zile za zamani body yake mbayaaaa...
Napenda hillux[emoji4] ford ranger, sijui namara... kiujumla napenda magari makubwa. Sitaki december niende na kamkebe nikabaguliwe[emoji23][emoji23][emoji23] ila sina hela ila jamani rumion, sijui probox sijui nn. Si bora ninunue carina ti. Unakuta kisharobaro kinaendesha rumion yake kimeweka wave, kinepaka supa black, amevaa supra midosho halaf amekaa kiupande anaendesha kamkebe kake anajiokitea warembo tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi Karibuni nilikua naona IST ndo y vijana ila naona zimejaa nyingi na pia kuna wimbi kubwa la wizi wa IST

Vijana wenye hela naona wanakimbilia Crown maana sahivi zimejaa sana

Naombeni maoni yenu kua ni gari gani sahivi inafaa kijana wa uchumi wa kati ?
BMW X1 au BMW X3
 
Watu wengi wamekuwa wanajiuliza, ni kwanini kwa sasa IST zipo nyingi mitaani, zinaibiwa zaidi au kuibiwa vipuri vyake. Haya ni baadhi ya majibu yake.

1. IST ndio gari inayopendwa kutumika zaidi mijini na watu wengi kuliko gari yoyote kwa sasa.

2. Ndio gari yenye soko la uhakika zaidi katika kuuza au kununua. (Ukitaka kuuza au kununua Ist hutahangaika sana)

3. Ni gari imara zaidi kwa mizunguko ya mijini miongoni mwa magari madogo.

4. IST ni gari yenye muonekano na utulivu wenye kuvutia wengi miongoni mwa magari madogo.

5. IST ni miongoni mwa magari yenye gharama nafuu za mafuta, vipuri na services.

6. IST ni gari imbayo mafundi wengi wanaweza kuitengeneza ikiharibika, kwa gharama nafuu.
 
Gari aina ya Toyota IST ndio pendekezo langu namba moja la gari ya kununua kwa kijana yoyote wa mjini mwenye mojawapo ya sifa hizi.

1. Anapambana kwa hali na mali kufikia ndoto za kumiliki gari kwa mara ya kwanza.

2. Amekata tamaa za kuendelea kumiliki gari baada ya kupata mateso ya kumiliki aina nyingine ya magari kwa mara ya kwanza.

3. Kipato chake cha kimaisha kwa mwezi kiko katika uchumi wa kati. (Chini ya shilingi milioni moja kwa mwezi).

4. Hana papara wala mbwembwe nyingi za maisha ya kushindana katika ujana.

5. Anapambana kutaka kutimiza ndoto nyingine nyingi na nzuri katika maisha yake ya sasa (Kwa mfano kuoa au kuolewa, kuwa na mtoto, kujenga nyumba, kusaidia ndugu na jamaa wa karibu, kufungua biashara nk)
 
1622048766813.png

Jaa humo na hii maxima 2019 kwa kuendea ofisini,safari zako za hapa mjini na viti vinafaa sana seats are very comfortable hata kwa kutolea huduma za imarjensia mheshimiwa
 
Hii ndo shida ya IST

Naskiki kesi za kuibiwa spare za IST na kuibiwa magari zinaongezeka. Niliambiwa pia unakuta muda mwingine funguo za IST zinaingiliana

Mimi natafuta gari la kimkakati kama kijana mwenye malengo ya maisha ya mbeleni
Gari gani la kimkakati?!
 
Mshanichanganya sijui hata ninunue ipi..manake zote mshaziponda
Nunua kwa mujibu wa uwezo wako kifedha, pia uangalie na consumption ya mafuta hasa kwa hapa Dar ambapo foleni haziepukiki. Usije jikuta umenunua gari unashindwa hata kuiendesha siku tatu kwa wiki kutokana na utumiaji wake mkubwa wa mafuta. Ukiwa ni mfanyakazi wa serikali basi nakushauri usizidishe gari ya cc 1500.

Pia utazame urahisi wa kupata spares kama unaweza kupata hapa au lazima uagize kutoka nje. Pia inahitaji service na maintenance nyingine ambazo utakuwa unatumia pesa tu.

Ukinunua mgari mkubwa utaishia kutumia fedha tu hasa ukiwa huna chanzo chengine cha fedha (utageuka chuma ulete).
 
Back
Top Bottom