Aljazera
JF-Expert Member
- Feb 11, 2015
- 637
- 224
Maana ya ICU ni nini? Kwanini mgonjwa atolewe ward ya kawaida apelekwe ICU? Mazingira ya chumba cha ICU liko be vipi?
Kuna chumba kinaitwa HDC=High Dependency Care(Chumba cha Wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu/huduma tegemezi)
Mgonjwa anaekua kwenye hiki chumba anakua hajiwezi kufanya chochote bila msaada toka kwa muuguzi na ni lazima awe na mpira wa kukojolea na wengi wao wanalishwa kwa kutumia mpira unaopitishwa puani.Kila Wodi katika Hospitali ya Bugando ina hiki chumba tena kinatazamana na Ofisi ya wauguzi.
ICU=Intensive Care Unit (Kitengo cha Huduma Kubwa) Hiki chumba katika Hospitali ya Bugando kiko wodi na2 na ni karibu kabisa na Chumba cha upasuaji na Idara ya Dharula.
Jina lingine maarufu la hicho chumba alichopelekwa Kigoda(R. I. P) kinaitwa Chumba cha Bahati Nasibu kiukweli ni Wagonjwa wachache sana wanaopelekwa kwenye hicho chumba wanatoka salama wengi wao hufariki. Wagonjwa wote waliolazwa humo wanapumulia Mashine ambazo zikileta hitilafu tu kwa muda mfupi Uhai wao unakua mashakani.
Sasa huyu Magufuli anapolidanganya Taifa kua aliwasiliana na Marehemu kabla na akiwa ICU ana maana gani?
Sasa fikiria mgonjwa anaeihitaji uangalizi maalumu hawezi kufanya chochote kile bila kusaidiwa ingawa anakua ajitambua kwa kiasi flani je huyo aliyeko ICU ambae kwa asilimia kubwa anaendelea kuishi kwa msaada wa mashine atawezaje kutumia Simu au Laptop tena simu yenyewe Smartphone?
Jamani mambo mengine tusipende kufanya Siasa tu?