Elections 2015 Magufuli akutana na nguvu ya Umma Mbeya, azomewa, aambiwa wanamtaka Lowassa

Elections 2015 Magufuli akutana na nguvu ya Umma Mbeya, azomewa, aambiwa wanamtaka Lowassa

Mtarajiwa Magufuli akiona vipi awaachie ccm yao maana wanamchomekea baba wawa mpaka anapiga pushapu kunusuru ccm bado wanasisiemu wanamzunguka ku muharibia

CCM wanamtwika Magufuli mzigo asiouweza
 
Hiyo siyo nguvu ya umma ila ni uhuni.

Uhuni mtu yeyote akiamua anaweza kuufaya, lakini matokeo yake ni kuvujika kwa amani.

Kama wao wameshaamua kuwa wanamtaka Lowassa nini kinawapeleka kwenye mkutano wa Magufuli?

Inaonekana kabisa kuwa kuna kundi lililojiandaa kufanya fujo na walishaandaa camera wapige hii picha ya video.

Ukawa badala ya kuchekelea vitu kama hivi inabidi mvikemee kwa sabau watanzania hawapendi vurugu, hawatamchagua mtu anayeandaa vikundi vya vurugu.

Atoroke aje hakuna namna nyingine.
 
Bavicha bana sasa hapo nguvu ya ipo wapi hao wahuni wachache wanaopiga kelele?

Wapiga kura wametulia majumbani hawana fujo.

Endeleeni kujifariji mtakimbia humu baada ya uchaguzi.

Cha msingi hapa ni kwamba ujumbe kaupata kuwa ni kweli wananchi wanahitaji mabadiliko lakini mabadiliko yenyewe yataletwa na Lowassa kupitia UKAWA na siyo kama anavyosema Magufuli mwenyewe kuwa ataleta mabadiliko wakati yuko ndani ya tenga la samaki walioza.
 
Mkuu nakushauri rudi kwenye jukwaa lako la wakubwa siasa uziwezi.
Nipo kotekote. Mark my words CCM ijiandae kuwekwa kwenye majumba ya ukumbusho baada ya 25th Oktoba.
 
Tunahitaji kura za wahuni, wavuta bangi, machangudoa na wengineo walio kwenye muktadha huo
Kamanda nilidhani uliondoka na rais wetu wa miyoni Padre Slaa kumbe umemtosa umebakia kula kuku na fisadi.

Teh teh teh
 
Kabla ya kusifia huu uhuni jiulize, je wewe unaweza kwenda kwenye mkutano wa mgombea usiyemtaka kwenda kuimba jina la mgombea mwingine? Ukiona huwezi kufanya hivyo jiulize, what is wrong with these kids?
 
Kama ni kweli walimzuia.Ni kosa kisheria.Anayeamua mtu kuwa raisi ni mpiga kura.Huwezi zuia mgombea wa chama kingine na kumwambia tunamtaka mgombea wetu.Inaelekea hao waliozuia hawajui sheria wala chochote.Hivi magari ya washawasha yangewamwagia maji na wakawapiga virungui wangesema wanaonewa?

Huwezi zuia msafara wa chama kisicho chako au kuuingilia msafara wa chama kingine.CHADEMA elimisheni hao wahuni weni na wanywa viroba.CCM ikiamua kumfanyizia huyo mtu wenu msije piga yowe.

Jeshi la polisi nalo likakamae lisiachie ujinga kama huo ujirudie tena
Mbona mnalialia sana?
Safari hii hakuna kusaidiwa na polisi ni ki vyenu vyenu tu.
 
vizuri hao km wanaakili wangemkataa ndani ya box.. lakini huko ni kuonesha kuwa lowasa anasapoti ya wahuni pekee...

Hao mnaowaita wahuni ndio waliomkimbiza madarakani rais wa Burkina Faso, sasa anaishi uhamishoni kama house boy.
 
Kampeni ni kumsikiliza mgombea kama hata kumsikiliza hutaki endelea na mambo yako, wapo ambao watampigia kura magufuri wakazi wa hapo hapo, huo uhuni unaweza kuleta hali ya hatari pindi waupande wa pili nao wakianza kuleta ukinzani juu yao.
 
Huko Mbarali nasikia vijana wanakunywa viroba hatareee...hatushangai kwa tukio hilo.

Ila mbinu hizo hata CCM wanaziweza...hazina ishara nzuri ya kudumisha amani kama kila chama kitafanya hivyo...
 
Hao mnaowaita wahuni ndio waliomkimbiza madarakani rais wa Burkina Faso, sasa anaishi uhamishoni kama house boy.
Issue ya Burkina Faso na Tanzania hazina uhusiano wowote usichanganye mambo Tanzania ni nchi ya demokrasia wananchi ndiyo wanahamua.
 
Siasa za kuandaa makundi kwa ajili ya kuzomea, kurusha mawe n.k halafu mnarekodi mikanda ili kuirusha hewani kwamba ni kundi kubwa hii haiwez kutufikisha popote zaidi ya hao mnaowatumia mwisho wakikosa kazi watajitengenezea kundi lao la uhalifu...mmmh. Hawa hawana mapenzi mema na Taifa letu.
 
Kabla ya kusifia huu uhuni jiulize, je wewe unaweza kwenda kwenye mkutano wa mgombea usiyemtaka kwenda kuimba jina la mgombea mwingine? Ukiona huwezi kufanya hivyo jiulize, what is wrong with these kids?

Na uhuni wa kusema mgombea wa ukawa kajinyea unaona ni sawa? Dawa ya moto ni moto
 
Ujinga na upumbavu mtupu?

Hivi unadhani na watu wa Magufuli wakianza kufanya hiki kinachofanywa na wajinfa wakisaidiana na wapumbavu kutakuwa na amani katika kampeni za uchaguzi.

Mshukuru watu wa upande wa Magufuli ni wastaarabu na wanafahamu dhana ya kukubali kutokubaliana katika msingi wa demokrasia.

ndo chanzo cha vurugu
 
Ni uhuni ambao unapunguza kura za ukawa toka kwa watu wastaarabu. Kama wewe umeshaamua unamtaka Lowassa huna sababu ya kwenda kupiga kelele kwenye mkutano wa Magufuli.

Matusi yalizaliwa CCM, matusi kwao CCM vitendo kwao UKAWA.
 
Back
Top Bottom