Elections 2015 Magufuli akutana na nguvu ya Umma Mbeya, azomewa, aambiwa wanamtaka Lowassa

Elections 2015 Magufuli akutana na nguvu ya Umma Mbeya, azomewa, aambiwa wanamtaka Lowassa

Hiyo siyo nguvu ya umma ila ni uhuni.

Uhuni mtu yeyote akiamua anaweza kuufaya, lakini matokeo yake ni kuvujika kwa amani.

Kama wao wameshaamua kuwa wanamtaka Lowassa nini kinawapeleka kwenye mkutano wa Magufuli?

Inaonekana kabisa kuwa kuna kundi lililojiandaa kufanya fujo na walishaandaa camera wapige hii picha ya video.

Ukawa badala ya kuchekelea vitu kama hivi inabidi mvikemee kwa sabau watanzania hawapendi vurugu, hawatamchagua mtu anayeandaa vikundi vya vurugu.

Ni uhuni kama ule TBC wanavyosoma magazeti kizushi
 
Hao ni vijana wanaopangwa kuleta fujo. Sasa wa CCM nao wakiwaletea fujo tutabaki? Chadema use common sense. Matusi kwenu na kila kitu.Huwezi kushinda kwa kuhonga na propaganda za hivyo.

Hawakuletwa na malori lskini! Ila amewakuta wamejikalia zao njiani wakiwa hawana ajira ya uhakika ma labda wakiwa wanawakimbia mgambo
 
Ujinga na upumbavu mtupu?

Hivi unadhani na watu wa Magufuli wakianza kufanya hiki kinachofanywa na wajinfa wakisaidiana na wapumbavu kutakuwa na amani katika kampeni za uchaguzi.

Mshukuru watu wa upande wa Magufuli ni wastaarabu na wanafahamu dhana ya kukubali kutokubaliana katika msingi wa demokrasia.

Mkuu this is just politik, angalia usijepata BP ukaanza kuuza mafuta...teh teh
 
Watu wanaongelea fujo na vurugu?!
But mi hapo sijaona dalili ya vurugu zaidi ya ushabiki. Ushabiki ni kitu cha kawaida kwenye mazingira kama haya
 
Mbowe na mpuuzi mwingine Sugu ni tatizo sana sijui kwanini hawa jamaa wa CDM/UKAWA wanamkubali kiongozi wa ovyo na bogus kama yule.

Watu wanatumia nguvu nyingi sana kufanya huu uchaguzi uwe wa kidemokrasia; nakuhakikishia uwezi kuwasikia viongozi wa UKAWA kutoka na kukemea hivi vitu ambavyo vinaweza lipuka muda wowote ni viongozi wa CCM tu wako makini kwenye kuzuia mambo kama haya kuweza kuzalisha fujo za papo kwa hapo.

Wameshaambiwa sana kama mkutano unaona si wa kwako na utaki kumpigia mtu kura usiende kuliko kujitokeza kwa malengo ya vurugu; yaani wanatakiwa wapigwe hawa kushinda kibano cha Mtwara wote na waliomzomea Haji Duni pia Nzega.

Vipi yule alitemdhalilisha Lowasa eti alijinyea Ccm ilishatoka kumkemea.

Ccm wameasisis siasa chafu na wao ndio watakao umia
 
UKAWA mjifunze siasa za kuvjmiliana. Kama tukiendekeza zomea zomea sijui kama tutafanikiwa kimaendeleo. Ndo maana wenye akili wanawakimbia. Wanabaki wajinga tu na malofa

Mbona ccm ndio wamejaa hao mapumb na malofa wacha kukebehi watu
 
Umati upi hao ni wahuni tu wanafanya fujo kama mnamtaka Lowassa na mnajiamini si msubiri siku ya kupiga kura.

Ungewapa ccm ushauri huo. wanatukana matusi ya nini kama hawamtaki lowasa si wasubiri tu tar. 25?
Lowasa kawachagulieni magufuli akaondoka zake bila matusi lakini wenzenu kila kukicha wanamtukama tu lowasa. Au wanamtukana ili kupunguza hasira kwa kuwachagulia magufuli halafu akaondoka kwenda upande wapili!?
 
Hao ni vijana wanaopangwa kuleta fujo. Sasa wa CCM nao wakiwaletea fujo tutabaki? Chadema use common sense. Matusi kwenu na kila kitu.Huwezi kushinda kwa kuhonga na propaganda za hivyo.

Wa kuhonga ni chadema tena? Sisi malofa hatuna hela za kuhonga bana hela za kununuwa watu ziko ccm.
 
Hawakuletwa na malori lskini! Ila amewakuta wamejikalia zao njiani wakiwa hawana ajira ya uhakika ma labda wakiwa wanawakimbia mgambo

Wanajikalia bila kufanya kazi, halafu ndio wanaleta vurugu za kihuni namna hiyo. Kama wanahitaji lowasa wasubili kura. Kupiga kelele kwa kuhongwa kutakusaidia nini. Chadema kuna kitu kimemisi somewhere kilikuwa chama flesh sasa kinakuwa na kuongozwa na wahuni.
 
[9/27, 13:58] Zawadi Beatus: Sasa hii ajabu yaani Mh Magufuli amezomewa na vijana wa mjini kijiweni waliochoka na ahadi za mama kuku mwanangu utanyonya kesho mnaanza kutafuta mchawi upinzani. Hao vijana ukiwafuatilia utakuta hawana kadi za chama chochote si chadema wala ccm ni watanzania. Badala ya kukaa chini kujitafakari kwanini vijana hawa makapuku, masulupwete wavaa malapulapu wanatuzomea mjirekebishe mnaanza kuwanyooshea vidole wapinzani, jeshi mnalo, taasisi za utafiti mnazo mngewaomba hata twaweza wafanye utafiti kwanini mnazomewa basi, serikali ipo chini yenu, kodi zote mnakusanya nyie, bajeti mnapanga nyie. Hivi hao vijana wangekuwa wamepewa ajira some where kwenye kiwanda wangeacha kazi kuja kuwazomea? Tujitafakari!!!!
[9/27, 14:03] Zawadi Beatus: Mimi nashangaa hivi mfanyakazi wa benki kwa mfano anapata wapi muda wa kwenda kumzomea Magufuli? Vijana watafutiwe suluhisho kikwete aliwaahidi ajira angetekeleza angeona kama Magufuli angekuwa anapata tabu
 
Hao ni vijana wanaopangwa kuleta fujo. Sasa wa CCM nao wakiwaletea fujo tutabaki? Chadema use common sense. Matusi kwenu na kila kitu.Huwezi kushinda kwa kuhonga na propaganda za hivyo.

Kweli wewe ni mfungwa, hauhitaji tafiti za Twaweza kujua kwamba Wananchi Wamekichoka CCM, hata ninyi mnaofaidika na ufisadi wao mkiitetea hamtashinda, hakuna siku Nuru ilishindwa na giza,,,

CCM OUT
 
Pro-Chadema kuweni wavumilivu October 25 siyo mbali kama mnaamini nyie ni nguvu ya umma subirini mpige kura siyo kuleta fujo kwenye mikutano ya vyama vingine.

Hata kama hamkubaliani na huyo mgombea fujo za nini wafuasi wao nao wakijibu kwa mgombea wenu mtakuwa wavumilivu.

Fanyeni siasa za kistaarabu msiwe malofa.
 
Hiyo siyo nguvu ya umma ila ni uhuni.

Uhuni mtu yeyote akiamua anaweza kuufaya, lakini matokeo yake ni kuvujika kwa amani.

Kama wao wameshaamua kuwa wanamtaka Lowassa nini kinawapeleka kwenye mkutano wa Magufuli?

Inaonekana kabisa kuwa kuna kundi lililojiandaa kufanya fujo na walishaandaa camera wapige hii picha ya video.

Ukawa badala ya kuchekelea vitu kama hivi inabidi mvikemee kwa sabau watanzania hawapendi vurugu, hawatamchagua mtu anayeandaa vikundi vya vurugu.

Siku zote munge kuwa na mawazo na akili kama hizi na mukaweza kuzisimamia kwa vitendo mungekuwa watu wa maana sana na amani isingekuwa inavunjika.

Mnajifanya kuwa ni watu mnaojali amani lakini ndio ninyi wenyewe mnaowaua wapinzani kwa mabomu,mnajifanya mnapenda amani lakini ndio ninyi wenyewe mnaotuma polisi kuwapiga wapinzani.

Mnajifanya watu wa amani lakini ndio ninyi wenyewe mnaoandaa maandamano feki kwa kuwatumia vijana kuandamana mpaka ofisi za vyama vya upinzani huku mkitumia vyombo vyenu vya habari kusambaza uhuni mnaoufanya.
 
Back
Top Bottom