Magari ya umeme kutoka China hatiani kupigwa marufuku Ulaya

Magari ya umeme kutoka China hatiani kupigwa marufuku Ulaya

NASHANGAA BANDARI YETU INACHAJI KODI BEI KUBWA KULIKO THAMANI ULIYONUNULIA GARI KUTOKA JAPAN WAKATI HAIKUCHANGIA TAIRI WALA SIDE MIRROR LAKINI BADO BEI INAZIDI YA MTENGENEZAJI, HII NCHI SIJUI IMELAANIWA?
Na watu wamekaa kimya yani wenye mamlaka hutakaa kusikia wanaliongelea hilo hata kwa bahati mbaya😀!!!

Lakini yote haya sababu wao wanakula rushwa hivyo maumivu ya maisha hawayafeel. Laiti kila kitu kingefanyika kwa haki sidhani kama upuuzi wa aina hii ungefumbiwa macho.
 
bidhaa zake anauza Bei chini kwa ubora ule ule kuteka soko duniani
Hapa umedanganya watu. Nina simu ya Tecno W3 ya mchina.
Ukiwa kwenye meseji ukaandika neno Facebook au WhatsApp meseji haiendi. Nimejaribu simu 2 za Tecno W3 ila bila bila.
Mchina anauza bidhaa kulingana na hela yako, bidhaa anazopeleka ulaya ni tofauti zinauzwa Afrika. Kuna bidhaa za kichina ukiziona unajua kabisa kuna rushwa ilifanya ili bidhaa ziuzwe hapa Tanzania.
 
Hapa umedanganya watu. Nina simu ya Tecno W3 ya mchina.
Ukiwa kwenye meseji ukaandika neno Facebook au WhatsApp meseji haiendi. Nimejaribu simu 2 za Tecno W3 ila bila bila.
Mchina anauza bidhaa kulingana na hela yako, bidhaa anazopeleka ulaya ni tofauti zinauzwa Afrika. Kuna bidhaa za kichina ukiziona unajua kabisa kuna rushwa ilifanya ili bidhaa ziuzwe hapa Tanzania.
Nadhani umeshapata jibu,hata Panadol ,sukari,nk ya bongo inayokwenda ulaya ni tofauti na za kuuzwa bongo.
Kanunue techno inayouzwa ulaya ulete mrejesho
 
Watengeneze magari ya umeme ili hivi viberiti kama Paso viuzwe laki tano
Mkuu kwanza hawawezi kutengeneza za bei ndogo sana kwa sababu za usalama wa gari lenyewe

Kama Tesla zenyewe zinawaka moto na wanajitahidi kuangalia wamekosea wapi sasa itakuwa mchina atengeneze zitakazokuwa zinalipuka kila wakati?

Haiwezekani kwa masoko ya sasa ni lazima atengeneze kwa standard zinazotakiwa
Kweli kuna baadhi ya tesla zimewaka moto 🇺🇸 ila sio nyingi ni ajali kama ajali tu ila ni la kushtua

Mchina nae atajitahidi kutengeneza kwa kiwango na bei rafiki ila kutegemea na gharama alizoingiza kwa utafiti
 
Shida wale mabwege pale TPA na TRA wanazichaji kodi hizo gari za umeme. Nimeshangaa mno wakati wenzetu wanazichukulia kama faida kwa mazingira zina msamaha wa kodi.
Ili wa discourage watu wasinunue, hofu yao ni kupoteza fedha za tozo wanazopiga kwenye mafuta. Hii nchi hatuoneani huruma hata kidogo
 
Wajerumani wanalia tu wao kila kitu wanadhani watashinda
Hata zamani wao walikuwa wa kwanza kutengeneza solar panels ila mchina alipoiba idea tu alifyatua kama kichaa na bei bwerereeee.

Jamaa wakakasirika wakasema tunataka China apandishe bei China akakataa wakatishia ulaya kuachana nae kibiashara na yeye akasema sinunui Wine za ulaya tena. Ukiangalia Wine wachina wanaagiza nyingi sana toka ulaya ikabidi ulaya waache mzozo

Sasa hili la kuwaogopa hapo 🇬🇧 tayari wana order kibao ya magari hayo na mpaka batteries zinaingia nyingi tu

Mpaka kufikia mwaka 2030 Uingereza watakuwa wameachana na magari ya diesel na petrol kwa pamoja

Hebu na sisi tuache kuwa Nzi tubadilike tuwe Nyuki

Tutafute wawekezaji hapo hapo tz wajenge kiwanda cha kutengeneza Batteries, mbona zamani vilikuwepo? Huyo mganga aliewaroga kamtafuteni sio akili zenu hizo

Dunia inaenda kwa kasi sana na nyie msiwe nyuma na kusubiri kutupiwa magari ya diesel kama nguo za mitumba

Hamuoni hiyo ni wake-up call?
Mkuu sisi hatuna haraka wala hatusumbui bongo zetu kwa issue za technologies, sisi kikubwa ni kupata Kazi/ ajira na kupambana kujenga nyumba kali😄😄😄😄
 
Viongozi wa Nchi za Ulaya ni wajinga sana...

Mmarekani ndio yupo nyuma ya tamko hili.


Ila hii vita hawataiweza , maana kwa vyoyote vile China ata - retalite, na itawa backfire vibaya
 
1694779601458.png
 
Back
Top Bottom