Magori: Selemani Mwalimu mchezaji gani yule wa kumlipia Tsh. Bil. 1 kwa mkopo?

Magori: Selemani Mwalimu mchezaji gani yule wa kumlipia Tsh. Bil. 1 kwa mkopo?

Suala kubwa hapa watu wengi hawalioni au hawataki kuliona kwa sababu zao wanazojua wao wenyewe. Suala hapa ni kusema uongo hadharani na dunia nzima ikitazama kupitia AZAM TV.
  • Sawa Simba haiwezi kulipa bilioni kama ni kweli Mwalimu alithaminishwa hivyo hata mimi nawaunga mkono Simba kukataa. Sasa kwa nini waliitangazia dunia uwongo kuwa wamemsajili wakati hawajamsajili?
  • Vipi kama wanaweza kudanganya hadharani hivi na dunia yote inaona vipi wakiwa mafichoni wameshadanganya mangapi?
  • Je viongozi wakitangaza jambo lingine lolote wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba na watanzania kwa ujumla wawaamini au wasiwaamini?
  • Sasa hivi itabaki kuwa ni kashifa kubwa kwa uongozi wa Simba kuwahi kutokea hivi karibuni mpaka pale itakapothibitika bila shaka yoyote kuwa huo ni ukurupukaji wa Ahmed Ally na kitengo cha habari. Na bila kuwajibishwa kwa wale wote waliohusika ikabaki hivi basi hapo viongozi wote ndio wahusika wa aibu yote iliyotokea siku ya Simba day.
 
mchezaji wa kawaida. Faida yake ni mzawa tu, hajazi nafasi za usajili.

Kama kutotoa Bilioni kwaajili ya mkopo ni uzembe wa viongozi, basi na mimi nautamani huo uzembe.

Namuelewa Hersi na Yanga yake kwanini amepush hili deal kwa nguvu. Muda utaongea.
Naku follow kabisa , ili nipate notification zako , siku iwe rahis kuku tag umbumbu wa viongozi wa simba
 
Hata milioni 300 sio ya kutoa kwa Wydad, mshahara 25 to 30M kwa Selemani sawa. Hiyo biashara Wydad wamenufaika parefu. Simba inaenda inavyotakiwa. Hawa wakulungwa wa Yanga janja janja nyingi. Inadhihirika zaidi ikija katika international games.

Kesho labda refa awaokoe😀😀.Doumbia anaanza kuheshimika kesho.
 
Niliwaambia Simba haina viongozi. Sele hata 200m hastahili ila huwezi kusema hiyo hadharani
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Crescentius Magori, ametoa kauli yake baada ya mchezaji Selemani Mwalimu kutangazwa Yanga, akieleza kuwa jambo hilo halina uzito wowote wa kuilaza au kuishtua Simba.

Soma kuhusu Sapraiziiii: Yanga yamsajili Selemani Mwalimu siku mbili baada ya kunukuliwa akisema ataichezea Simba Msimu wa 2026/27

Akizungumza na waandishi wa habari, Magori amepuuza taarifa za kuwepo kwa Taharuki na kuhoji kwa mshangao jinsi gani mchezaji aliyenunuliwa kwa takriban bilioni moja kisha kuondoka kwa mkopo aweze kuilaza au kuipa presha Simba SC, akisisitiza kuwa klabu hiyo haiwezi kulipa vitu vya hewani.

Yule mzee ubongo ushachoka, bado anaishi kizaman🤣
 
G.S.M na YANGA kuna mchezo wanacheza sana w M.L
Muda ndio mwalimu mzr.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Halafu wanatakiwa kujua sisi tunaona miyeyusho unatangaza mchezaji umemsajili halafu kesho anaenda kwingine ni dharau sana.
 
Watakatisha fedha ndio wanazo pesa za kuchezea ngoja mama yao aondoke tutaelewana tu, yale mabakuli yao wasijisahau wakayatupa.

Wasije na visingizio vyao vya wamefilisika.
Thibitisha unachoongea.

Ukiitwa mahakamani unaweza tetea hoja yako
 
Niliwaambia Simba haina viongozi. Sele hata 200m hastahili ila huwezi kusema hiyo hadharani
Nakubaliana na wewe. Nafikiri Magori alikuwa kwenye panic mode na ni kitu ambacho sio sahihi kwa Kiongozi kama yeye.
 
Thamani yake kubwa kwenye kuwavuruga wapinzani.
Hii inaenda kuwagawa na kufubaza mauzo ya jezi na mahudhurio ya wanasimba kwenye kurasa za mitandao za Simba na viwanjani
Inaweza kuwarudisha nyuma wadhamini klabu ikapoteza mapato tarajiwa ....
Fikiria mbali.
Yes, ila Simba ikishinda shilingi inaweza ikageuka.
 
Kwanini walimtangaza Simba day

Taarifa ya mwanzo mpaka akarudi wydad ilikuwa ni malipo ya million 125 tu
Leo magori anasema ni billion Moja, kwanini tumuamini tena

Takataka
 
Simba inatakiwa kuchagua kukaa kimya na kubeba makombe sio kutoa visingizio,maelezo pia iache siaza za kizaman kwenye mpira wa kisasa unaotaka pesa au elimu
 
Bora angekaa kimya tu.
Angekaa tu kimya.

Hapo Simba ni wazi hakuna umoja baina ya viongozi wao Kwa wao, Huenda Kuna shida kubwa kwenye strategies zao za USAJILI.

Magori ana jazba kubwa Huenda alikaa na Sulee Teacher lkn akageukwa na upande wa Mwalimu na timu yake kiarabu.
 
Sele hakua na impact kihivyo, na hata alipokua kikosini alikua benchi, na hata angekuwepo bado angeanzia benchi, sasa ana thamani ipi ya kupewa 1B tena kwa mkopo?
Hao waliomchukua wana pesa za kuchezea na wanajua Pa kuzitoa..
Utakatishaji ktk ubora wao, na sahivi yuko uongozini basi atabaluza pesa chafu hadi basi.
Duuh.
 
Back
Top Bottom