Magazeti karibu yote ya leo yapuuza habari za ujio wa Lissu

Ninavyojua ukifunika chungu kilichopo jikoni ndio kinachemka zaidi.
Nimepitia kurasa za mbele za magazeti ya leo yote haya kuonyesha tukio kubwa la ujio wa TAL isipokuwa Mwananchi pekee.
Hii dalili za uoga, mkakati wa wasiojilikana, kuminywa kwa uhuru wa media au......?
Watashindana lakini hawatashinda.
Yote matatu ni MAJIBU sahihi kabisa.
Wanajimaliza. Wanajikaanga kwa mafuta yao
Mkuu, wamiliki wa magazeti wana watoto wanasomesha na wana ndugu wanawategemea. Hawataki yawakute ya Tanzania Daima na Mwanahalisi
Waache waendelee kuzuia mafuriko kwa mikono! Vyombo vingi vya habari vimekuwa havijiamini na vingine vina hofu ya mkono mbaya wa chama kilichoko Ikulu wakati hata katika nafasi za kura za maoni ya ubunge wana habari karibu wote wamefyekwa!
 
Nimepitia kurasa za mbele za magazeti ya leo yote haya kuonyesha tukio kubwa la ujio wa TAL isipokuwa Mwananchi pekee.
Hii dalili za uoga, mkakati wa wasiojilikana, kuminywa kwa uhuru wa media au......?
Ni kutojitambua na majibu watayapata leo katika mauzo ya siku (yatashuka saana)....tayari wadau tumesusia magazeti hayo...na funzo limeeenea sasa nchi nzima kwamba ukitaka habari za uhakika utazipata kwenye mitandao ya Jamii (i.eJamii forum ikiwa kiongozi)...mbona mara hii wataulewa ule msemo wa "usiache mbachao kwa msaala upitao".....ngoja tuwanyooshe
 
Nimepitia kurasa za mbele za magazeti ya leo yote haya kuonyesha tukio kubwa la ujio wa TAL isipokuwa Mwananchi pekee.
Hii dalili za uoga, mkakati wa wasiojilikana, kuminywa kwa uhuru wa media au......?
Kwani ujio wa Lissu una impact gani kwa taifa? kiasi kwamba wananchi wasipopata hiyo habari basi kuna shida kubwa itatokea katika maisha yao ya kila siku.
 
Shida yako Gulwa unadhani magazeti yaliyopo nchini ni Mzalendo na Habari Leo pekee! Kuna magazeti mengine kibao. Kayasome ndo uje uandike tena.
 
Waache waendelee kuzuia mafuriko kwa mikono! Vyombo vingi vya habari vimekuwa havijiamini na vingine vina hofu ya mkono mbaya wa chama kilichoko Ikulu wakati hata katika nafasi za kura za maoni ya ubunge wana habari karibu wote wamefyekwa!
Hawajafyekwa ila hawakupata kura za kutosha, bado wanayo nafasi ya kuteuliwa na vikao vya juu! Ndiyo maana ilikuwa ni lazima yatokee hayo yaliyotokea
 
Nimepitia kurasa za mbele za magazeti ya leo yote haya kuonyesha tukio kubwa la ujio wa TAL isipokuwa Mwananchi pekee.
Hii dalili za uoga, mkakati wa wasiojilikana, kuminywa kwa uhuru wa media au......?
Yaani unataka Mgeni akipona tu na kurudi nyumbani aandikwe front page?. Ameshapona shukuru Mungu basi.
 
Pia ongeza na" Kujipendekeza kwa wamiliki na wahariri wa media zetu" rejea hotuba ya mh rais kwa TAKUKURU.
 
Watoa pesa wanafuatilia mtu wao, jana kilibuma sana.. pangechapika hadi sasa wangekuwa wanareport live. Waambie wafuatilie mambo yao TZ ni tamu mno.
Yaani Jana Serikali nimeipongeza sana, ilijua namna ya kuruka ule mtego. CHADEMA walikusanya watu kila kona kwenda kumpokea Lissu licha ya katazo la polisi. Wakajua polisi watazuia yale maandamano ili itokee vurugu wapate headlines na sympathy kama walivyozoea. Matokeo yake wameachwa wamecheza movie yao, walivyomaliza wakaenda kukojoa wakalala. Leo wameamka wanataka vyombo vya habari vyote viripoti upuuzi wakati tuna msiba wa kitaifa.
 
Kwani ujio wa Lissu una impact gani kwa taifa? kiasi kwamba wananchi wasipopata hiyo habari basi kuna shida kubwa itatokea katika maisha yao ya kila siku.
Kama hauna impact na hapa ungepita kimyakimya
 
Nimepitia kurasa za mbele za magazeti ya leo yote haya kuonyesha tukio kubwa la ujio wa TAL isipokuwa Mwananchi pekee.
Hii dalili za uoga, mkakati wa wasiojilikana, kuminywa kwa uhuru wa media au......?
Bila hio habari nani atanunua hayo magazeti like lililoandika hiyo habari ndio litauza uandike msiba wa Mkapa utegemee kuuza labda wa Lumumba ndio watanunua
 
Shida yako Gulwa unadhani magazeti yaliyopo nchini ni Mzalendo na Habari Leo pekee! Kuna magazeti mengine kibao. Kayasome ndo uje uandike tena.
Tutajie hayo mengine yaliyoipa umuhimu
 
Yaani Jana Serikali nimeipongeza sana, ilijua namna ya kuruka ule mtego. CHADEMA walikusanya watu kila kona kwenda kumpokea Lissu licha ya katazo la polisi. Wakajua polisi watazuia yale maandamano ili itokee vurugu wapate headlines na sympathy kama walivyozoea. Matokeo yake wameachwa wamecheza movie yao, walivyomaliza wakaenda kukojoa wakalala. Leo wameamka wanataka vyombo vya habari vyote viripoti upuuzi wakati tuna msiba wa kitaifa.
Waache wafu wazike wafu wao
 
Back
Top Bottom