Nimepitia kurasa za mbele za magazeti ya leo yote haya kuonyesha tukio kubwa la ujio wa TAL isipokuwa Mwananchi pekee.
Hii dalili za uoga, mkakati wa wasiojilikana, kuminywa kwa uhuru wa media au?
===
Maoni ya Wachangiaji
Hii dalili za uoga, mkakati wa wasiojilikana, kuminywa kwa uhuru wa media au?
===
Maoni ya Wachangiaji
Kwanza nikusahihishe kidogo. Katika magazeti ambayo angalau yanaonekana kuwa ni magazeti, MWANANCHI na MAJIRA yameiripoti ukurasa wa mbele habari ya ujio wa LISU. Kwamba magazeti mengine hayakuripoti (au yaliipa uzito kidogo kwa kuiweka ndani labda) haliwezi kuwa jambo la kushangaza. Jambo la kushangaza ingekuwa magazeti yote, yakiwemo yanayogharimiwa kumtukana Lissu, yangeipa uzito habari hiyo.
Kama MWANANCHI (ambalo linajitahidi kusimamia taaluma licha ya misukosuko linayokutana nayo) wameripoti hiyo habari inatosha sana. Hivi vipeperushi vinawafurahisha wanaovilipia na kuvigharimia kuchapishwa kwake lakini wala haviuziki wala kusomwa, watu wameishavishtukia. BBC wameipa coverage kubwa sana, Aljazeera wameipa uzito, CNN wameipa uzito. Watu wenye akili wanatazama huko. Startv wameirusha, ITV wameisrusha inatosha. Mitandao ya kijamii imechapisha inatosha kabisa.
Turudi kwenye swali sasa. Je, Hii ni dalili za uoga, mkakati wa wasiojulikana, kuminywa kwa uhuru wa media au......? Hapa jibu lake ni kwamba inawezekana yote haya matatu ni sahihi!