Ukimuuliza Netanyahu kwanini mabomu yanayopigwa na ndege za IDF yanaua raia Gaza? Atakujibu ndege zake zinapopiga mabomu huwa zinawalenga askari wa Hamas, lakini bahati mbaya mabomu mengine yanawaangukia raia wasio na hatia.Vipi kuhusu madaktari na wauguzi walioambukizwa Hepatitis B katika mazingira ya kazi? Je, nao ni wazinzi?
Je, waliopata maambukizi ya VVU kutoka kwa mama nao ni wazinzi?
Vipi kuhusu wazinzi ambao hawana hayo magonjwa, je hiyo adhabu ya Mungu inabagua?Ukimuuliza Netanyahu kwanini mabomu yanayopigwa na ndege za IDF yanaua raia Gaza? Atakujibu ndege zake zinapopiga mabomu huwa zinawalenga askari wa Hamas, lakini bahati mbaya mabomu mengine yanawaangukia raia wasio na hatia.
Watu wakiacha uzinzi, madaktari hawawezi kupatwa na Hepatitis B. Watu wakiacha uzinzi, watoto hawawezi kupata maambukizi ya VVU kutoka kwa mama zao.
Daah, wewe ni Enthusiastic hasa!Vipi kuhusu wazinzi ambao hawana hayo magonjwa, je hiyo adhabu ya Mungu inabagua?
Na kama STDs ni adhabu ya Mungu kutokana na uzinzi je, kwa nini wanao tumia Condom na PREP hawapati hayo magonjwa? Je, Mungu anazuiliwa na condom kutoa adhabu?
Eye openerUkisoma historia ya Waisraeli, utaona jinsi Mungu alivyotoa mapigo kumi kwa Wamisri waliokataa kumtii. Mojawapo ya mapigo hayo ni majipu mabaya yaliyowakumba watu wa Misri (Kutoka 9:8–11). Hili lilikuwa onyo kwamba Mungu anaweza hata kutumia magonjwa kama fimbo ya kuwaadhibu wale wanaokataa kuishi katika njia zake.
Leo hii, tunashuhudia jinsi magonjwa ya zinaa (STDs) yanavyoenea kwa kasi. Wanasayansi wamejitahidi sana kutengeneza dawa, chanjo, na mbinu za kinga, lakini kila kukicha magonjwa mapya yanaibuka, kama vile UKIMWI (AIDS) ambao mpaka sasa bado hauna tiba kamili. Hata yale magonjwa ya zinaa yaliyokuwa yakidhibitiwa kwa urahisi zamani, sasa yamekuwa sugu dhidi ya dawa nyingi. Je, hii inaweza kuwa ishara kwamba wanadamu wanapopuuza sheria za Mungu, wanajitafutia mapigo yasiyo na suluhisho?
Mungu hapendezwi na uzinzi na uasherati, ndio sababu amesema wazi katika Maandiko kwamba wanaofanya dhambi hizo watakuwa miongoni mwa watu watakaotupwa motoni milele. Biblia inaonya sana tuikimbie zinaa na kujiepusha na uasherati. Mtu asiyeweza kujizuia, anatakiwa aoe au kuolewa badala ya kufanya uzinzi.
Maandiko yanatuambia tena kwamba "...yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye." Kwa mantiki hiyo, naamini hata magonjwa ya zinaa ni kiboko cha kuwarudi wanaopenda uzinzi na uasherati. Na wakiendelea kukaidi, ziwa la moto wa milele linawangojea.
Njia pekee ya kuepuka mapigo hayo ya sasa na yale ya milele, ni kutubu dhambi, kuacha uzinzi na uasherati, na kuishi maisha safi ya kumpendeza Mungu.
Inawezekana unatamani kuacha uzinzi lakini kila ukijaribu unashindwa. Yesu anakuita leo akupumzishe mzigo huo, unaokusumbua na kukulemea (Mathayo 11:28).
Netanyahu ni genocidal dictator na mhalifu wa vita.Ukimuuliza Netanyahu kwanini mabomu yanayopigwa na ndege za IDF yanaua raia Gaza? Atakujibu ndege zake zinapopiga mabomu huwa zinawalenga askari wa Hamas, lakini bahati mbaya mabomu mengine yanawaangukia raia wasio na hatia.
Watu wakiacha uzinzi, madaktari hawawezi kupatwa na Hepatitis B. Watu wakiacha uzinzi, watoto hawawezi kupata maambukizi ya VVU kutoka kwa mama zao.
Ongeza hapo H. PyloryKijana, kama huyajui magonjwa yanayoenezwa kwa zinaa, nakutajia hapa ujihadhari usije ukatumbukia katika uzinzi/uasherati ukaambukizwa.
VVU/HIV – Ni virusi vinavyoshambulia kinga ya mwili. Mtu akiambukizwa anaweza kuishi muda mrefu bila dalili, lakini taratibu kinga hupungua. Hatimaye, hali hiyo humsababishia UKIMWI (AIDS) ambapo mwili hushindwa kupambana na magonjwa mengine.
Kisonono (Gonorrhea) – Husababisha usaha sehemu za siri, maumivu wakati wa kwenda haja ndogo, na mara nyingine maumivu tumboni kwa wanawake. Hali hiyo inaweza kusababisha ugumba/utasa.
Kaswende (Syphilis) – Huanza na kidonda kisichouma sehemu za siri au mdomoni, baadaye vipele mwilini. Ikiendelea, huweza kuathiri moyo, mishipa ya fahamu na hata ubongo.
Chlamydia – Mara nyingi haina dalili mwanzoni, lakini huleta maumivu wakati wa kujisaidia au kuongezeka kwa uchafu sehemu za siri. Kwa wanawake, inaweza kuharibu mirija ya uzazi na kusababisha ugumba/utasa.
Trichomoniasis – Husababishwa na vimelea vidogo (protozoa). Dalili zake ni harufu mbaya, uchafu wa rangi ya njano-kijani, kuwashwa, na maumivu wakati wa "kuchimba dawa."
Herpes Simplex Virus (HSV) – Husababisha vidonda vya malengelenge vinavyouma sehemu za siri au mdomoni. Ni ugonjwa wa kudumu kwa kuwa virusi hubaki mwilini na kujirudia mara kwa mara.
Human Papillomavirus (HPV) – Husababisha vipele au vinyama nyama (warts) sehemu za siri na pia huongeza hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.
Hepatitis B – Ni virusi vinavyoshambulia ini, vinaweza kuenezwa kwa ngono na njia nyingine. Vikikomaa, husababisha saratani ya ini na ini kushindwa kufanya kazi.
Duuh, mapigo hayo ni hatari sana. Ee Mungu kiokoe kizazi hiki cha uzinzi