Magonjwa ya zinaa(STDs) ni pigo la Mungu kwa wazinzi na waasherati?

Magonjwa ya zinaa(STDs) ni pigo la Mungu kwa wazinzi na waasherati?

Unavyoandika utadhani ngono inafanywa na wazinzi pekee...
 
UTI na pid ni magonjwa ya zinaa au sio zinaa?
UTI sio ugonjwa wa zinaa, bali ni maambukizi ya njia ya mkojo yanayosababishwa na bakteria. PID nayo pia sio ugonjwa wa zinaa moja kwa moja, mara nyingi hutokana na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa kama kisonono na chlamydia
 
Ongeza hapo H. Pylory
Helicobacter pylori (H. pylori) ni bakteria wanaoishi tumboni na kusababisha vidonda vya tumbo na gastritis. Hao hawapo kwenye kundi la STDs kwa sababu wanaenezwa kwa kula chakula au kunywa maji machafu
 
PID nayo pia sio ugonjwa wa zinaa moja kwa moja, mara nyingi hutokana na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa kama kisonono na chlamydia
Acha uongo wewe kwenye masuala ya kitaalamu unaleta ulokole. Mara PID sio ugonjwa wa zinaa. Halaf tena unasema unatokana na kutotibiwa vizuri kwa kisonono au chlamydia ambayo ni magonjwa ya zinaa. Are you insane?
 
Acha uongo wewe kwenye masuala ya kitaalamu unaleta ulokole. Mara PID sio ugonjwa wa zinaa. Halaf tena unasema unatokana na kutotibiwa vizuri kwa kisonono au chlamydia ambayo ni magonjwa ya zinaa. Are you insane?
PID ni matokeo ya kuambukizwa kisonono au chlamydia. In other words, kisonono kinazaa PID.
 
PID ni matokeo ya kuambukizwa kisonono au chlamydia. In other words, kisonono kinazaa PID.
Sio kweli hiyo ni sehemu tu ya sababu na sio the only cause.

PID (Pelvic Inflammatory Disease) ni ugonjwa wa maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke, kama vile mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi (fallopian tubes), na ovari. Husababishwa na bakteria, hasa kupitia njia ya ngono.

Visababishi vya PID:

1. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs) – haswa:
- Chlamydia trachomatis
- Neisseria gonorrhoeae (gonorrhea)

2. Kuenea kwa bakteria wa kawaida ukeni hadi kwenye viungo vya ndani vya uzazi.

3. Sababu zingine zinazochangia:
- Kuwa na wapenzi wengi wa ngono.
- Kutotumia kinga (kondomu).
- Historia ya PID.
- Kuingiza vifaa kama IUD bila usafi wa kutosha.
- Douching (kusafisha uke kwa maji yenye kemikali) – huweza kuvuruga bakteria wa kawaida.

Dalili kuu:
  • Maumivu ya chini ya tumbo
  • Homa
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni
  • Maumivu au kuchoma wakati wa kukojoa

Ikiachwa bila matibabu, PID inaweza kusababisha ugumba, mimba ya nje ya kizazi, au maumivu ya muda mrefu.

Unahitaji maelezo ya matibabu pia?
 
Vipi kusukari,stroke,pressure,homa ya ini na figo.
 
Pole sana Wakilli
Naona uzi huu umekuwa mchungu kwako kama Metronidazole. Jitahidi umeze tu, ili upone Wakilli wangu
 
Visababishi vya PID:

1. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs) – haswa:
  • Chlamydia trachomatis
  • Neisseria gonorrhoeae (gonorrhea)
Sasa mbona hiyo AI yako imeniunga tu mkono?! Au hujaelewa ilivyokwambia? Imesema: visababishi vya PID ni maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
 
Back
Top Bottom