Mazingira gani yanayotunzwa na magari ya umeme! Hio Lithium inapatikana vipi na huo umeme wa kuchajia izo betry unapatikana vipi! kuzidisha load tu kwenye grid.
Ili ujue kama umeendesha gari, usikie engine inavonguruma! other than that utakuwa unaendesha scooter ya maringi manne na cabin tu.
Hata hizi electric vehicles kama ukitaka zitoe sauti kubwa hilo linawezekana sana tu mbona.
Na sauti zitakuwa ni halisi na wala siyo mimic sound, sababu ni ukweli kwamba motor ya gari za umeme nazo pia huzalisha sauti kama ambavyo motor zingine zozote vile zinavyozalisha sauti wakati zikizunguka.
Tukumbuke hata Mashine ya Kusaga Nafaka nayo ni motor ya umeme na huwa inazalisha sauti kubwa tu, ndiyo ni motor kama motor ya kwenye gari za umeme.
Rejea umeme ni nishati (energy), na nishati ya umeme inaweza kubalishwa kuwa sauti (sound energy).
Hata speakers za simu yako ndiyo kitu zinachofanya, zinabadilisha electric signal into sound waves, kisha sauti inasikika.
Vivyo hivyo kwa Combustion Engine za gari za petrol na diesel, ile sauti inakuja kutokana na Nishati ya Kikemikali iliyomo kwenye Mafuta kuunguzwa na kuzalisha nishati nyingine ikiwemo nishati ya sauti (sound energy) inayotoka katika injini.
Energy can neither be created nor destroyed, but it can be transformed from one form into another.
Namalizia kwa kuandika hivi, katika electric vehicle kinachofanyika ni kwamba kwenye gari kuna Motor ambayo hufanya kazi ya kubadilisha Nishati ya Umeme (Electrical Energy) ili iwe Nishati ya Kimakenika (Mechanical Energy).
Injini za Petrol au Diesel hizi hubadilisha Chemical Energy ya Petrol au Diesel ili iwe Mechanical Energy.
Mechanical Energy ndiyo inayozungusha gari, na kufanya gari lijongee.
Pia motor za electric vehicles inapozunguka huwa inazalisha sauti pia. Sema tu ile sauti ni ndogo sana.
Lakini ukitaka electric vehicles nazo zizalishe sauti kubwa, Kitaalamu hiyo inawezekana kabisa.
Ni kama Motor na mfumo mzima wa Machine ya Kusaga Nafaka zinavyotoa sauti.. Ndiyo motor ya machine ya kusaga Nafaka inafanya kazi kama vile Motor ya Gari za Umeme tu.
Motor zote hubadilisha umeme (electrical power) ili kuwa Mechanical Energy, ambapo mechanical energy ndiyo huzungusha kitu na kufanya kijongee.
Hata Mwili wa Binadamu nao hubadilisha Chemical Energy iliyopo katika Chakula na kuwa Mechanical Energy inayotuwezesha kujongea (kutambaa, kuogelea, kuruka, kukimbia, kutembea etc.)