Mkuu
Mchambuzi,
Je,viashiria vya maendeleo kiuchumi vikoje Kwa sasa walau tangu Bajeti ya 2016/2017 ianze kazi?
Zipo namna nyingi kujadili swali lako hili muhimu. Ningependa kuchokoza zaidi mada kuliko kuja na majibu ya moja kwa moja ili kwa pamoja tuweze kusaidiana kupata majibu husika. Naomba nilitazame suala hili kwa jicho la kisekta ingawa kama tutakavyoona, many issues are “cross cutting”, hayasimami peke yake. Na suala hili la serikali kutozingatia cross cutting issues and provide funds accordingly ni moja ya sababu kubwa kwanini kama taifa tumekwama kimaendeleo. Kwa kipindi kirefu sana, approach to economic development by the government has been more ‘atomistic’ than ‘holistic’. Kwa mfano unakuta mwaka mmoja wa fedha kipaumbele cha serikali kinakuwa ni Elimu, mwaka unaofuatia, Elimu inaachwa njiani huku ikiwa haijapata karibia nusu ya fedha zilizotengwa kwa ajili yake, na serikali kuhamia sekta nyingine kwa mfano Miundombinu nk. Nothing holistic.
Kama njia moja wapo ya kujadili swali lako, ningependa kulijadili katika muktadha wa Mtaji Watu (Human Capital). Katika hoja yangu ya msingi nilijadili kwamba Mtaji Watu (Human Capital) inajengwa na nguzo kuu mbili, zikisaidiwa na nyingine moja. Nguzo kuu hizo ni Kiwango cha AFYA za wananchi na Kiwango cha Elimu miongoni mwa wananchi, huku suala la LISHE (nutrition) nalo likiwa na mchango muhimu towards that end. Kwa maana hii, katika hali ya kawaida, serikali ilitakiwa kuweka vipaumbele vya muda mrefu sana katika sekta kuu tatu kama njia ya kumtafutia mtanzania maendeleo ya kweli. Sekta hizo ni:
1. Elimu
2. Afya
3. Lishe (kilimo)
Katika hoja yangu ya msingi nilijadili jinsi gani katika nyakati mbalimbali Umoja wa Africa (AU) ulikuja na maazimio ambayo yalizitaka nchi wanachama kuwekeza ipasavyo katika maeneo haya matatu. Maazimio hayo ni kama ifuatavyo:
1. Azimio la Dakar (Senegal), mwaka 2000 lililohusu ELIMU/Mtaji Watu/Human Capital. Kupitia azimio hili, viongozi wa AU walikubaliana kwamba ili kuboresha the aforementioned kwa uchumi na hali za maisha ya wananchi wao, kila serikali ilipaswa kuanza kutenga sio chini ya 20% ya jumla ya bajeti nzima kila mwaka kwa ajili ya sekta ya Elimu pekee.
2. Azimio la Abuja (Nigeria), mwaka 2001 lililohusu AFYA. Chini ya azimio hili, viongozi wa AU walikubaliana kwamba kila nchi ianze kutenga sio chini ya 15% ya jumla ya bajeti nzima kila mwana kwa ajili ya sekta ya Afya pekee.
3. Azimio la Maputo (Msumbiji), mwaka 2003 lililohusu KILIMO NA USALAMA WA CHAKULA. Chini ya azimio hili, viongozi wa AU walikubaliana kutenga sio chini ya 10% ya bajeti nzima kwa ajili ya sekta ya Kilimo Pekee.
Utekelezaji wetu katika hili umekuwa ni wa kusua sua katika kipindi chote kilichofuatia maazimo haya muhimu. Tukiangalia hata katika bajeti ya kwanza ya serikali mpya ya Rais Magufuli, deviation katika hilo ni ya kutisha. Kwa mfano:
*Sekta ya AFYA - Kati ya jumla ya bajeti ya TZS trilioni 29.5 kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, kiasi kilichotengwa kwa ajili ya sekta ya Afya ni TZS 845 Bilioni tu, sawa na 2.8% ya bajeti yote kwa kipindi hicho vis a vis lengo la AU la angalau 15%.
*Sekta ya ELIMU - Kati ya jumla ya bajeti ya TZS trilioni 29.5 kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, kiasi kilichotengwa kwa ajili ya sekta ya Elimu ni TZS 1.3 trilioni tu, sawa na 4.4% ya bajeti yote kwa kipindi hicho vis a vis lengo la AU la angalau 20%.
*Sekta ya KILIMO - Kati ya jumla ya bajeti ya TZS trilioni 29.5 kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, kiasi kilichotengwa kwa ajili ya sekta ya Kilimo ni takribani TZS Bilioni 280 tu, sawa na 1% ya bajeti yote kwa kipindi hicho vis a vis lengo la AU la angalau 10%.
Kiasi kilichotengwa kwa ajili ya sekta hizi muhimu tatu (in total) is less than 10% of the total budget. Swali linalofuata ni je, where did the 90% of the budget go? Kwa mfano jumla ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya Sekta za Afya, Elimu na Kilimo (in total) ni kidogo kuliko fedha zilizotengwa kwa ajili ya sekta moja tu ya Miundombinu.
Kama taifa, tumekuwa tunaimbishwa na serikali ile ile kwamba maadui watatu wa maendeleo ya nchi yetu ni:
-Umaskini
-Ujinga
-Maradhi.
Je tumefanya nini kubadilisha hali hii? Zaidi ya 70% ya watanzania wanategemea Kilimo kama shughuli ya kujipatia riziki zao, na hawa ndio sehemu kubwa ya wananchi maskini wa kipato. Kwa miaka zaidi ya 50 ya uhuru, hakuna lolote la maana ambalo limefanywa kubadilisha hali hiyo.
Sekta za Elimu na Afya, hivyo hivyo, hali ni mbaya sana. Kwanini Serikali haielewi kwamba siri ya mafanikio ipo katika kuziendeleza sekta hizi tatu ambazo ni muhimu kwa ujenzi wa Human Capital?
Tumekuwa tunaambiwa kwamba kasi ya uchumi inakuwa, na kwamba Tanzania ni moja ya nchi zinazofanya vizuri sana duniani. Kwa mfano tangia mwaka 2000, kasi ya kukua kwa uchumi kwa wastani ni karibia 7%. Tukumbuke kwamba mwaka 2000 wakati wadau wa maendeleo wanatuletea Mipango ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) walisema kwamba nchi ambazo zitafanikiwa kukuza uchumi kwa kasi ya 7% kwa miaka 15 mfululizo zitakuwa katika nafasi nzuri ya kupunguza umaskini kwa asilimia isiyopungua 50%. Huu ni mwaka wa kumi na sita tunaufunga, je tumeweza kupunguza umaskini kwa kiasi gani/asilimia ngapi? Nikitaja takwimu hapa kwa mfano X%,
Kobello atakuja mbio kuhoji uhalali wa namba husika kwa sababu nje ya kuvura vurga mada, hana kingine cha kufanya kulinda ujira wake Lumumba.
Kwa kifupi, kasi ya kukua kwa uchumi katika kipindi husika haijawahi kuishirikisha sehemu kubwa na muhimu ya nguvu kazi ya nchi, kwa mfano wakulima, machinga nk. Vile vile mafanikio ya kasi hii ya kukua kwa uchumi hayajashuka chini kwa wananchi walio wengi, na hakujawa na mkakati maalum wa kuhakikisha hilo linatokea. Badala yake kinachoendelea ni wananchi kujiingiza katika shughuli za kujiokotea okotea tu ili mradi maisha yaendelee.
Tukirudi katika suala la Human Capital na mchango wake katika maendeleo ya uchumi na watu wake, kwanini serikali haioni kwa mfano umuhimu wa “Afya” towards that end?
- Kwa kutekeleza azimio la Abuja (Afya), tungeweza kupata faida nyingi. Kwa mfano, afya bora hupelekea gains in labor productivity. Poor health inapunguza labor force kwa maana ya mortality rates, early retirements etc. Haya ndio yanayotokea nchini sasahivi.
- Kwa kutekeleza azimio la Dakar (Elimu), tungeweza pia kupata faida nyingi. Elimu kama ilivyo kwa afya improves labor productivity, pia inakuza entrepreneurship, innovation and technical advancement katika uchumi/taifa. Education plays a prominent role to secure economic and social progress of individuals esp improving their income/welfare (maisha bora).
- Kwa kutekeleza azimio la Maputo (Kilimo/lishe/usalama wa chakula), vile vile tungeweza kupata faida nyingi. Nutrition enhances life span ya wananchi; lakini pia in schools and production spheres inside the economy, good nutrition helps the brain to absorb knowledge.