Magonjwa ya zinaa(STDs) ni pigo la Mungu kwa wazinzi na waasherati?

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Ukisoma historia ya Waisraeli, utaona jinsi Mungu alivyotoa mapigo kumi kwa Wamisri waliokataa kumtii. Mojawapo ya mapigo hayo ni majipu mabaya yaliyowakumba watu wa Misri (Kutoka 9:8–11). Hili lilikuwa onyo kwamba Mungu anaweza hata kutumia magonjwa kama fimbo ya kuwaadhibu wale wanaokataa kuishi katika njia zake.

Leo hii, tunashuhudia jinsi magonjwa ya zinaa (STDs) yanavyoenea kwa kasi. Wanasayansi wamejitahidi sana kutengeneza dawa, chanjo, na mbinu za kinga, lakini kila kukicha magonjwa mapya yanaibuka, kama vile UKIMWI (AIDS) ambao mpaka sasa bado hauna tiba kamili. Hata yale magonjwa ya zinaa yaliyokuwa yakidhibitiwa kwa urahisi zamani, sasa yamekuwa sugu dhidi ya dawa nyingi. Je, hii inaweza kuwa ishara kwamba wanadamu wanapopuuza sheria za Mungu, wanajitafutia mapigo yasiyo na suluhisho?

Mungu hapendezwi na uzinzi na uasherati, ndio sababu amesema wazi katika Maandiko kwamba wanaofanya dhambi hizo watakuwa miongoni mwa watu watakaotupwa motoni milele. Biblia inaonya sana tuikimbie zinaa na kujiepusha na uasherati. Mtu asiyeweza kujizuia, anatakiwa aoe au kuolewa badala ya kufanya uzinzi.

Maandiko yanatuambia tena kwamba "...yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye." Kwa mantiki hiyo, naamini hata magonjwa ya zinaa ni kiboko cha kuwarudi wanaopenda uzinzi na uasherati. Na wakiendelea kukaidi, ziwa la moto wa milele linawangojea.

Njia pekee ya kuepuka mapigo hayo ya sasa na yale ya milele, ni kutubu dhambi, kuacha uzinzi na uasherati, na kuishi maisha safi ya kumpendeza Mungu.

Inawezekana unatamani kuacha uzinzi lakini kila ukijaribu unashindwa. Yesu anakuita leo akupumzishe mzigo huo, unaokusumbua na kukulemea (Mathayo 11:28).
 
"Ikimbieni zinaa. Dhambi nyingine zote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe." (1 Wakorintho 6:18)

"Usizini." (Kutoka 20:14)

"Mungu anataka nyinyi muwe watakatifu na mjiepushe kabisa na maisha ya zinaa." (1 Wathesalonike 4:3)
 
Kijana, kama huyajui magonjwa yanayoenezwa kwa zinaa, nakutajia hapa ujihadhari usije ukatumbukia katika uzinzi/uasherati ukaambukizwa.

VVU/HIV – Ni virusi vinavyoshambulia kinga ya mwili. Mtu akiambukizwa anaweza kuishi muda mrefu bila dalili, lakini taratibu kinga hupungua. Hatimaye, hali hiyo humsababishia UKIMWI (AIDS) ambapo mwili hushindwa kupambana na magonjwa mengine.

Kisonono (Gonorrhea) – Husababisha usaha sehemu za siri, maumivu wakati wa kwenda haja ndogo, na mara nyingine maumivu tumboni kwa wanawake. Hali hiyo inaweza kusababisha ugumba/utasa.

Kaswende (Syphilis) – Huanza na kidonda kisichouma sehemu za siri au mdomoni, baadaye vipele mwilini. Ikiendelea, huweza kuathiri moyo, mishipa ya fahamu na hata ubongo.

Chlamydia – Mara nyingi haina dalili mwanzoni, lakini huleta maumivu wakati wa kujisaidia au kuongezeka kwa uchafu sehemu za siri. Kwa wanawake, inaweza kuharibu mirija ya uzazi na kusababisha ugumba/utasa.

Trichomoniasis – Husababishwa na vimelea vidogo (protozoa). Dalili zake ni harufu mbaya, uchafu wa rangi ya njano-kijani, kuwashwa, na maumivu wakati wa "kuchimba dawa."

Herpes Simplex Virus (HSV) – Husababisha vidonda vya malengelenge vinavyouma sehemu za siri au mdomoni. Ni ugonjwa wa kudumu kwa kuwa virusi hubaki mwilini na kujirudia mara kwa mara.

Human Papillomavirus (HPV) – Husababisha vipele au vinyama nyama (warts) sehemu za siri na pia huongeza hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.

Hepatitis B – Ni virusi vinavyoshambulia ini, vinaweza kuenezwa kwa ngono na njia nyingine. Vikikomaa, husababisha saratani ya ini na ini kushindwa kufanya kazi.

Duuh, mapigo hayo ni hatari sana. Ee Mungu kiokoe kizazi hiki cha uzinzi
 
Vipi kuhusu madaktari na wauguzi walioambukizwa Hepatitis B katika mazingira ya kazi? Je, nao ni wazinzi?
Je, waliopata maambukizi ya VVU kutoka kwa mama nao ni wazinzi?
Ukimuuliza Netanyahu kwanini mabomu yanayopigwa na ndege za IDF yanaua raia Gaza? Atakujibu ndege zake zinapopiga mabomu huwa zinawalenga askari wa Hamas, lakini bahati mbaya mabomu mengine yanawaangukia raia wasio na hatia.

Watu wakiacha uzinzi, madaktari hawawezi kupatwa na Hepatitis B. Watu wakiacha uzinzi, watoto hawawezi kupata maambukizi ya VVU kutoka kwa mama zao.
 
Vipi kuhusu wazinzi ambao hawana hayo magonjwa, je hiyo adhabu ya Mungu inabagua?
Na kama STDs ni adhabu ya Mungu kutokana na uzinzi je, kwa nini wanao tumia Condom na PREP hawapati hayo magonjwa? Je, Mungu anazuiliwa na condom kutoa adhabu?
 
Daah, wewe ni Enthusiastic hasa!
OK. Ni vizuri kufahamu kwamba, sio kila dhambi huadhibiwa saa hiyohiyo au kwa njia ileile ya mwili. Kama ulivyosema, ni kweli kuna wazinzi wasioambukizwa na wanaonekana kuwa na afya njema, lakini Biblia inasema:
"Dhambi za watu wengine ni dhahiri nazo zinawatangulia kwenda hukumuni; na dhambi za watu wengine zinawafuata nyuma yao." (1 Timotheo 5:24)

Hiyo ina maana kwamba Mungu ana njia na wakati wake wa kushughulika na kila dhambi – wengine hupata mapigo mapema na wengine baadaye, na wengine hadi siku ya hukumu. Hata Waswahili wanasema: "Za mwizi ni arobaini", yaani mwizi anaweza akaiba kwa siku 39 asikamatwe, akajiona salama tu lakini akiiba siku ya 40, anajikuta anachomwa moto ndani ya tairi😳 na wananchi waliojichukulia sheria mikononi.

Kuhusu condom na PrEP, hizi ni mbinu za kibinadamu za kupunguza maambukizi tu. Lakini je, zinazuia hukumu ya Mungu? Jibu ni hapana. Kwa sababu hukumu ya Mungu sio lazima ionekane katika mwili. Inaweza kuonekana pia katika nafsi na roho. Kuna member mmoja humu ali-comment kwenye uzi wangu fulani kwamba amejisikia hatia baada ya kuzini. Kujisikia hatia ni pigo pia. Unaishi bila amani.

Kwa hiyo hata kama mtu anaweza kujilinda na kondomu asipate magonjwa ya zinaa, bado hawezi kujilinda na hukumu ya Mungu siku ile ya mwisho juu ya watendao dhambi ya uasherati.
Ufunuo 21:8
"Bali waoga, na wasioamini, na wenye machukizo, na wauaji, na waasherati, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwaka moto na kiberiti; hiyo ndiyo mauti ya pili."
 
Ukisoma historia ya Waisraeli, utaona jinsi Mungu alivyotoa mapigo kumi kwa Wamisri waliokataa kumtii. Mojawapo ya mapigo hayo ni majipu mabaya yaliyowakumba watu wa Misri (Kutoka 9:8–11). Hili lilikuwa onyo kwamba Mungu anaweza hata kutumia magonjwa kama fimbo ya kuwaadhibu wale wanaokataa kuishi katika njia zake.

Leo hii, tunashuhudia jinsi magonjwa ya zinaa (STDs) yanavyoenea kwa kasi. Wanasayansi wamejitahidi sana kutengeneza dawa, chanjo, na mbinu za kinga, lakini kila kukicha magonjwa mapya yanaibuka, kama vile UKIMWI (AIDS) ambao mpaka sasa bado hauna tiba kamili. Hata yale magonjwa ya zinaa yaliyokuwa yakidhibitiwa kwa urahisi zamani, sasa yamekuwa sugu dhidi ya dawa nyingi. Je, hii inaweza kuwa ishara kwamba wanadamu wanapopuuza sheria za Mungu, wanajitafutia mapigo yasiyo na suluhisho?

Mungu hapendezwi na uzinzi na uasherati, ndio sababu amesema wazi katika Maandiko kwamba wanaofanya dhambi hizo watakuwa miongoni mwa watu watakaotupwa motoni milele. Biblia inaonya sana tuikimbie zinaa na kujiepusha na uasherati. Mtu asiyeweza kujizuia, anatakiwa aoe au kuolewa badala ya kufanya uzinzi.

Maandiko yanatuambia tena kwamba "...yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye." Kwa mantiki hiyo, naamini hata magonjwa ya zinaa ni kiboko cha kuwarudi wanaopenda uzinzi na uasherati. Na wakiendelea kukaidi, ziwa la moto wa milele linawangojea.

Njia pekee ya kuepuka mapigo hayo ya sasa na yale ya milele, ni kutubu dhambi, kuacha uzinzi na uasherati, na kuishi maisha safi ya kumpendeza Mungu.

Inawezekana unatamani kuacha uzinzi lakini kila ukijaribu unashindwa. Yesu anakuita leo akupumzishe mzigo huo, unaokusumbua na kukulemea (Mathayo 11:28).
Eye opener
 
Ukimuuliza Netanyahu kwanini mabomu yanayopigwa na ndege za IDF yanaua raia Gaza? Atakujibu ndege zake zinapopiga mabomu huwa zinawalenga askari wa Hamas, lakini bahati mbaya mabomu mengine yanawaangukia raia wasio na hatia.

Watu wakiacha uzinzi, madaktari hawawezi kupatwa na Hepatitis B. Watu wakiacha uzinzi, watoto hawawezi kupata maambukizi ya VVU kutoka kwa mama zao.
Netanyahu ni genocidal dictator na mhalifu wa vita.
 
Vipi watoto wanaobakwa na kuambukizwa hayo magonjwa??
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Suleiman alikua mzizi na hakupata hata gono acha kutupanga buana!
20250720_180322.jpg
 
Nashukuru Mnoo Kwa Huduma Za Kiroho Unazozimwaga Kupitia Platform Hii Ya JAMII AFRICA,,Zinanibariki Si Kidogo...Baba Muumba Aendelee Kukujalia Afya ya Mifupa,,Damu Na Nyama... ​
Amen. Sifa kwa Yesu
 
Netanyahu ni genocidal dictator na mhalifu wa vita.
Huyo bado anaongozwa na sheria za Musa za jino kwa jino, hivyo usimshangae. Yeye anaona anayoyafanya ni halali kabisa!
 
Kijana, kama huyajui magonjwa yanayoenezwa kwa zinaa, nakutajia hapa ujihadhari usije ukatumbukia katika uzinzi/uasherati ukaambukizwa.

VVU/HIV – Ni virusi vinavyoshambulia kinga ya mwili. Mtu akiambukizwa anaweza kuishi muda mrefu bila dalili, lakini taratibu kinga hupungua. Hatimaye, hali hiyo humsababishia UKIMWI (AIDS) ambapo mwili hushindwa kupambana na magonjwa mengine.

Kisonono (Gonorrhea) – Husababisha usaha sehemu za siri, maumivu wakati wa kwenda haja ndogo, na mara nyingine maumivu tumboni kwa wanawake. Hali hiyo inaweza kusababisha ugumba/utasa.

Kaswende (Syphilis) – Huanza na kidonda kisichouma sehemu za siri au mdomoni, baadaye vipele mwilini. Ikiendelea, huweza kuathiri moyo, mishipa ya fahamu na hata ubongo.

Chlamydia – Mara nyingi haina dalili mwanzoni, lakini huleta maumivu wakati wa kujisaidia au kuongezeka kwa uchafu sehemu za siri. Kwa wanawake, inaweza kuharibu mirija ya uzazi na kusababisha ugumba/utasa.

Trichomoniasis – Husababishwa na vimelea vidogo (protozoa). Dalili zake ni harufu mbaya, uchafu wa rangi ya njano-kijani, kuwashwa, na maumivu wakati wa "kuchimba dawa."

Herpes Simplex Virus (HSV) – Husababisha vidonda vya malengelenge vinavyouma sehemu za siri au mdomoni. Ni ugonjwa wa kudumu kwa kuwa virusi hubaki mwilini na kujirudia mara kwa mara.

Human Papillomavirus (HPV) – Husababisha vipele au vinyama nyama (warts) sehemu za siri na pia huongeza hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.

Hepatitis B – Ni virusi vinavyoshambulia ini, vinaweza kuenezwa kwa ngono na njia nyingine. Vikikomaa, husababisha saratani ya ini na ini kushindwa kufanya kazi.

Duuh, mapigo hayo ni hatari sana. Ee Mungu kiokoe kizazi hiki cha uzinzi
Ongeza hapo H. Pylory
 
Back
Top Bottom