Uchaguzi 2020 Magufuli 2020: Jogoo la Shamba linapowika mjini, wa mjini hujaribu kujitutumua!

Uchaguzi 2020 Magufuli 2020: Jogoo la Shamba linapowika mjini, wa mjini hujaribu kujitutumua!

Hakuna ninachokitetea kwa sababu siwezi kutetea suala ambalo halipo!

Kikao cha mpango kazi serikalini hakiwezi kuwa kama mkutano wa hadhara ndio maana kuna sheria na kanuni za utumishi wa umma ikiwa ni pamoja na kutunza siri za serikali!
Je, ni Kweli 96% ya Wagombea wa Upinzani kwenye SM unaamini hawakufaa, na 100% CCM walikuwa Correct?
 
Hakuna Uchaguzi Mkuu mwepesi kama ule wa 2020!

Hofu yangu ni kujikuta bungeni kuna wabunge wa upinzani wasiozidi 10 baada ya Uchaguzi Mkuu 2020!

Sidhani kama wabunge wa upinzani watazidi wawili au sanasana maximum ni watano au saba tu
 
Je, ni Kweli 96% ya Wagombea wa Upinzani kwenye SM unaamini hawakufaa, na 100% CCM walikuwa Correct?
Sina jibu halisi la swali lako kwa sababu sijui procedure zilivyokuwa katika kujaza fomu.

Inawezekana kuna baadhi ya wagombea wa upinzani hawakutendewa haki lakini pia tuelewe kuwa kulikuwa na nafasi ya hao wagombea kukata rufaa kama hawakutendewa haki.

Wakati wagombea hao wakijiandaa kukata rufaa, baadhi ya viongozi wa juu wa vyama vya upinzani wakatoa matamko kuwa vyama vyao vimejitoa katika uchaguzi.
 
Kitu ambacho ni dhahiri nawewe unakijua ni Kuwa CCM=Majeshi ya Nchi=Serikali=Judiciary.
Kuna njia ipi ya Kujitetea Wananchi wapenda haki na Demokrasia? Najua Nafsi yako inaelewa vizuri hata kabla ya Kueleza haya.
 
Praise and worship team katika ubora wenu, mkumbusheni tu kwamba Ghaddafi alikuwa akiwalipia hadi mahari vijana wa Libya, na mumkumbushe kwamba makaburu wameleta maendeleo makubwa South Africa lakini watu walitaka uhuru wao ndio jambo muhimu kuliko chochote.

Upuuzi kama huu peleka kwa wapuuzi wenzako.
 
Zero sum game.. Magufuli kuna vitu amefanya vizuri kuna vingine anachemka ukweli usemwe.

Issue ya ukabila na kuminya demokrasia huwezi kusema eti sio bora kwa taifa. Ajirekebishe.

Pia issue ya 'ego' ina m cost sana abadilike pia kwenye hilo..
 
Aache watu wawe huru kujieleza Kama kwa TRUMP......akiendelea hivi siku ukipatikana Uhuru wa kujieleza itakuwa patashika nguo kuchanika

Ungejua jinsi gani Trump anapambana na Fake News na tena anawaita "maadui wa wananchi" huwezi kuamini. Uhuru wa "kujieleza" siyo absolute... Ila naelewa unataka kumaanisha nini.
 
Matola,
Mtu anyeujibu upuuzi wakati anajua ni upuuzi sijui anaitwaje?

Mleta ''upuuzi'' na mjibu ''upuuzi'' anayejua ni ''upuuzi'' sijui nani bora kwa watu wenye fikra pana!

Nadhani ulichofanya ni sawa na kile Mark Twain aliwahi kusema, ''It's better to keep your mouth shut and appear stupid than open it and remove all doubt''.
 
Mbona nakuheshimu sana we jamaa!!!!Hebu ficha ujinga wako!!!!Unae msifu hajafanya chochote zaidi ya kuzua taharuki tu hapa nchini!!!Kwani ndege hazikuwepo?Viwanda havikuwepo?Hizo fly over sio mpango wake bali wa kidunia ndo mana imf wanatoa fedha wala wateja wa hzo fly over sio watz maskini bali wazungu wenyewe sio sisi wala hatuna faida nazo!!!Acha uzushi!Mwambie atuambie wapiga risasi na watekaji kawatoa wapi?Hayo mambo yapo rwanda sio tz!!!
 
Mwambieni asijaribu kuruhusu demokrasia ichukue mkondo wake, UJOGOO wake utakwenda na maji mara moja.
Demokrasia haitolewi kama zawadi na haiombwi. Kama unaamini hakuna demokrasia unatakiwa uidai kwa mbinde au kwa upinde. Jifunze sehemu nyingine duniani wamefanyaje. Mbona wakati wa JK watu walikuwa wanaidai demokrasia walipoona inaminywa..?Nini kimebadilika sasa?
 
Naona kumekucha tayari, mmeanza tena kutuhadaa baada ya kupewa bahasha za khaki, tuacheni tupumzike.
 
Akimurudisha Ben saa8 akiwafunga waliomuua Mawazo huko KATORO busanda akiwafutia mikesi viongozi wote wenye makesi yasiyo kichwa wala miguu akituambia kwenye Ndege kama Taifa tumewekeza sh ngapi. Mwisho akili mbere ya hazara kua amefanya zambi kodi zetu kuyanunua makina waitara na genge lote aluhusu siasa kama katiba yetu inavyoerekeza sasa hivi mimi navaa kijani.
 
Demokrasia haitolewi kama zawadi na haiombwi. Kama unaamini hakuna demokrasia unatakiwa uidai kwa mbinde au kwa upinde. Jifunze sehemu nyingine duniani wamefanyaje. Mbona wakati wa JK watu walikuwa wanaidai demokrasia walipoona inaminywa..?Nini kimebadilika sasa?
Mkuu, wewe ndiye Profesa Palamagamba nini? Umesahau kabisa kilichowapata akina Ben Saanane, Azory Gwanda, Tundu Lissu na wengineo? Utawala huu una tofauti gani na ule utawala wa MR AMIN kule Uganda? Una tofauti gani na ule utawala wa Omar al-Bashir?
Mwisho wa utawala huu wa KI-IMLA ni lazima utakuwepo tu, sio lazima iwe sasa Mkuu. Hilo halina mjadala
 
Naunga mkono hoja , hakuna binadamu asiye na kasoro. Lakini ukweli ni kuwa kasoro za magufuli ni chache, na utekelezaji wake ni wa hali ya juu kabisa.

Hii miradi anayoitekeleza ikikamilika, basi tutaona dunia itakavyo mnyenyekea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom