Magori: Selemani Mwalimu mchezaji gani yule wa kumlipia Tsh. Bil. 1 kwa mkopo?

Magori: Selemani Mwalimu mchezaji gani yule wa kumlipia Tsh. Bil. 1 kwa mkopo?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Crescentius Magori, ametoa kauli yake baada ya mchezaji Selemani Mwalimu kutangazwa Yanga, akieleza kuwa jambo hilo halina uzito wowote wa kuilaza au kuishtua Simba.

Soma kuhusu Sapraiziiii: Yanga yamsajili Selemani Mwalimu siku mbili baada ya kunukuliwa akisema ataichezea Simba Msimu wa 2026/27

Akizungumza na waandishi wa habari, Magori amepuuza taarifa za kuwepo kwa Taharuki na kuhoji kwa mshangao jinsi gani mchezaji aliyenunuliwa kwa takriban bilioni moja kisha kuondoka kwa mkopo aweze kuilaza au kuipa presha Simba SC, akisisitiza kuwa klabu hiyo haiwezi kulipa vitu vya hewani.

 
Kasema ukweli.
Screenshot_2026-08-11_130056.jpg

 
Tunaweza kulaumu kushindwa kukamilisha deal kwa wakati. Na kuuma kuna kuja kwasababu tumeshazoea kuzodoana kati ya Simba na Yanga.

Lakini hebu tusemezane kwa upole, je Sele Mwalimu anathamani ya Bilioni 1 kwa mkopo?!

Last season yote alikuwa anatokea benchi na hata sisi mashabiki hatukuwahi kumwamini Sele Mwalimu.
 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Crescentius Magori, ametoa kauli yake baada ya mchezaji Selemani Mwalimu kutangazwa Yanga, akieleza kuwa jambo hilo halina uzito wowote wa kuilaza au kuishtua Simba.

Akizungumza na waandishi wa habari, Magori amepuuza taarifa za kuwepo kwa Taharuki na kuhoji kwa mshangao jinsi gani mchezaji aliyenunuliwa kwa takriban bilioni moja kisha kuondoka kwa mkopo aweze kuilaza au kuipa presha Simba SC, akisisitiza kuwa klabu hiyo haiwezi kulipa vitu vya hewani.

Kiukweli hata mimi sijaumia. Labda kwasababu ya kutambiana kati ya Simba na Yanga.
 
Kwanini sasa walimtangaza kwenye siku ya tamasha lao?
Waliamini katika professionalism na makubaliano ya mdomo. Of course timu nyingi huwa zinafanya hivyo.

Tofauti hapo ni Yanga kuingilia deal ili kuvuruga mchakato mzima na kuzima kelele ambazo zishaanza kutokea kwao baada ya kupoteza mechi huku wakifunikwa vibaya sana na Aigles Du Congo.
 
Back
Top Bottom